Nahitaji msaada wa kifedha, nimekwama

mkuu kweli umesoma thread yangu vizuri?? samahan lakin! vifaa vyote ninavyo mkuu kama brender,juice dispenser,freezer etc ila kinachofanya pesa ionekane ni nyingi ni kwa sababu ya kodi tu! na unajua ni lazima uwe na sehemu ya kuishi kwanza kabla ya yote Mkuu! na kama isingelikuwa kodi kukalibia kuisha siku chache zijazo ningepambana taratibu bila hata kuja kuomba hapa!
mkuu sio kila anateomba ni mjinga,muhuni,mvivu au tapeli! saa nyingine ni mambo yanaingiliana tu! natamani unelielewa hali niliyonayo sasa hivi!
Pia mkuu unajua mashine ya juice ni sh ngapi??? unafikir ni bei rahisi tu? mbona inazidi hata pesa niliyoomba kukopeshwa hapa?? Mkuu mambo mengine ni vigumu kuyaelezea
 


Mkuu, chukua LIKE 800! umeonesha busara, hekima, na uungwana. Unayaelewa MAISHA vyema.

-Kaveli-
 
Mleta mada, hebu changamkia hiyo fursa aliyokupa dada Miss Natafuta . Kama kwenye kibarua hicho utapata 15,000 per day, then miezi miwili utapata hiyo LAKI 6 unayohitaji. Miezi miwili siyo mingi kaka, siku hazigandi.

Sisi pia (najisemea mimi binafsi) hatuna kitu, tuna ungaUnga tu mjini hapa, ila tunaweza kukuchangia nauli na ya msosi kwa siku za kuanzia.

Kumbuka kuna vijana wengi tu (including mimi) hatupati fursa kama hizo, na tunazihitaji haswa ila kupata msamalia mwema wa kukuunganisha kama hivyo ni ngumu! Mimi binafsi, naona kupata elfu 15 per day ni fursa nzuri tu for start-up kwa sisi vijana ambao hatuna 'connection' wala 'network' hapa town, ukizingatia kwamba bado hujaoa na unaishi alone.

Mkuu usiache hiyo fursa.

-Kaveli-
 
mkuu nashukuru sana,we unaelewa maisha tuliyonayo vijana,miss natafuta nimeshamPM kumuelewesha vizuri maana naona hapa kwenye thread kuna watu wengine wana nia mbaya na wana mawazo finyu sana! nashukuru Mkuu
 
Mwanzo mgumu.....tufanye subira mwendokasi ni mkombozi wetu hapa Dar
 
Mkumbuke pia zege halimwagwi kila siku, pia zege likimwagwa linachukia siku 14 mpaka 28 kukauka sasa sijui inakuwa VP hapo.... Labda kuwe kuna kazi za aina nyingine
 
jamaa haeleweki msome vizuri mimi napenda mtu straight sipo nae tena
 
hapa mjini uaminifu ni kitu kikubwa sana siwezi kukupeleka kwa watu mtu huaminiki siku ingine naonekana mimi mzushi eti
unataka hela ya haraka si utaenda kuiba hata vitu site?
da!!!aiseee basi sawa dada tuishie tu hapa ila asante kwa challenge ulionipa!!
 
Mkumbuke pia zege halimwagwi kila siku, pia zege likimwagwa linachukia siku 14 mpaka 28 kukauka sasa sijui inakuwa VP hapo.... Labda kuwe kuna kazi za aina nyingine
mkuu kumbe umenielewa vizuri, japo hata hiyo ya zege sijaikataa ila nimesema tu kwa kuwa hili tatizo ni la haraka ndo maana nikaomba hata kama bado mtu yupo mwenye nia na uwezo nahitaji msaada wake wa kunikopesha hicho kiasi! na nikasema atakayehitaji details zaidi kama tataka kunisaidia aniPM, pia nikasema atakayetaka kunisaidia kwa riba nae anicheck tuelewane ila inashangaza pale watu wanapokuchukulia muhuni! ningekiwa muhuni basi hata nisingejitahidi kufight mpaka kuweza kununua vifaa nilivyonavyo kwa sasa! ila nimeamini hizi ni challenges watu waliofanikiwa wanazokutana nazo Mkuu
 
sijapenda kabisa hii comment yako kuwa ya kwanza
 
Mara Huna Hata Kitanda, Mara Nitaweka Rehani Vitu Vyangu. Una Vitu Gani Sasa? Naona Wewe Ni Msanii Tu. Pia Nakushauri Nenda Pride Au Finca, Wao Wana Mikopo Ya Vikundi, Na Dhamana Yake Weka Hivyo Vitu Vyako Vya Ndani
siyo vizuri kum discourage mtu, kama kutapeliwa tumeshatapeliwa wengi na tumeshafanikisha mengi, kuna hatua za kuweza kumjua mtu kama kweli una lengo la kumsaidia, omba yasikukute wewe.
 
Me nataka utuambie ukweli kuhusiana na alicho comment Losser bad....mara ulisema umemaliza chuo vizuri...mara uliishia mwaka wa pili....em tueleweshe kwanza hapo...
nimekuPM maana kwa sababu mwanzoni nilisema kama kuna mtu mwenye nia ya kunisaidia basi ili apate uhakika zaidi kama atataka kuniuliza chochote zaidi aniPM
 
Mkuu mimi nakushauri uendelee na juhudi zako za kutafuta huo mtaji wa sh 600,000. Usikatishwe tamaa na watu wanaokubeza na kukukejeli hapa. Mimi nimesoma ulichoandika na inaonekana kabisa wewe ni mtu uliye na shida na unatafuta msaada. Unajua sisi waafrika tukipata huwa tuna tabia ya kubeza wasio nacho. Kwa mfano kuna member mmoja anajiita Miss Natafuta yeye ameamua kukukebehi na kusema atakupa kazi ya zege. Hajajua status ya afya yako au variables nyingine nyingi zinazomwezesha mtu kufanya kazi ya kubeba zege. Sio kila mtu anaweza kufanya kazi ya kubeba zege. Na sio kila mtu anaweza kuuza juice. Mimi ni mchapakazi mzuri tu na kuna wakati nilipitia kwenye changamoto kama zako lakini hata ungenipa kazi ya kubeba zege kipindi hicho NISINGEFANYA. Yes, nisingefanya sio kwasababu mimi ni mvivu ila mwili wangu hauwezi kuhimili kazi za nguvu na mazingira kama hizo. Wewe fikiria je ni kila mtu anaweza kucheza mpira au kuwa daktari? Jibu ni hapana. Na nakushauri usitetereke bali kazania kitu unachofikiri utakifanya vizuri na kwa mafanikio. I wish ningekuwa niko kwenye nafasi ya kuweza kukusaidia ningefanya hivyo bila kinyongo. Ushauri wangu kwako ni: Usikikate tamaa. Wanaokukejeli achana nao. Endelea kuelezea shida yako kwa watu unaodhani wanaweza kukusaidia. Hata hii thread endelea kui-update. Nina uhakika mwisho wa siku utafanikiwa kwani penye nia pana njia. Nothing is impossible. Usione aibu kuomba kwa lengo maalum kama hili. Kuomba kubaya ni kuomba bila madhumuni na malengo maalum yenye tija.
 
hujui maisha niliyopitia mkuu siwezi kumkebehi mtu na shida zake
wewe msome vizuri huyu kijana anataka tu mkopo na mimi siwezi kumgeuzia malengo yako na ujue hakuna kazi mbaya kama kumdhamini mtu mahali akiharibu wewe ndo umeharibu
 
hiyo fursa ya kazi naomba unipatie mimi Miss Natafuta
Huyo naye ana kazi au anawayeyusha tu.Anaway kama mtu huwezi kumsaidia mtu unaweza tu kukaa kimya kuliko kumkatisha tamaa.Kumbuka leo kwake kesho pengine inaweza kua kwako.Si lazima ukose pesa kama yeye,kuna matatizo chungu nzima ambayo watu wanataabika nayo duniani.Kwahiyo usijione umefika kwa kua una pesa.Kijana pole kwa changamoto unayopitia na wewe usichague kazi.Mafanikio ya harakaharaka yana changamoto nyingi...
 
hujui maisha niliyopitia mkuu siwezi kumkebehi mtu na shida zake
wewe msome vizuri huyu kijana anataka tu mkopo na mimi siwezi kumgeuzia malengo yako na ujue hakuna kazi mbaya kama kumdhamini mtu mahali akiharibu wewe ndo umeharibu
mimi sina shida ya mkopo naiomba hiyo fursa ya kazi lakini huna muda na mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…