Nahitaji kupungua Mwili/ Kilo. Naumia sana

Mdigokhan

JF-Expert Member
May 2, 2022
843
1,923
Khabari zenu,

Nimekuwa mtu wa kujisikia vibaya sana nikiuangalia mwili wangu. Mimi ni kijana wa miaka 28, nina kilo 93.

Nimenenepa sana. Nina kilo nisizozipenda, nimetumia mbinu ya mazoezi Ila nahisi kushindwa cuz ratiba za kujitafutia ridhiki zinabana. Natamani Nipungue nifikie hata kilo 75.

Mwili unanifanya nikivaa sipendezi kabisaa. Shepu mbaya, nina umbo la Kiazi sieleweki. Kitambi kikubwa.

Kuna jamaa yangu aliwahi nambia ili nipungue kwa haraka niwe nakunywa konyagi na nivute bangi ila nimefanya hivyo hakuna matokeo yoyote zaidi ya kujiumiza kuwa mlevi tu (Nimeacha).

Mwili nadhani unafanya mpaka nikiwa na mpenzi wangu kitandani simfikishi maana dakika 2 tu nishakojoa. Naumia na hii hali. Naombeni mbinu jamani, najua kuna watu humu walikuwa kama mie au zaidi ya mie.

Kitambi ninacho, nina maziwa makubwamakubwa yaani aibu siipendii hii hali naumia sana.

Miaka kadhaaa nyuma nilikuwa kawaida tu. Sikuwa kama sasa ila nashangaa nazidi kufumuka mwili yaani mpaka nakuwa na kibamia.
 
Subiri wataalam zaidi waje.
Ushauri wangu simple, jaribu intermittent fasting, wiki 2 za mwanzo itakua ngum but after that ni ushindi tu. Na pia utapungua tarratibu kistaarabu.
Ukishindwa, then temana na wanga 100% ili mwili uchome mafuta yote fasta.
 
Khabari zenu...

Nimekuwa mtu wa kujisikia vibaya sana nikiuangalia mwili wangu...Mimi ni kijana wa miaka 28 Nina kilo 93...

Nimenenepa Sana Nina kilo nisizozipenda, nimetumia mbinu ya mazoezi Ila nahisi kushindwa cuz Ratiba za kujitafutia Riziki Zinabana...Natamani Nipungue Nifike hata kilo 75...

Mwili Unanifanya nikivaa Sipendezi kabisaa, Shepu mbaya Nina umbo la Kiazi Sieleweki...Kitambi kikubwa...

Kuna jamaa yangu aliwahi nambia ili nipungue kwa haraka niwe nakunywa KONYAGI na nivute BANG$ ila nimefanya hivyo hakuna matokeo yoyote zaidi ya kujiumiza kuwa mlevi tu(Nimeacha)

Mwili nadhani unafanya mpk nikiwa na mpenzi wangu kitandani Simfikishi maana dakika 2 tu nishakojoa... Naumia na Hii hali Naombeni mbinu Jamani najua kuna watu humu walikuwa kama mie au zaidi ya mie...

Kitambi ninacho, nina maziwa makubwamakubwa Yani aibu siipendii hii hali naumia sana...

Miaka kadhaaa nyuma nilikuwa kawaida tu Sikuwa kama sasa ila nashangaa nazidi kufumuka mwili Yani mpk nakuwa na kibamia...

Uzi na picha....View attachment 2646189
Duh! Hapo kukimbia huwez kaka? Mana ukitaka asubuhi na mbio km 5 mwez wako mmoja tu. Kwisha kaz
 
Daaahhh pole sana
Subiri madaktari waje
Dr Restart njoo huku umwambie mwenzio kitambi umekiondoaje
Hahaha!. Dawa ya uhakika ya kupunguza kitambi ni kupunguza kiwango na aina ya vyakula na vinywaji.

Mazoezi pia yanasaidia sana lakini uwe na commitment nayo. Ukiacha tu unafutuka zaidi ya awali.

Angetuambia ratiba yake ya chakula na aina tungemuambia apunguze nini. Ila vyakula vya wanga vinaongeza sana uzito. Matumizi ya vinywaji vya sukari (soda), vivyo hivyo.

Matumizi ya bangi na vilevi ndo vibaya zaidi. Bia zina kiwango kikubwa cha wanga. Ukinywa tu, kilo hizo.
Aachane kabisa na matumizi ya bangi na pombe. Kamwe havitapunguza uzito. Labda baada ya kuugua, kilo zitapungua.
 
Khabari zenu...

Nimekuwa mtu wa kujisikia vibaya sana nikiuangalia mwili wangu...Mimi ni kijana wa miaka 28 Nina kilo 93...

Nimenenepa Sana Nina kilo nisizozipenda, nimetumia mbinu ya mazoezi Ila nahisi kushindwa cuz Ratiba za kujitafutia Riziki Zinabana...Natamani Nipungue Nifike hata kilo 75...

Mwili Unanifanya nikivaa Sipendezi kabisaa, Shepu mbaya Nina umbo la Kiazi Sieleweki...Kitambi kikubwa...

Kuna jamaa yangu aliwahi nambia ili nipungue kwa haraka niwe nakunywa KONYAGI na nivute BANG$ ila nimefanya hivyo hakuna matokeo yoyote zaidi ya kujiumiza kuwa mlevi tu(Nimeacha)

Mwili nadhani unafanya mpk nikiwa na mpenzi wangu kitandani Simfikishi maana dakika 2 tu nishakojoa... Naumia na Hii hali Naombeni mbinu Jamani najua kuna watu humu walikuwa kama mie au zaidi ya mie...

Kitambi ninacho, nina maziwa makubwamakubwa Yani aibu siipendii hii hali naumia sana...

Miaka kadhaaa nyuma nilikuwa kawaida tu Sikuwa kama sasa ila nashangaa nazidi kufumuka mwili Yani mpk nakuwa na kibamia...

Uzi na picha....View attachment 2646189
Nikiwa na miaka 10++ nilikuwa mnene sana ila baada ya kuingia boarding nilipungua sana.. kilichonikuta ni limit ya chakula nilichokuwa nakula, maana asubuhi ni uji mkavu, mchana ugali na haushibi, usiku ni ugali na haushibi kivile (wale tulosoma shule za katoliki maharage kama Karanga), nachotaka kusema ni kuwa kupunguza mwili hakuna namna zaidi ya kuwa na discipline, jaribu kujiasses kwa siku unakula vyakula gani, na hakuna shortcut, kupunguza mwili ni jambo linalohitaji nidhamu sana

Pia jitahidi usinywe beverages kama soda, energy, apple punch n k hizo zinaongeza sana mwili asikwambie mtu

Kuhusu mazoezi usifanye mazoezi ya kujiumiza sana, mazoezi pekee ambayo ni salama ni jogging, jogging ya nusu saa deile inatosha kukufanya uwe na mwili wa kawaida kama ukimantain kwa mwezi mzima

Narudia tena hakuna shortcut ya kupunguza uzito inahitaji discipline ya kutosha
 
Mkuu

Umeanza ku panic wakati sahihi kabisa so kazi ya kupungua itakuwa rahisi zaidi

Kupungua start from the will as sio kitu kirahisi but kanuni kuu ni 2 tu

1. Punguza sana kula, kunywa maji sana, matunda na mboga mboga acha kabisa sukari na wanga
2. Mazoezi ni lazima kwenye kupungua vizuri na si hiyari so acha kisingizio cha ratiba, mimi huwa nafanya mazoezi kishingo upande sana kuanzia 2000h mpaka 2100h

Mengine ngoja madaktari waje
 
Back
Top Bottom