Nahisi simpendi mke wangu

Nahisi simpendi mke wangu

Mkeo ana asili ya ukorofi tu na pengine ana mambo ya kishirikina
Sijaona sehemu kama umeandika mmeshafunga ndoa, kama hamjafunga ndoa achana nae, atakuja kukuua huyo
 
Ninajua kutunza mwanamke, ukikutana nae kama hajabeba watoto utasema ni binti hajazaa. Watu huwa hata hawaamini kama hao watoto kawazaa yeye, angekuwa amechoka angekuwa mtulivu sana.

stori yako ya uongo bana.
 
Elizabeth hukuwa umesoma vizuri andiko langu la kwanza ndiyo maana ukanijia juu namtisha. Lakin suala la ndoa huwezi kulitenganisha na YESU ikiwa nje ya hapo ndiyo hivyo baadaye anaanza kulialia. nilichokuwa najaribu ni kumrejesha kwa mwasisi wa ndoa zote, wewe ukawaunag'ang'ana amwache. hata hivo kama nilikuwa nasingizia basi nilikuwa nasingizia yesu na siyo YESU labda kama huelewi kati ya YESU na yesu na hicho ndiyo kilichokufanya uhamaki

Kama sijakuelewa samahani na hata baada ya kukuelewa nitasema hivyo hivyo, hauwezi ukasema unamrejesha mtu kwa Yesu bila basis yeyote hapa nitaanza kukuuliza matatizo yake yatafumbuliwa vipi once "ukimrejesha" kwa Yesu?
Kutisha ni kumbana mtu na kumuonyesha hakuna option zaidi ya ulizompa ukidai ndio suluhu
 
Ni stori ndefu nikisimulia jinsi tulivyoanzana, ila nahisi kuna kitu kilitumika kuingia kwenye dimbwi hili. Tangu nasoma O-Level nilikuwa nimejiwekea vigezo vya nani atakuwa mke wangu. Mpaka nikaviandika kwenye daftari. Juzi kati nikiwa nasoma kwenye library yangu nikakuta vigezo hivyo hivyo niliviandika nikiwa Chuo Kikuu, ia kilichotkea huwezi amini, uzuri wa sura na vingne vilinchaganya ama kulikuwa na nguvu ya ziada ya kunitoa akili.
Sijui kama hao wazee wataweza kubadilisha maisha ya huyu mwanamke kwani tumeshaongea na mama yake mara nyingi na kuahidiwa atabdilika. Lakini mpaka leo nasubiria mabadliko siyaoni. Mpaka hapa tunapozngumza ingawa mke wangu ni mama wanyumbani na tuna mfanyakazi nguo nanyosha mwenyewe kwa miaka yote. Taa ikiungua niko safarini nasubiriwa nije nibadili mwenyewe. Muda si mrfu nimepigiwa simu kuwa umeme umeisha nyumbani. Ninunue ilhali niko mikoani mingine yeye yuko ndani. Hela ninayomwachia ni nyingi nikisema hapa watu watadhan nafanya promo.

1.Ingawa sina uzoefu sana na swala la ndoa lakini nimekuja kugundua matatizo mengi ya ndoa yanasababishwa na misingi yenyewe ya ndoa,ndio maana nauliza kama mlipendana na mkaridhia kuishi pamoja bila shinikizo la kitu chochote,watu wanaweza kuoana kwa vigezo visivyo na mantiki sana, mfano watu wanaweza kuoana just for the sake of ujauzito lakini kumbe hawapendani,au mwingine anaona hivi nisipomuoa huyu nina uhakika gani atatokea mwingine wa kuyakubali mapungufu yangu lakini in reality hawapendani.

2. communication pia husaidia, kama mmetofautiana ni vizuri mnamaliza tofauti zenu haraka iwezekanavyo,kwa sababu kama tofauti zenu hamziongelei matokeo yake mtu anakuwa kayapanga tu moyoni siku likilipuka ndio kama hivyo.

