Asante dada kwa herHahahaaa! I'm not that extreme... Lol
Nishakuwa kwenye situation kama hiyo na nikwambie tu haina afya kabisa, hata ukijidai sijui unamgeukia Yesu asuluhishe hutopata hiyo suluhu.
1. Kila mtu amezaliwa huru humu Duniani na ana haki kabisa ya kuishi anavyotaka, amini navyokwambia nikisema kuishi anavyotaka maana amepewa uwezo huo.
2. Yesu hamfundishi mtu kuishi maisha ya uwoga yaliyo kinyume cha furaha ya moyo wake, Jamaa anahitaji tiba ya nafsi na wala si reconciliation na mtu ambaye hata hajaiomba hiyo reconciliation
3. Dawa nzuri ni kutoka katika misery aliyopo sasa. Aji assess na kuji analyze, akiwa calm and collected then njia zitaanza kufunguka Yesu wa kweli atapata hata nafasi ya kufanya kazi......
Natumaini umenielewa ndugu. Nyumba ya Mungu ni yenye utulivu, Yesu hawezi kukaa kwenye fujo zilizo kwenye kichwa cha ndugu yetu. Asante
Ndoa hizi tabu kweli
Sample yangu tupo wachache sana na mimi ninakuhakikishia sipo kwenye hilo kundi la mabwege rafiki!!!! sasa nikuulize wewe rafiki hivi ule ushauri uliomshauri jamaa mwanzilishi wa mada hii unaukumbuka? ule wa yeye amuue huyo mke au sijui aende haraka Rufiji, kigoma pangani na wapi sijui ulikuwa unamaanisha akapate suluhsho kwa nani huko? au ndiyo unadhani ndiyo mzuri kuliko nilivyomshauri mimi halafu umemalizia kwa herufi kubwa rafiki "TUMSIFU YESU KRISTU". unamaaisha kuwa matatizo yetu tuyatatue wenyewe wa kwenda huko pangani nk au kumuua huyo mke?nikuulize tu rafiki hivi YESU uliyemtaja ana rangi mbili? yumkini na wewe unamtaja tu lakini humjui!!!! (usihamaki jibu tu maswali yangu yote nitakuelewa )
Hapa ni JF siyo kanisani ndiyo, lakini swala la ndoa ni la Mungu na ndiyo mwasisi wake ukimtoa ndiyo hapo utakimbilia Pangani na kwingineko au kuua kama ulivyomshauri jamaa ukadhani unatafuta suluhisho kumbe unatendakazi ya aliyekinyume na Mungu)
Lati hujajaaliwa kalio? Naona unaongea kwa uchungu sana!! Usijali wapo wengi tu wasioangalia kalio.ndio shida yakumpendea mwanamke shepu hiyo... mnapoamua kuchagua mwanamwali wakuoa mnakimbiliaga makalio na sura mnajua ndio mmepata sasa acha akunyooshe, watoto wazuri wenye akili timamu wapo hamuwaoi kisa hana ---- sasa impact yake ndio hiyo, sikuonei huruma hata tone endelea kukomesheka hadi upate dipresheni nakuongea pekeyako
Mnuso wangu wa sita unanipa shida kuamini kilicholetwa hapa angalao kwa asilimia fulani. Miaka 10, watoto 3, shida imeanza kabla ya ndoa, ..... sawa! Ana digrii, ametafuta mke wa nyumbani, anakiwanja lkn watagawana nyumba.... sawa! Mbona yote yanamwelekea mwanamke tuuuuuuu? Mbona hausikii kero za upande wa pili. Asimwache bhana aende ampigie magoti aliyomkosea, mbona mke shegga kabisa!
Uko sahihi kabisa. Hapa kuna vitu vingi hatuvijui ila tunakimbilia kusema huyu mwanamke ni this n that. Ogopa sana mwanaume anaekupa stori kujionyesha kuwa ye ni victim wa matukio mabaya ya mkewe au girlfriend. Mtu wa namna hii mara nyingi ni mbaya na guilty consciousness yake kwa anayoyafanya humfanya kujivictimize ili aonekane ye ni mwema. Hivi unaweza ukawa na matatizo ya uhusiano tangu mnaanza kuishi pamoja then hamfungi ndoa, then mnapata two more kids bila ndoa. Na mnaishi tu, na haya matatizo mmejaribu vipi kuyatatua as in third part imehusishwa?(wazazi mmewahusisha matatizo yenu na walifanya nini?)Ulisema ulimrudisha kwao kwasababu gani? Je , hana hata kaka zake au babake ? Nashindwa kuamini sababu ipo familia yenye tatizo kama lako lakini mlalamikaji ndiye hasa tatizo.Mi nadhani huyu mshikaji nae ana yake...huyo dada anaweza reveal ya mkuu hapa ukashangaa...red flag #1 :kwa miaka yote 10 hujamuoa,u are wrong na the woman is mad on u about that,definetly,mtu kakuzalia,kakulelea kwa miaka kumi halafu umuoi?aisee lazima achanganyikiwe on that....red flag #2 :dada kalalamika michepuko,obvious utakua unahusika hapa...red flag3#:kuna mambo yapo family related kwa upande wenu,hayo na mke wa kwanza wa dingi yako,na kifo chake,nk,siri wanazijua wao na wewe labda,hapo nako ni another issue....
Spade4spade . Nimesoma huu uzi mara nyingi na kupitia maoni ya watu wengi but speaking from experience nachelea kuamini hii stori kwa asilimia mia. There is a lot that was going on hatujaaelezwa. In short I don't buy it. Nina mkasa wa mwanaume mkorofi, mwenye roho ngumu na asiyejali hisia za mkewe na yeye ndiye haswa chanzo cha shida kwenye nyumba. Lakini huzunguka na stori kama hii sasa nashindwa kuelewa huruma za wananchi juu yake sijui huwa zinamsaidiaje wakati deep down his heart anajua ye ndiye chanzo cha mkewe kutomwamini and all other stuffs.
Ninajua kutunza mwanamke, ukikutana nae kama hajabeba watoto utasema ni binti hajazaa. Watu huwa hata hawaamini kama hao watoto kawazaa yeye, angekuwa amechoka angekuwa mtulivu sana.
Nilifanikiwa kuoa miaka kumi iliyopita na katika maisha yetu ya wawili tumefanikiwa kupata watoto watatu, wote wa kiume.
Migogoro katika maisha yetu ilianza mara baada ya kuanza kuishi pamoja. Mimi na mke wangu tulianza kuishi pamoja kabla ya kufunga ndoa. Binafsi nilimpenda sana na nilitamani kumfanyia kila ninaloweza ili awe na amani na furaha.
Kiukweli tulianza kuishi kwa amani na furaha mpaka pale mke wangu huyu alipoanza chokochoko dhidi ya mama yangu. Alianza kuniambia kuwa mama yangu hampendi na wala alikuwa hataki aolewe na mimi na kisha akaanza kwashambulia wifi zake. Nilijiuliza maswali mengi na baade nikagundua kuwa ni maneno ya kutunga.
Kilichonifanya niamini ni baada ya kukumbuka kwamba mimi na mke wangu tumechukuana kwa maamuzi yetu binafsi (mimi siwashirikishi wazazi) na pili ni kwamba wazazi wangu wanaishi mbali na anapoishi huyo mwanamke, na tatu hapajawahi kuwa na mahusiano yoyote na wala mawasiliano yoyote baina ya familia hizi mbili.
Hapo nikaanza kumuona mke wangu kama mtu wa shari. Mke wangu nilimtoa bara kuja kuishi naye Dar es Salaam na nilitamani kuja kufunga nae ndoa.
Baada ya kuishi naye kwa mwaka mmoja jijini Dar es Salaam na tukiwa tumefanikiwa kupata mtoto mmoja tulipanga safari ya kwenda kijijini kuwasalimia wazazi pamoja na kujitambulisha kwao. Ilipofika Jumapili nilimwambia tutaenda kanisani na tutajitambulisha tukiwa pamoja ili kanisa litupokee na baadae tuanze mchakato wa ndoa.
Tulikubaliana kwa ajili ya hilo ila tulipofika kanisani kabla ya kuingia kwenye ibada huyu mwanamke akaniambia nisimtambulishe kanisani na wala nisijaribu kumtaja. Nilipatwa na hasira iliyoharibu ibada yangu na tuliporudi nyumbani ikawa ni ugomvi tu.
Mimi ni msomi mwenye digrii na mke wangu ni mama wa nyumbani. Niliamua kuoa mama wa nyumbani kutokana na nature ya kazi yangu inayonihitaji kuwa mbali na nyumbani kwa kipindi kirefu nikiwa kwenye camp.
Maisha yaliendelea hukutukiwa na migogoro isiyoisha kila mara akinituhmu kwa mambo mbalimbali, mara nyingine alinituhumu kuwa nina mke mwingine na nimemjengea nyumba na mara nyingine ananituhumu kuwa namuua kwa UKIMWI.
Sikujisikia vizuri na mara kwa mara nilikuwa naenda kupima ili awe na amani na kuna kipindi nilikuwa namchukua kwenda kupima ila yeye anachukua vipimo vingine na kukataa kupima UKIMWI.
Mimi huwa napima na majibu namuonyesha. Katika hali hizo nilijikuta maisha yangu nyumbani yanakosa furaha na mara kwa mara ni mizozo mara huu mara ule. Hata tendo la ndoa ilikuwa nadra kulipata kwa hiari na wakati mwingine nahisi ana mwanamume mwingine anayemzuzua.
Mbali na kuwa mbali kwa muda mrefu, muda mfupi tunaopata kuwa pamoja unakuwa na majonzi tele. Kuna kipindi nilisafiri kwa wiki sita 6 na niliporudi nikadhani mwenzangu amenikumbuka ila nilichokiona usiku ni kibaya. Tulienda kulala na alipojilaza tu akavunga amesinzia usingiz mzito, nilijaribu kumuamsha ila akavunga kufa. Nilijaribu kulala ila sikuweza kupata usingizi nikaamua kwenda kulala kwenye sofa sebuleni ili nijisikie niko safarini.
Kuna kipindi nilipoteza kazi akaniambia ameonyeshwa kuwa hayo ni mapigo na wala sitakaa nipate kazi tena. Wakati huo nilikuwa nimepata kiwanja hapa Dar es Salaam na nikiwa najipanga kuanza ujenzi.
Nilikaa mtaani miezi miwili na baadae nikapata kazi mpya. Baaada ya kupata nilimwambia nataka kuanza ujenzi, yeye aliniambia ni vema nikaacha kujenga kwani nitapata hasara.
Nilimuuliza hasara gani nitapata akasema hiyo nyumba itakuja kuuzwa ili tugawane hela. Mi nilimambia simsikilii yeye ila naangalia mahitaiji ya watoto wangu kwamba wanatakiwa kuwa na nyumbani kwao.
Nilibahatika pia kupata gari na siku moja nikiwa safarini peke yangu kwenye gari nilipata ajali ya kugongwa na gari nyingine. Bahati nzuri ni gari iliharibika ila mimi nilibaki salama.
Baada ya tukio hilo siku moja tukiwa kwenye mzozo alinitolea neno kali kuwa nilipata ajali kwa maombi yake. Anadai aliomba nikipakia mwanamke kwenye gari yangu nipate ajali. Nilijisikia kumrukia nimle nyama mbichi lakini nikajizuia.
Mizozo imekuwa mingi mpaka najisikia kumtapika, sina amani wala furaha niwapo
mkuu achana nae huyo gubegube la sivyo atakuletea kila aina ya nuksi na hata kukurestisha in peace. kama anataka mgawane mali mpe, we baki kuhudumia watoto. Mali kitu gan, na anafanya hivyo makusudi akitumia ngao ya watoto na mali kuwa hutakuwa na uthubutu wa kumuacha. Tena muache kwa herufi kubwa, msomi kama wewe mwenye shahada unapelekeshwaje na huyo leyman, unatuaibisha aisee.