Nahitaji Kujiunga na upadre

Nahitaji Kujiunga na upadre

Kwa hiyo itakuwa ngumu kupokelewa??
Mdogo wangu kamaliza form six mwaka jana amejiunga tayari yupo malezi huko analelewa,Mkuu usikafe tamaa utafanikiwa nakwambia jaribu kuulizia padre yoyote aliyepo karibu yako
 
Nimeutumikia Upadri kwa takriban miaka 9 hakuna cha maana kule.
Afu kwanini mapadre mnaongoza kwa magonjwa ya kisukari? Nini tatizo? Nimeona mapdre wengine mpaka wanatembea na vitunguu maji mfukoni kwa ajili ya kutafna mda wote!
 
Nakumbuka siku navua joho la Upadri pale Parokia ya Itigi Singida wale masista walibaki midomo wazi. Nikavua lisanamu la msalaba shingoni nikalitupa pale kwenye sakafu, nikasema Bismillah nikasepa. Hawakuamini!!

Walinibembeleza kama mtoto nirudi Parokiani, mpaka wakakata tamaa.

Mpaka leo kuna waumini hawaamini kama nimeshaukimbia ukatoliki.
Nimehudumu parokia kibao. Kuanzia Itaga Tabora, Nikaenda Kipalapala, Nikahamia Geita, Askofu Aloysis Balina akaniita pale Ngokolo Shinyanga, mwisho nikamalizia Itigi Singida (kabla sijaifuata dini ya haki).

Al Islam Huadin Ulladhy Baa Sallahu Bih
Mkuu mpaka geita? Unamfahamu father masolwa? Ni zaidi ya mwanajeshi huyo padre amenichapa fimbo sana nikiwa kwenye mafundisho ya miito mitakatifu! Ukipanda gari lake bila ruhusa yake anakupeleka kijiji tofauti na kwenu afu anakwambia shuka!
 
Yaani hiyo interviews najua kuna member hata hamjawahi kuona hizo mambo mnataka kudesa kwangu.....
Usikate tamaa, mapadre wamekua wachache sana siku hizi, wataku accodate tu, ikizingatiwa una 1st degree tayari. Ila tegemea 6yrs minimum huko.
 
Naomba kupata mawasiliano ya mashirika mbalimbali ya mapadre ambayo naweza kujiunga nayo.

Kiwango cha elimu yangu nina degree moja na umri nina miaka 24.
Natamani kumtumikia Mungu katika utume huo.
Kwa sasa nipo Dar es Salaam

Kuna mashirika ya upadre kadhaa hapa Dar es Salaam. Kwa kuanzia, waone maparoko wafuatao:

1) Parokia ya Kimara (Calretian Fathers)
2) Paroko wa Mbezi Beach - Gasper de Buffalo (Damu Azizi ya Yesu)
3) Paroko wa Yombo Vituka (Wakamiliani - Wa hudumu wa Wagonjwa)
4) Paroko wa Hananasifu (Holy Spirit Fathers)
 
Upo vizuri mkuu, ngoja niwacheki hao wa hananasifu
 
Usikate tamaa, mapadre wamekua wachache sana siku hizi, wataku accodate tu, ikizingatiwa una 1st degree tayari. Ila tegemea 6yrs minimum huko.
Miaka ya kusoma sio shida maana mm kusoma ndo napenda na kuwa na privacy na Mungu
 
Mdogo wangu kamaliza form six mwaka jana amejiunga tayari yupo malezi huko analelewa,Mkuu usikafe tamaa utafanikiwa nakwambia jaribu kuulizia padre yoyote aliyepo karibu yako
Kweli mkuu, kuna wanao katisha tamaa na wengine wanatia moyo
 
Kanisani unaenda kweli ww?!
Jumuiya unasali!? Unasali jumuiya gani?
 
Naomba kupata mawasiliano ya mashirika mbalimbali ya mapadre ambayo naweza kujiunga nayo.

Kiwango cha elimu yangu nina degree moja na umri nina miaka 24.
Natamani kumtumikia Mungu katika utume huo.
Kwa sasa nipo Dar es Salaam
Please nitafute huku, nikuunganishe ndugu
 
Mkuu kama unataka kuwa Padre, una degree na bado mashirika yao umeshindwa kuyajua basi nakushauri usiende huko, huna wito. Yaani hata padre wako umeshindwa kuongea naye akaku-guide? Hata huko kanisani unaenda kweli?
dah umesema jambo la msingi sana kaka, huyu hana wito aache tu, pengine hata kutumikia kanisani hakuwahi, unakuja kuomba msaada jr, huna paroko,katekista wala viongozi wa kiroho hapo kanisani, kaka mashirika ya upadri si kama vyuo vya kawaida. wewe sidhani kama utaweza kusoma miaka 8-10 ya upadri
 
Ushahuri mzuri, ila ndo kuanza kujipendekeza wengine hatujazoea ila taratibu mambo yataeleweka. Ila nilitaka nipate connection ya moja kwa moja
wewe kwa majibu haya huwezi kuwaa padri. kanisa halihitaji watu wanaoenda huko kwa kuogopa changamotoa za maisha. upadri unafuata filtration system kubwa sana ,lazima uanzie chini kwenye jumuia na parokia yaoko, siyo JF
 
Nina mengi ila naona utakata tamaa mapema. Elewa 8 kati ya 10 ya unaowaona mapadre sio mapadre. Pa kuanzia nenda kwa paroko wako akupe miongozo vizuri kwani kila shirika lina mtindo au karama tofauti.
 
Mkuu kama unataka kuwa Padre, una degree na bado mashirika yao umeshindwa kuyajua basi nakushauri usiende huko, huna wito. Yaani hata padre wako umeshindwa kuongea naye akaku-guide? Hata huko kanisani unaenda kweli?
Ajira zimekuwa ngumu, upadri sio ajira bali ni wito was kujitolea ...Nakuunga mkono.
 
Back
Top Bottom