3. La mwisho,kama mtu ni wa kupenda sala basi kwenye ndoa ndio inabidi upende kusali zaidi kuliko zamani na kama si mtu wa kupenda sala basi kwenye ndoa inabidi uipende sala kilazima coz uchawi upo na watu wanaweza kubadilika hadi usiamini kama uliyenae ndie yule uliyeoana nae.

Hapo ndoa haipo tena ila mwenye maamuzi ya mwisho ni wewe
 
Kama sijakuelewa samahani na hata baada ya kukuelewa nitasema hivyo hivyo, hauwezi ukasema unamrejesha mtu kwa Yesu bila basis yeyote hapa nitaanza kukuuliza matatizo yake yatafumbuliwa vipi once "ukimrejesha" kwa Yesu?
Kutisha ni kumbana mtu na kumuonyesha hakuna option zaidi ya ulizompa ukidai ndio suluhu
afadhali umekuwa friendly dada!!!!! sasa tunaweza kuongea!!!!! kama ni kutoa option nyingine unadhani ya kuachana ndiyo option sahihi?ndiyo maana nikakutaka ujiweke wewe kwenye hiyo nafasi uone kam ni rahisis kiasi hicho au the magnificent ikiambatana na ya mkonopaka walionishambulia mimi kupitia andiko lako kwangu uliloniambia namtisha. au ule ushauri wao eti amuue au ende pangani, kigoma Rufiji hao unasemaje
 
Hahahahaaaa, mi kiazi! Hakyanani umenichekesha sana bhana! Yaani kumbe ushauri mzuri ni kuharibu, haya ngoja nitoe ushauri wa kuharibu ili niwe na miaka 22 afu nimeoa, afu nipo kwangu nimejenga bangaluuu na wazazi wangu wako mbaali kama mwanza na mtwara. miss chagga.
jamani nini tena inabidi uwaache tu watuu kama hawa
 
Mbona unahamak dada??? kwani shetani ni mbaya? kama kweli unaliona hilo kuwa shetani ni mbaya mbona ulimshauri mwenzio kutenda jambo la kishetani na ukawa unadhani unamhari vyema

ha ha ha ha ulitaka nimshauri akaa nae hadi kifo kimpate miaka 800?????
na ushauri wangu sio sheria mkuu......
sijawahi kuona shetani na wala sijui ubaya wa shetani....binadamu ndo wanafanya mabaya
 
afadhali umekuwa friendly dada!!!!! sasa tunaweza kuongea!!!!! kama ni kutoa option nyingine unadhani ya kuachana ndiyo option sahihi?ndiyo maana nikakutaka ujiweke wewe kwenye hiyo nafasi uone kam ni rahisis kiasi hicho au the magnificent ikiambatana na ya mkonopaka walionishambulia mimi kupitia andiko lako kwangu uliloniambia namtisha. au ule ushauri wao eti amuue au ende pangani, kigoma Rufiji hao unasemaje

Hahahaaa! I'm not that extreme... Lol
Nishakuwa kwenye situation kama hiyo na nikwambie tu haina afya kabisa, hata ukijidai sijui unamgeukia Yesu asuluhishe hutopata hiyo suluhu.
1. Kila mtu amezaliwa huru humu Duniani na ana haki kabisa ya kuishi anavyotaka, amini navyokwambia nikisema kuishi anavyotaka maana amepewa uwezo huo.
2. Yesu hamfundishi mtu kuishi maisha ya uwoga yaliyo kinyume cha furaha ya moyo wake, Jamaa anahitaji tiba ya nafsi na wala si reconciliation na mtu ambaye hata hajaiomba hiyo reconciliation
3. Dawa nzuri ni kutoka katika misery aliyopo sasa. Aji assess na kuji analyze, akiwa calm and collected then njia zitaanza kufunguka Yesu wa kweli atapata hata nafasi ya kufanya kazi......

Natumaini umenielewa ndugu. Nyumba ya Mungu ni yenye utulivu, Yesu hawezi kukaa kwenye fujo zilizo kwenye kichwa cha ndugu yetu. Asante
 
Pole kaka yangu, yani roho imeniuma utazani mimi ndo natendewa hayo, huyo si mke bali mfano wa mke nahisi ibilisi mzima mzima anaishi ndani yake, na kwa vile hamjafunga ndoa me nakushauri mrudishe kwao sio aende peke yake mpeleke na ukimfikisha waeleze wazazi wake kwamba uvumilivu umekushinda na kamwe mtoto wao hawezi badilika kwahiyo umeamua kumuacha, na kwa vile mna nyumba mbili, mpe moja yeye aisha atakavyo na wewe ishi kwenye hiyo nyingie, anza upya hakuna jinsi hapo
 
na kwa hali ilivyo am afraid iko siku atakutoa roho
 
ha ha ha ha ulitaka nimshauri akaa nae hadi kifo kimpate miaka 800?????
na ushauri wangu sio sheria mkuu......
sijawahi kuona shetani na wala sijui ubaya wa shetani....binadamu ndo wanafanya mabaya

asante kwa heri
 
Pole sana mkuu.. Achana nae endelea na maisha mengine

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
watu sampuli yako ndi husababisha waTZ tuendelee kuonekana maBw.ege miaka hadi miaka.....
we mpaka mtu afe ndo ujue kuna tatizo hapo? haya mambo mengine YESU anapenda kuona tunayatatua wenyewe....sio kila kitu tumuachie yeye....
After all hapa sio kanisani,ya kaisari mpe kaisari,ya mungu mpe mungu....!!

TUMSIFU YESU KRISTU
Sample yangu tupo wachache sana na mimi ninakuhakikishia sipo kwenye hilo kundi la mabwege rafiki!!!! sasa nikuulize wewe rafiki hivi ule ushauri uliomshauri jamaa mwanzilishi wa mada hii unaukumbuka? ule wa yeye amuue huyo mke au sijui aende haraka Rufiji, kigoma pangani na wapi sijui ulikuwa unamaanisha akapate suluhsho kwa nani huko? au ndiyo unadhani ndiyo mzuri kuliko nilivyomshauri mimi halafu umemalizia kwa herufi kubwa rafiki "TUMSIFU YESU KRISTU". unamaaisha kuwa matatizo yetu tuyatatue wenyewe wa kwenda huko pangani nk au kumuua huyo mke?nikuulize tu rafiki hivi YESU uliyemtaja ana rangi mbili? yumkini na wewe unamtaja tu lakini humjui!!!! (usihamaki jibu tu maswali yangu yote nitakuelewa )

Hapa ni JF siyo kanisani ndiyo, lakini swala la ndoa ni la Mungu na ndiyo mwasisi wake ukimtoa ndiyo hapo utakimbilia Pangani na kwingineko au kuua kama ulivyomshauri jamaa ukadhani unatafuta suluhisho kumbe unatendakazi ya aliyekinyume na Mungu)
 
Mm naonea watoto huruma! Lkn kuachana pia ni jambo la msingi! Mbona wanawake wazuri wapo na watakutunzia watoto vizuri tu! Ana mambo mabaya yote, mtu mwenyewe hafanyi kazi analeta dharau! Wapo wanawake kibao wanatafuta mume wa mf wako na wanalia kila siku yy hawazi hilo? Tena usije ukalikoroga kuongeza mtoto mwingine! Huyo hakufai hata mungu amjui huyo! Kubali si chaguo lako tena watoto wenyewe wa kiume????? Kama unauwezo wa kutosha peleka watoto wote boarding, pili mrudishe nyumbani kwao anza maisha upya achana na ibirisi huyo, hakuonei huruma na wewe mwenyewe pia hujionei huruma??????
 
ha ha ha ha ulitaka nimshauri akaa nae hadi kifo kimpate miaka 800?????
na ushauri wangu sio sheria mkuu......
sijawahi kuona shetani na wala sijui ubaya wa shetani....binadamu ndo wanafanya mabaya

Ahsante kwa heri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom