Nahitaji Critical Thinking hapa tafadhali

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,132
Sawa ni kweli kwamba Mwanao alifariki akiwa na huyo Binti katika Starehe zao na hata hivyo Marehemu Mwanao nae kama kungekuwa kuna uwezekano na Sheria za Kuhukumu Maiti basi yawezekana hata Yeye pia huko huko aliko mavumbini basi angehukumiwa Kifungo cha miaka 30 kwa kufanya Mapenzi na Binti aliye chini ya Umri wa miaka 18.

Mpaka sasa nawaza na akili yangu imegoma kabisa kuelewa baadhi ya matukio yanayohitaji mno tafakuri tunduizi ( critical thinking ) ya kilichotokea jana katika Nyumba moja ya Sheria na Utoaji wa hukumu nchini Tanzania maeneo ya Posta.

Hivi Mama wa Marehemu amepata faida gani labda kwa kufurahia Binti mdogo kwenda Lupango kwa miezi 24? Hivi Mama wa Marehemu kitendo cha kutoka pale Nyumba ya Sheria na Hukumu Posta huku akifurahi na moja kwa moja kwenda alipolala Mwanae Kinondoni kumsalimia kilikuwa kina maanisha nini?

Kama ni mashindano je Mama wa Marehemu alikuwa anashindana nini na Binti aliyehukumiwa miezi 24 Gerezani? Zile furaha pale Posta zilizokuwa zikisindikizwa na machozi zilitokana na nini hasa? Je baada ya ule ushindi wa Kisheria na Kihukumu wa jana Marehemu ameshafufuka na sasa amerudi Kwake Sinza?

Hivi hapakuwa na room ya mazungumzo yoyote ya Kidiplomasia baina ya pande mbili Kinzani / Hasimu zaidi ya Kukomoana na kuonyeshana nani ni Bingwa / Mshindi? Kwahiyo kumbe siku hizi Wakristo nchini Tanzania tunarudishiana ubaya kwa ubaya ( wenyewe mnasema kama noma na iwe noma ) kwa wale Maadui zetu.

Naomba kuuliza hivi laiti kama zile Mali za aliyelala sasa pale Mtaa wa Mkulima Kinondoni zingekuwepo hadi hivi leo na zinazalisha Mama Marehemu angepoteza muda na Kesi hiyo? Je hapa tukiamini kama labda ukazaji wa Vyuma ndiyo umejenga hasira kwa Mama hadi akaamua Kumkomo Binti wa Watu tutakuwa tumekosea?

Nimalizie tu kwa kusema kwamba huko nyuma nilikuwa nasikia tu kwamba Watanzania japo masikioni mwa wengi wanasifika kwa kuwa Wakarimu ila nilichokigundua na leo mtanisamehe sana ni kwamba hakuna Watu wenye roho mbaya, makatili and pure sadists kama Watanzania kubali kataeni.

Kama Mkristo wa kweli binafsi sikuona haja yoyote ya Mama Marehemu kulishikilia hili jambo bango hivi na badala yake ningesamehe tu na kumuachia kila kitu Mwenyezi Mungu na kuendelea na maisha yangu bila Marehemu nikijua / kuamini kwamba kila jambo hupangwa na Mwenyezi Mungu.

Huyu Mama anaweza kudhani kuwa amefanikiwa 100% ila kwa jicho kali la Kisaikolojia nasema wazi kabisa kwamba Mama Marehemu huenda sasa akawa katika data base yake ndiyo ameharakisha kuongeza idadi kubwa ya Maadui kuliko Marafiki na hali ambayo huenda pia ikampelekea akawa na maisha magumu na ya shida pengine hata kuliko ambapo huyo Binti aliyefungwa angekuwepo uraiani.

Wadau huu ni mtazamo wangu tu na kama na Wewe una wako nakukaribisha sana nawe pia uweze Kutiririka na Kuserereka hapa na jisikie huru kunipinga kwa Hoja kwani hapa Great Thinkers tunaunganisha bongo zetu na kulifikiria hili nje ya box kabisa ili tuwekane sawa. Naomba leo katika uzi huu kusiwepo na matusi ya aina yoyote yale ila madongo ya hapa na pale Kwangu nayaruhusu ila siyo matusi. Nimetahadharisha mapema tu ili huko mbele ya safari tusije kulaumiana.

Nawapendeni nyote na karibuni pia.

Nawasilisha.
 
Tusimtwishe mzigo Mungu,ana mambo mengi ya kufanya,kila kitu tumuachie yeye tu wakati mambo mengine inawezekana kumalizana hapahapa,...BTW najaribu kuwaza kama jaji angekuwa jinsia nyingine...
 
