Ndugu wadau nilikuwa naomba ushauri wenu nipo kwenye ajira ya uwalimu kutokana na. Mda nilioka nahitaji kubadilisha kutoka uwalimu kwenda uhamiaji au Computer science au ICT katika wizara yoyote au hata ndani ya Elimu hiyo hiyo nina level ya Elimu shahada BAED naomba ushauri wenu nifanyeje ili nitimize malengo maana hivo ndio vitu ambavyo nilitaman kuvifanya tangu nakuwa ila kutokana na familia zetu na mambo ya mkopo wa chuo nikajikuta nimeangukia kwenye Uwalimu
Naomba kuwasilisha
Sikia huu USHUHUDA labda UTAWEZA kukusaidia..
Niliajiriwa Idara x katika halmashauri z, nilikua na diploma.
Ila kiukweli Mimi nilipenda sanaa fani y.
Baada ya miaka 2 nika apply chuo course y na kuomba ruhusa ya masomo.
Nikaenda kusoma masomo ya fani y.
Nikaunga na masters kabisaa ya fani y.
Nilivyorudi kutoka masomoni nikahamishiwa bomani kutoka kijijini nilipokuwa naitumikia fani x, nikawa mfanyakazi wa Idara y bomani.
Nikakuta mkuu wa Idara y amepata shavu la kwenda kusoma phD ulaya, hivyo nikawa na kaimu huku jamaa ananifundisha kazi.
Nasubiri mwezi wa 7 kufanyiwa RECATEGORIZATION ili niwe mkuu wa Idara kamili wa y.
Then na wewe.....
Nenda chuo kasome bachelor ya IT then maliza.
peleka Cheti kwa utumishi wako subiri RECATEGORIZATION.
Huku unasubiri kubadilishiwa muundo.
Ukimaliza unaweza kuwa unatafuta Kazi kwengine kupitia ajira.go.tz au wizara ya utumishi huwa wanapost nafasi kibao za kufanyia Kazi UN na AU na kwengine huko (int. Org) kwa watumishi wa umma..
Chukua hatua....
Mimi nilichukua hatua, sikutaka ndoto zangu zife.
Sikuipenda Kazi x, umasikini wa nyumbani ulinifanya nikaisomee na kuajiriwa serikalini ili tu nitoke kwenye mikono ya kulelewa na ndugu.
Sikuacha ndoto zangu za kuwa y KUFA.
#YNWA