Nahitaji chupi ngapi?

Sijui kwa wengine ila kwa mimi chupi ni muhimu ,kwasababu unaweza kubwa na hali ikaweza kukuletea aibu na kukaa huwezi nakuchomoa shati huwezi nadhani naeleweka!
 
Hii Hiii hiiiii hii Hooo Aaaa!

Nakumbuka enzi zile nilipokuwa huru sikuwa navaa chupi kabisa tangu niingie katika utumwa huu wa kujitakia imebidi nivae chupi.

Darasa la kwanza mpka la 5 nilikwenda shule huku nikipiga Kengele njia nzima. Darasa la tano mwishoni nililima Robo Eka ya mahindi nilipo vuma debe kaa 7 hivi niliuza na kununua chupi ya kwanza aina ya James Bond 007. Rangi ya Pundamilia ya blue na White

Nilikuwa nikiifua usiku na kuikausha kwa Taulo. Teknolojia hiyo bado naitumia mpaka leo. Nakunja taulo moja mara tatu naweka Kauka nikuvae yangu kisha nakunja taulo jingine mara tatu na kuliweka juu ya chupi kisha naweka kitu kizito zaidi ya kilo 5. Kwangu kitu kizito, ilikuwa ni Beseni lilojaa maji na kuliweka juu ya Dryer yangu usiku kucha. Asubuhi inakuwa imekauka vizuri kabisa.

Miak 6 ya sekondari nilikuwa nazo 2 tu.
Jeshini Burombora nilikua nayo moja tu na baadaye 0 kwani haikua chupi tena bali nyuzi lekevu mfano wa sketi ya kipepe. Nilikuwa naifua nakuianika juani, wakati inakauka mie napiga mbizi Lake Tanganyika kule kwa Zitto.
Uzuri mimi si mtu wa Mademu kabisa, hata leo hii hapa US kwenye uwingi wa mademu pochi yako tu, mie bado naheshimu Ufula (Private part) yangu.

Siku moja baada ya chupi yangu kukauka upepo uliipeperusha ikakwama mahali, nikaanza kuitafuta huku nikiwa nimevaa bukta ya kijani ya JKT. Mademu wawili walisoma Msalato Sec School( Huenda wapo hapa wanasoma hiui hadithi) walipita pale waliniuliza natafuta nini nikawaambia natafuta noti ya shilingi mia, niliipoteza jana. Walinisaidia kutafuta kaa nusu saa hivi wakagive up na kuondoka. Baadaye nikaiona ikiwa imekwama machakani katikati ya mawe.

hiii hiiiii hiiii Aaaaah!

Siku hizi navaa Boxer aina ile ya Kaptula muda si mrefu nahisi nitakuwa huru tena na kuanza kupiga Kengele kama awali.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom