Nahitaji kuacha kunywa pombe

Nahitaji kuacha kunywa pombe

ICD 10 ina ongelea alcohol dependency, ni tatizo kubwa ila sasa kuingia kwenye sonono ndio kitu kikubwa sana.

Tafuta AA ya karibu ita saidia
 
mm nliamua tu nliamka na hangova moja iyo ya kvant na hansonchoic ilntesa mpaka mchana nkaenda shop nkanunua hanson mbil moja nikainywa kwa shida sana nlvyomlza ile ya pl skuifungua nkaanza kurud hom uku najiulza faida za mateso haya nkaipga chin ile mpya nkasema kwanzia leo snyw tena pombe nashukuru Mungu ile apetite ya pombe imekata kabsaaa
 
Easy tu mkuu, siku ukilewa alaf majamaa wakakubeba wakaenda kukupelekea moto nakuhakikishaia hauwezi kunywa pombe tena. Jaribu hii njia
 
Mimi mwenyewe ina nitesa sana. Ila naamini kuna sikua nitaacha.

Ukitambua kwamba ni tatizo (wanaita insight) tayari upo kwenye asilimia kubwa ya kupata suluhisho.

Kukosa usingizi (insomnia) ni sehemu ya withdraw syndromes pamoja na kupata maruweruwe, kwa mfano mimi napataga hallucinations kabisa, kuona vitu visivyo na uhalicia.

Rehab zipo ila principles ni hizo hizo watakuambia lazima nia itoke kwako ili uweze kuacha, lazima utayari utoke ndani yako.

Kama una hisi hali ni mbaya sana chukua likizo kazini nenda rehab, au kama uko dar kuna AA groups za jioni, haya ni mafunzo maalumu mnakutana walevi na kushauria na kuna kua na mwalimu wa follow up.

Kuhusu maruweruwe kuna hizi dawa za benzodiazepines huwa zina uzwa kwa cheti cha daktari kwa kua ukizoea zina sababisha uraibu nazo, mimi hua na tumia 'clonanzapine' kwa dar huwa unaweza pata pharmacy bila masharti magumu. Tumia kwa muda mfupi maruweruwe yataisha na utapata usingizi ila usiruhusu zikuzoee.

Pata muda wa kufanya mazoezi baada ya kutoka kazini ukichoka utalala tu na itapunguza muda wa kukaa bila kitu cha kufanya na hauta waza pombe.

Kama kuna kitu kina kuletea sonono tafuta usuluhishi, fanya sana ibada au yoga au gym. Watu wanao kuletea mawazo hasi achana nao.

Ila mwisho wasiki lazima kiwe ni kitu kina toka ndani yako, uamuzi wa ndani kabisa utoke kwako na kwa nia moja. Madaktari wa sober au kufungiwa ndani haisaidii bila kuamua kwa dhati.
Asante sana nilikuwa nasubiri majibu kama yako, ubarikiwe sana
 
pombe imeniludisha nyuma sana tena sana,achana nayo nina mwaka na nusu sijagusa nahisi naelekea kuweza kuiacha lakn pia nilitumia dawa za kienyeji na nilidhamiria kuacha kabisa.
Hizo dawa ulipataje mkuu?
 
Back
Top Bottom