Nahitaji kuacha kunywa pombe

Nahitaji kuacha kunywa pombe

🇹🇿Kwanza hongera sana kwa kuweza kulitambua tatizo na kuanza juhudi za kupambana na tatizo mwenyewe. Hapo umeshafanikiwa kupona ugonjwa huo kwa asilimia 80

🇹🇿 Ni kweli pombe na ulevi mwingine vimewaharibia watu maisha yao sana. Kuna watu walikuwa na akili nyingi sana kazini ila wamefukuzwa kazi kwa sababu ya ulevi uliopindukia, kuna watu wamefariki dunia mapemba kwa.kuharibu viungo vyao vya ndani kwa sababu ya pombe kali, kuna watu wamevunja ndoa zao kwa sababu ya ulevi, kuna watu.wameuawa kwa kuhisiwa ni wezi usiku wakitoka kwenye ulevi

🇹🇿 Mlevi ni mbinafsi na huitesa familia yake, asilimia kubwa ya mapato huitumia kunjwa na wanaoitwa marafiki na nyumbani asilimia ndogo tuu ya mapato hutumika

🇹🇿 Ukiona kitu fulani kinafurahisha sana mwili wako ujue kinakutafuna ndani kwa ndani, maumivu yake utayasikia baadaye. Huwezi kuwa myumwa wa mwili na.ukiona kitu kimepingwa sana na mila , na dini usikijaribu maana ukikijaribu utavutiwa na kukiacha utashindwa ndiko shetani alikojificha

🇹🇿 Usidanganyike na watu wanaokunjwa lakini mambo yao yapo safi, Miili yetu imeumbwa kwa udongo tofauti. Kuna wachache wenye uwezo wa kuhimili vilevi ila wengi ulevi huwa ndio vyanzo vya matatizo yao ya ndoa, ukoo , dini , kazi na familia

🇹🇿 Ukiacha ulevi unapoteza kundi kubwa la marafiki ambao unadhani walikuwa ni washauri wako na wengine wanakupa mchango/ ramani ya kazi lakini amini usiamini ukiacha ulevi unapata marafiki wapya wema na wazuri, utaanza kuaminika kazini, nyumbani na vikao vya watu wa busara

🇹🇿 Kuna watu kama mimi niliamka tu siku moja nikasema kuanzia leo pombe basi. Nina miaka zaidi ya 20 sasa tangu niache, niliteseka kwa muda ila iliisha nikahamia kuwa adicted wa soda mwakahuu ulipoanza nikasema bas na hadi leo nimeacha soda

🇹🇿 Nadhani naamini kuna baadhi ya koo wana laana ya kutokunywa pombe na ukijaribu kunywa inainhia kichwani na kukuletea uchizi, wapo watu walitegemewa sana na familia zao ila pombe ndio hivyo imeharibu mfumo mzima wa maisha yao

🇹🇿🇹🇿 Sina ushahidi nimewahi kusikia kuna ushirikina wa kulogewa pombe ambapo utakuwa mlevi hadi pombe zikuue na nasikia kuna dawa za kienyeji unaweza kuchanganjiwa kwenye pombe ukatapika vitu vya ajabu na kuanzia hapo utakuwa umeacha pombe kabisa na ule uchizi wa pombe unaisha na kurudia akili zako
Mkuu hongera kwa kuacha, watu wengi wanateseka
 
Pombe haina shida ukinywa kiasi.. kwa week unatenga siku moja ya kunywa pombe na marafiki zako...

Kila kitu ukikifanya kwa kiasi kinaleta afya.. na kitu chochote ukikifanya kwa kupindukia inakuletea matatizo kwenye familia yako na maisha yako kiujumla..

Kunywa soda sanaa au juice tatizo hilo, kusali sanaa na kusahau kazi ni tatizo hilo hela zako atakula zote nabii...

