Mimi rafiki yangu hela tu sina marafiki kabisa
Marafiki zangu walikuwa shule ya msingi basi
Achana na mambo ya urafiki kijana tafuta hela wapambe watakuja tu
Nukuu za biblia ama nukuu zozote za kidini hazifai kutumiwa kutolea mifano ya kimaongezi, kwa sababu imejaa mafumbo ya kutafakarisha yanayostahili tafsiri!
Unaelewa kuwa kuumbwa kwa mfano wa Mungu haina maana unayofasiri wewe hapa.
Maana ya kufanana na Mungu katika muktadha wa kufanana naye ni kwa 'Roho na akili za ufahamu na utashi' siyo kwa mwili wa nyama.
Kwa jibu ulilompatia aliyekuomba picha umemaanisha sisi binadamu tumefanana na Mungu kisura, kwa jibu hilo tayari umemkufuru Mungu.