Miaka miwili sio mingi,
After all so kwamba anaenda kwenye mateso,
Watu wengi hufananisha jela na mateso.

Ni heri aende jela akitoka atakua huru na hili swala kuliko lingekuja kumchukua katika wakati mwingne.
 
Alichoniacha hoi huyo mama ati anaishukuru serikali ya awamu ya tano, haya ni mauzauza matupu hajui hata muhimili wa mahakama ni nini.

Huyu mama kwa mara ya kwanza nilimsikia amekuja kwenye msiba wa Kanumba Dar na mpaka leo amezamia Dar na hana hata mpango na mzazi mwenzanke Baba Kanumba na amejipa haki zote za urithi wa marehemu, huyu mama ni sehemu ya mashetani tunaoishi nao humu duniani wakiwa na maumbo ya binadamu.

Since day one, tulipopata taarifa za kifo cha Kanumba hapa JF mpaka leo msimamo wangu juu ya Kanumba haujawahi kuyumba wala kubadilika, kwangu Kanumba alikuwa ni mbakaji tu na wala si vinginevyo.

Mungu amuweke anapostahili.
 
Gentamycine mtu akiiba akafungwa ni sawa au kuna haja kumsamehe tu akiwa amemuibia mkristu?
 
Kesi za mauaji ni Kesi za Jamhuri dhidi ya mtuhumiwa kwa hiyo mama Kanumba hangeweza kusema amesamehe Kesi iondolewe mahakamani mimi naona kosa la mama huyu ni kushangilia adhabu iliyotolewa kwa Lulu
Ni kweli mama kanumba asingeweza kusema asamehewe ambacho angeweza kufanya ni kutotokea mahakamani yeye na mashahidi mwisho wa siku keai ingefutwa kwa kukosa mashahidi
 
Two years ni michache kwa nadharia ya namba na uhalisia wa adhabu yake kwa aina ya kosa alilokutwa nalo Lulu,Ila ni Mingi kwa maana ya maisha aliyozoea na maisha mapya ambayo ataenda kuishi huko Lupango

Mwanadamu wa kawaida ana hulka ya vitu viwili katika maisha yake adaption ya mazingira yanayokuzunguka na pia kuwa na uwezo wa kusahau jambo hata kama lilikuwa kubwa kias gan ila hufkia mwisho na maisha yanaendlea, Hili swala linaonekana Gumu kwa pande zote mbili kwa sasa ila baada ya miez sita kuanzia sasa kila mtu ataanza kulichukulia kawaida kipind hicho na kifungo nacho kinakarbia kuisha.

Hii ni nafas pekee ya Lulu kujipanga na kurud upya uraian akiwa mkamilifu bila kuwa na mzigo wowote mgongon kwa maana atakuwa ameshatumikia adhabu yake, Kibiashara na aina ya maisha yake ya usanii inaweza kuwa ni opportunity nzur sana ya kubadlisha maisha yake kama akiamua kutumia vzur kutokuwepo kwake kwenye hii jamii, Atapata nafas ya kutafakari upya aina ya maisha yake na pia anaweza kuwa biashara nzur kwake kwenye tasnia yake ya usanii na matangazo kwa maana kila mtu atataka kujua nin kimtokea kwa kipind hicho alichokuwa huko,

Exclusive ya Maisha yake ya Jela inaweza kuwa ni fursa nzur ya kutengeneza kipato cha kutosha na kuanza maisha mengne kwa maana atapata nafas ya kufanya total overhaul ya maisha yake.

Ningekuwa Familia ya Lulu ningeshaur atumikie hii miaka miwili kuliko kufanya focus ya kukata rufaa kwa maana after two years na kwa umri wake bado mdogo atakuwa ameshautua huu mzgo mkubwa ambao ameish nao toka kifo cha kanumba.
 
Watanzania ni watu wa matukio!Jambo moja la msingi nililojifunza kutokana na sakata hili ni mizani ya haki bila kujali umaarufu wa mtu. Kosa limefanyika, ingekuwa vipi lulu asingekuwa maarufu, je tungekuja na fikra kama hizi??Au ni kujikosha tu...Tulilie haki itendeke bila kujali umaarufu wa mtu!
 
Huwezi Jua ni NINI kilichokuwa kinaendelea sidhan kama ni rahisi kwa yule mama kufurahia mtoto wa mwenzie afungwe kama malipizo ya mwanae kuawa..
 
Kwanini hoja imejengwa na "Angekua na biashara zake angekazana na kesi?" kesi ya mauaji mlalamikaji ni jamhuri, hata kama mama angekaa kimya jamhuri ingeweza kuendelea na kesi bila uwepo wake.