Kila kitu afanye kwa kiasi

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
Swala linaanzia apo kwenye kiasi, nina ndugu yangu zamani alikuwa anakunywa jumapili pekee, saivi amekuwa chakari anakunywa mda wote mapombe machafu
 
Ukiamua kwa dhati unaacha, mimi ni shuhuda kupitia mimi mwenyewe. Nimekunywa sana kwa zaidi ya miaka 20 na sasa najisikia huru huu naenda mwezi wa 4, au hesabu nzuri ya muda nilioacha hesabu tangu siku ya mechi ya AFCON kati ya Egypt na Senegal waliofikia mikwaju ya penati ndio siku niliyokunywa kwa mara ya mwisho. Najichanganya nao rafiki zangu ambao wanakunywa na hata raundi nawaagizia lakini hata mzuka wa kutamani sina kabisa, hawaamini macho yao. Kwa kweli najisikia niko huru sana na hata baadhi ya mambo ya kazi nayazingatia kwa wakati, imani kwa wadau imeongezeka sio kama nilivyokuwa nakunywa, kwa ujumla nimegundua kuwa "pombe zilinichelewesha sana.." (in Magu's voice - RIP).
 
Punguza kunywa pombe ndugu uwe unakunywa asteaste usiache kabisa. Pombe inaongeza akili.
 
Ukiamua kwa dhati unaacha, mimi ni shuhuda kupitia mimi mwenyewe. Nimekunywa sana kwa zaidi ya miaka 20 na sasa najisikia huru huu naenda mwezi wa 4, au hesabu nzuri ya muda nilioacha hesabu tangu siku ya mechi ya AFCON kati ya Egypt na Senegal waliofikia mikwaju ya penati ndio siku niliyokunywa kwa mara ya mwisho. Najichanganya nao rafiki zangu ambao wanakunywa na hata raundi nawaagizia lakini hata mzuka wa kutamani sina kabisa, hawaamini macho yao. Kwa kweli najisikia niko huru sana na hata baadhi ya mambo ya kazi nayazingatia kwa wakati, imani kwa wadau imeongezeka sio kama nilivyokuwa nakunywa, kwa ujumla nimegundua kuwa "pombe zilinichelewesha sana.." (in Magu's voice - RIP).
Asante sana kwa kunipa uzoefu, naamini ntaweza. Jana nimemeza piriton nmelala vizuri
 
Piga chini kampani zote za tungi...
Oa..
Kama unakaa nyumba ya walevi hamaa...
Fikiri malengo mapya, kama huna nyumba anza ujenzi...kama huna watoto zaa...
Usikae na hela ambayo haina kazi...
Anza dose ya kutoa sumu ya pombe mwilini...
 
Ushauri mzuri sana ila nashauri ndugu zake wachonge jeneza ili siku akilewa sana akalala fofofo aamke akiwa kwenye jeneza na hao ndugu zao waekti kama wanalia huku wamevaa nguo nyeusi. Hatarudia tena kunywa kilevi hata pilipili ataiogopa akizan hulewesha
😂
 
🇹🇿Kwanza hongera sana kwa kuweza kulitambua tatizo na kuanza juhudi za kupambana na tatizo mwenyewe. Hapo umeshafanikiwa kupona ugonjwa huo kwa asilimia 80

🇹🇿 Ni kweli pombe na ulevi mwingine vimewaharibia watu maisha yao sana. Kuna watu walikuwa na akili nyingi sana kazini ila wamefukuzwa kazi kwa sababu ya ulevi uliopindukia, kuna watu wamefariki dunia mapemba kwa.kuharibu viungo vyao vya ndani kwa sababu ya pombe kali, kuna watu wamevunja ndoa zao kwa sababu ya ulevi, kuna watu.wameuawa kwa kuhisiwa ni wezi usiku wakitoka kwenye ulevi

🇹🇿 Mlevi ni mbinafsi na huitesa familia yake, asilimia kubwa ya mapato huitumia kunjwa na wanaoitwa marafiki na nyumbani asilimia ndogo tuu ya mapato hutumika

🇹🇿 Ukiona kitu fulani kinafurahisha sana mwili wako ujue kinakutafuna ndani kwa ndani, maumivu yake utayasikia baadaye. Huwezi kuwa myumwa wa mwili na.ukiona kitu kimepingwa sana na mila , na dini usikijaribu maana ukikijaribu utavutiwa na kukiacha utashindwa ndiko shetani alikojificha

🇹🇿 Usidanganyike na watu wanaokunjwa lakini mambo yao yapo safi, Miili yetu imeumbwa kwa udongo tofauti. Kuna wachache wenye uwezo wa kuhimili vilevi ila wengi ulevi huwa ndio vyanzo vya matatizo yao ya ndoa, ukoo , dini , kazi na familia

🇹🇿 Ukiacha ulevi unapoteza kundi kubwa la marafiki ambao unadhani walikuwa ni washauri wako na wengine wanakupa mchango/ ramani ya kazi lakini amini usiamini ukiacha ulevi unapata marafiki wapya wema na wazuri, utaanza kuaminika kazini, nyumbani na vikao vya watu wa busara

🇹🇿 Kuna watu kama mimi niliamka tu siku moja nikasema kuanzia leo pombe basi. Nina miaka zaidi ya 20 sasa tangu niache, niliteseka kwa muda ila iliisha nikahamia kuwa adicted wa soda mwakahuu ulipoanza nikasema bas na hadi leo nimeacha soda

🇹🇿 Nadhani naamini kuna baadhi ya koo wana laana ya kutokunywa pombe na ukijaribu kunywa inainhia kichwani na kukuletea uchizi, wapo watu walitegemewa sana na familia zao ila pombe ndio hivyo imeharibu mfumo mzima wa maisha yao

🇹🇿🇹🇿 Sina ushahidi nimewahi kusikia kuna ushirikina wa kulogewa pombe ambapo utakuwa mlevi hadi pombe zikuue na nasikia kuna dawa za kienyeji unaweza kuchanganjiwa kwenye pombe ukatapika vitu vya ajabu na kuanzia hapo utakuwa umeacha pombe kabisa na ule uchizi wa pombe unaisha na kurudia akili zako
Umemaliza.

Bravo.
 
Habari za kwenu humu
Nina mwaka wa 12 sasa nakunywa pombe, nahitaji kuacha lakini nashindwa. Kila nikijaribu kuacha napata wakati mgumu sana hasa nimeshazoea nikinywa napata usingizi mapema usiku. Wiki hii nimejaribu kuacha kunywa siku moja, lakini usiku sikupata usingiz kabisa... Nimehisi mauzauza usiku mzima, nimekaa macho mpaka asubuhi.
Je hali hii ndo huwatokea wanywaji wote au ni kwangu tu? Jana kuna rafiki yangu ambae hatukuonana kitambo sana, ameisha sana kwa sababu ya pombe. Hii imenifanya nifikirie kuacha hii kitu, mana ninakoelekea si pazuri.

Nifanyeje ili niweze kuacha bila kupata hayo mauzauza ya kukosa usingizi?
Ni uamuzi mzuri . ... Usiendelee kung'ang'ania kitu kisicho na manufaa kwako. Pombe japo nzuri , ikitumiwa vibaya huleta madhara yasiyoweza kurekebishwa . Chukua hatua !!! Ni kuacha... Huhitaji ushauri... Acha !!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Piga chini kampani zote za tungi...
Oa..
Kama unakaa nyumba ya walevi hamaa...
Fikiri malengo mapya, kama huna nyumba anza ujenzi...kama huna watoto zaa...
Usikae na hela ambayo haina kazi...
Anza dose ya kutoa sumu ya pombe mwilini...
Hii dozi ikoje mkuu
 
Back
Top Bottom