Kwanini mama kafurahi? Ni kwakua kapata closure. Articles nyingi zinazozungumzia abduction cases na murder huonyesha kua familia huridhishwa na hukumu ya kesi kwakua wanapata hitimisho.

Kuna kesi ya mama mmoja, Marekani, kajfungua kichanga akaletewa akaambiwa kimefariki, akataka akaone mara ya mwisho akagomewa.

Siku ya mazishi akapoint kua anahisi jeneza halina kitu ndani, wakampinga, na akawa diagnosed na postnatal distress.

Hiyo ilikua ni miaka ya 70.

Akaishi kwa miongo kumi akifanya kampeni akitaka kaburi lifukuliwe ili ajiridhishe na adhihirishe kua kichanga chake hakikufa siku ile. Akagewa ruhusa 2017 kaburi likafukuliwa ndani ya jeneza zikakutwa nguo bila dalili ya kuonyesha kua ndani kuliwahi kua na kiumbe.

Mama wa watu akasema nilichokua napambana nacho kwa miaka yote ni kupata hitimisho/ closure, haina maana kua mwanangu atarudi.
 
Great Thinker hapa hawahitajiki................ na nitakujibu 1 -4 au 5

1. Mama Kanumba hakumshitaki Lulu
2. Lulu alikuwa ameshitakiwa na Jamhuri
3. Nadhani wewe bado huna mtoto au bado kijana mdogo sanaa.....
4. Lulu alishashindikana na alikubuhu kwa mambo ya kikubwa... kabla ya kifo cha Kanumba alifanya party ya kuwa 18
5. Lulu na mama yake hawakupaswa hata kwa dawa kumdharau yule mama.... bado yeye kusema anakwenda kumzika rasmi mwanae kuna baya gani?


wakati Lulu na mama yake wanakuja na discover huku akimpiga kikumbo mama wa marehemuu as if ni mke mwenzake wewe uliona sawa tuu acheni kwanza hata hiyo miaka miwili nayo ni bado ni michache sana tena mno.

CV niliwahi kutumikia kifungo kwa kosa la mauji bila kukusudia hiyo ni adhabu tosha kwa life time yake........ Mungu ampe ujasiri amalize salama...........
 
Ni kweli mama kanumba asingeweza kusema asamehewe ambacho angeweza kufanya ni kutotokea mahakamani yeye na mashahidi mwisho wa siku keai ingefutwa kwa kukosa mashahidi


Hata kama mwanae amekufa sio kwa kuzira hivyo khaaa eti kutokutokea mahakamani khaaa
 
Believe me... She won't take much time there... Magu or Bashite will set her free before the end of this year!!!
 
Lulu na mama ake lulu hawakuwa na adabu hata kidigo kwa mama lkanumba. behind the scene walikuwa wakimdharau na kumtukana sn mama k...
Kosa moja alilolifanya Lulu ni kuweka ukaribu wa kupitiliza na mama Kanumba baada ya kutoka jela. Baada ya kukwaruzana mama alikuwa na jazba na Jana alifurahia kale katoto kanakomkosea adabu na kaliko sababisha kifo cha mwanae kanaenda jela.
 
Nadhani kilichotekea ni suala la kisheria na Lulu pale alikuwa mshitakiwa lakini kisheria pia ni shahidi katika kase yake mwenyewe.

Na ushahidi wa kimazingira ndiyo uliomfunga Lulu.Mama Kanumba ana haki ya kushukuru Mahakama kwa kutenda haki dhidi ya mshitakiwa kwani kwanza ni haki yake kisheria kujua hatma ya kesi ya maauaji ya mwanawe lakini kisaikolojia inampa faraja moyoni kuwa sasa haki imetendeka na maneno maneno tena kuhusu kesi ya mwanawe imekwisha kwani kesi imeshaamuliwa.

Unless otherwise kuna kuna kukata rufaa hivyo moyoni ana amani kabisa haijalishi kifungo ni cha muda gani lakini mtenda amepata adhabu kwa mujibu wa sheria kwake hiyo inatosha kabisa kumuondoa katika mateso aliyokuwa anapata akisoma katika magazeti na mitanda kuhusu jinsi alivyokuwa anapeta na kufanya starehe huku kesi ikiwa haijulikani imeishaje.

Mama Kanumba kwenda kuona kaburi la mwanawe ni heshima tu na kutoa salam kwa marehemu hata kama amelala mauti lakini kiimani wengine wanaamini kuwa anasikia kuwa yule aliyetenda kosa amepata adhabu yake hivyo kiimani inampa mama faraja pia na namna ya kuondoa sonona na mawazo mengine lakini zaidi ni heshima na mila zetu za kiaafrica kutembelea makaburi.
 
Back
Top Bottom