Nahisi simpendi mke wangu

Nahisi simpendi mke wangu

Mmeshawahi kuzungumza kuhusu kutengana??
Labda kutenganan kwa mwaka hivi...ili kujiangalia upya??
 
Ww ndo mwenye matatizo!!!! Kama mke wako hakupendi husingekuwa nae, kuna vitu viwili; either ulimtesa sana wakati unamchumbi au ulimuonyesha kuwa una wapenz nje ndo maana alikuchukia, kama ulivyosema kuwa kazi zako ni za nje huenda ulikuwa na vichenchele huko, au hukuwahi kwenda naye huko ulikokuwa ukifanya kazi hivyo imani yake kwako ilipotea, yaani kuna kitu ulikifanya sio bure, na kwa nn ulikuwa ukipima ukimwi eti kumuakikishia kama ulikuwa wajiamini?????? Huenda mwenzetu unachepuka sana, Sikushauri umuache kwakuwa umeshazaa nae, na ana watoto wako tena wakiume usije kufa mpweke, maana hao watoto once wakikuwa wanaweza kukubadilikia, Muonyeshe upendo mke wako jaribu kumsahaurisha yaliyopita, atabadilika maana wanawake ni dhaifu sana. ZINGATIA
 
Sasa wewe ushasema ni mama wa nyumbani unategemea nini...
Mama wa nyumbani huwa wakati mwingi humuhisi mumewe anachepuka sababu yeye yupo nyumbani hana la kufanya / yupo free..Hivyo anataka akikusms umjibu wkt ule ule hajui kuwa wewe wkt mwingine upo busy
...Anataka akikupigia cm upokee...sababu yeye haoni unachokifanya kazini hajui pengine wkati mwingine upo na wageni au boss au ktika mazingira ambayo huwezi pokea cm..Basi yeye huhisi anaibiwa tuuu...
Kingine mama wa nyumbani upeo wa kufikiri hupungua kwani yeye huzungukwa na watu wa mitaani tuu wanaobaki wkt wengine wameenda makazini so ni umbea tuu, au yeye ni kukaa tuu hakuna anachokiwazaa zaidi ya mawwazo machafu machafu na mawazo ya mapenzi tuu..

Uliyataka so uyanywe..Usimuache vumilia..ila pole sana...mpeleke akasome kidogo ubongo upanuke huoo..




Nilifanikiwa kuoa miaka kumi iliyopita na katika maisha yetu ya wawili tumefanikiwa kupata watoto watatu, wote wa kiume.

Migogoro katika maisha yetu ilianza mara baada ya kuanza kuishi pamoja. Mimi na mke wangu tulianza kuishi pamoja kabla ya kufunga ndoa. Binafsi nilimpenda sana na nilitamani kumfanyia kila ninaloweza ili awe na amani na furaha.

Kiukweli tulianza kuishi kwa amani na furaha mpaka pale mke wangu huyu alipoanza chokochoko dhidi ya mama yangu. Alianza kuniambia kuwa mama yangu hampendi na wala alikuwa hataki aolewe na mimi na kisha akaanza kwashambulia wifi zake. Nilijiuliza maswali mengi na baade nikagundua kuwa ni maneno ya kutunga.

Kilichonifanya niamini ni baada ya kukumbuka kwamba mimi na mke wangu tumechukuana kwa maamuzi yetu binafsi (mimi siwashirikishi wazazi) na pili ni kwamba wazazi wangu wanaishi mbali na anapoishi huyo mwanamke, na tatu hapajawahi kuwa na mahusiano yoyote na wala mawasiliano yoyote baina ya familia hizi mbili.

Hapo nikaanza kumuona mke wangu kama mtu wa shari. Mke wangu nilimtoa bara kuja kuishi naye Dar es Salaam na nilitamani kuja kufunga nae ndoa.

Baada ya kuishi naye kwa mwaka mmoja jijini Dar es Salaam na tukiwa tumefanikiwa kupata mtoto mmoja tulipanga safari ya kwenda kijijini kuwasalimia wazazi pamoja na kujitambulisha kwao. Ilipofika Jumapili nilimwambia tutaenda kanisani na tutajitambulisha tukiwa pamoja ili kanisa litupokee na baadae tuanze mchakato wa ndoa.

Tulikubaliana kwa ajili ya hilo ila tulipofika kanisani kabla ya kuingia kwenye ibada huyu mwanamke akaniambia nisimtambulishe kanisani na wala nisijaribu kumtaja. Nilipatwa na hasira iliyoharibu ibada yangu na tuliporudi nyumbani ikawa ni ugomvi tu.

Mimi ni msomi mwenye digrii na mke wangu ni mama wa nyumbani. Niliamua kuoa mama wa nyumbani kutokana na nature ya kazi yangu inayonihitaji kuwa mbali na nyumbani kwa kipindi kirefu nikiwa kwenye camp.

Maisha yaliendelea hukutukiwa na migogoro isiyoisha kila mara akinituhmu kwa mambo mbalimbali, mara nyingine alinituhumu kuwa nina mke mwingine na nimemjengea nyumba na mara nyingine ananituhumu kuwa namuua kwa UKIMWI.

Sikujisikia vizuri na mara kwa mara nilikuwa naenda kupima ili awe na amani na kuna kipindi nilikuwa namchukua kwenda kupima ila yeye anachukua vipimo vingine na kukataa kupima UKIMWI.

Mimi huwa napima na majibu namuonyesha. Katika hali hizo nilijikuta maisha yangu nyumbani yanakosa furaha na mara kwa mara ni mizozo mara huu mara ule. Hata tendo la ndoa ilikuwa nadra kulipata kwa hiari na wakati mwingine nahisi ana mwanamume mwingine anayemzuzua.

Mbali na kuwa mbali kwa muda mrefu, muda mfupi tunaopata kuwa pamoja unakuwa na majonzi tele. Kuna kipindi nilisafiri kwa wiki sita 6 na niliporudi nikadhani mwenzangu amenikumbuka ila nilichokiona usiku ni kibaya. Tulienda kulala na alipojilaza tu akavunga amesinzia usingiz mzito, nilijaribu kumuamsha ila akavunga kufa. Nilijaribu kulala ila sikuweza kupata usingizi nikaamua kwenda kulala kwenye sofa sebuleni ili nijisikie niko safarini.

Kuna kipindi nilipoteza kazi akaniambia ameonyeshwa kuwa hayo ni mapigo na wala sitakaa nipate kazi tena. Wakati huo nilikuwa nimepata kiwanja hapa Dar es Salaam na nikiwa najipanga kuanza ujenzi.

Nilikaa mtaani miezi miwili na baadae nikapata kazi mpya. Baaada ya kupata nilimwambia nataka kuanza ujenzi, yeye aliniambia ni vema nikaacha kujenga kwani nitapata hasara.

Nilimuuliza hasara gani nitapata akasema hiyo nyumba itakuja kuuzwa ili tugawane hela. Mi nilimambia simsikilii yeye ila naangalia mahitaiji ya watoto wangu kwamba wanatakiwa kuwa na nyumbani kwao.

Nilibahatika pia kupata gari na siku moja nikiwa safarini peke yangu kwenye gari nilipata ajali ya kugongwa na gari nyingine. Bahati nzuri ni gari iliharibika ila mimi nilibaki salama.

Baada ya tukio hilo siku moja tukiwa kwenye mzozo alinitolea neno kali kuwa nilipata ajali kwa maombi yake. Anadai aliomba nikipakia mwanamke kwenye gari yangu nipate ajali. Nilijisikia kumrukia nimle nyama mbichi lakini nikajizuia.

Mizozo imekuwa mingi mpaka najisikia kumtapika, sina amani wala furaha niwapo
 
Sasa wewe ushasema ni mama wa nyumbani unategemea nini...
Mama wa nyumbani huwa wakati mwingi humuhisi mumewe anachepuka sababu yeye yupo nyumbani hana la kufanya / yupo free..Hivyo anataka akikusms umjibu wkt ule ule hajui kuwa wewe wkt mwingine upo busy
...Anataka akikupigia cm upokee...sababu yeye haoni unachokifanya kazini hajui pengine wkati mwingine upo na wageni au boss au ktika mazingira ambayo huwezi pokea cm..Basi yeye huhisi anaibiwa tuuu...
Kingine mama wa nyumbani upeo wa kufikiri hupungua kwani yeye huzungukwa na watu wa mitaani tuu wanaobaki wkt wengine wameenda makazini so ni umbea tuu, au yeye ni kukaa tuu hakuna anachokiwazaa zaidi ya mawwazo machafu machafu na mawazo ya mapenzi tuu..

Uliyataka so uyanywe..Usimuache vumilia..ila pole sana...mpeleke akasome kidogo ubongo upanuke huoo..

Hilo la shule nilijaribu akaacha, nikamwambia achague fani nimpeleke VETA ili akimaliza nimfungulie ofisi awe msimamizi, bado akakataa. Kuna rafiki yangu kamfungulia duka mke wake Kariakoo akanishauri tuwakutanishe wake zetu ili na mke wangu nifungulie biashara kama hiyo ili ikiwezekana wawe wanasafiri pamoja, lakini kakataa.
 
Tatizo la mke wako ni moja tu, hana kinachomkeep busy. mfungulie biashara...yooote yataisha. idle mind is the workshop of the devil. naakikaa na idle minds wengine ndo wanamjaza upumbavuuu!!
 
ehhh basi huyo anataka roho yakooo:faint:




Hilo la shule nilijaribu akaacha, nikamwambia achague fani nimpeleke VETA ili akimaliza nimfungulie ofisi awe msimamizi, bado akakataa. Kuna rafiki yangu kamfungulia duka mke wake Kariakoo akanishauri tuwakutanishe wake zetu ili na mke wangu nifungulie biashara kama hiyo ili ikiwezekana wawe wanasafiri pamoja, lakini kakataa.
 
Unashindwa nini kuachana na huyo mwanamke mazima??
 
Duh pole sana na hongera kwa kuwa mvumilivu. But mwenye last decision ni ww hata kama watu milion wakikushauri haitasaidia kitu. Fanya maamuz sahihi ambayo unafikir hayatakudhuru. Kwa mazingira hayo unayoishi na mkeo upo at risk position. Amani ni kitu cha msingi sana ktk maisha. Sasa kama mkeo ana tabia hizo unafikiri ni nn hatima ya maisha yako? Tafuta mstakabali wa watoto wako...then fanya maamuzi sahihi
 
Nimeshafikiria kuachana nae na hilo limekuwa wazo linalozunguuka kwenye kichwa changu kwa muda sasa, nimepoteza mapenzi na yeye kabisa. Naona kama tunaishi nyumba mbili tofauti na ninatamani akae mojawapo ya nyumba zetu na mimi nikae nyingine. Ukweli kuna kipindi nilimwambia achukue kila kitu aniache huru tu, kwani najua hana moyo wa kutafuta.

Nimejaribu kumpeleka shule nikijua tatizo litakuwa ujinga akaamua kuacha. Akawa ananilaumu kuwa simpendi kwa kuwa hana kazi nikamwambia afungue biashara nimpe mtaji akakataa. Kuna rafiki yangu amemfungulia duka mke wake aliniomba nimkutanishe mke wake na wangu ili amfundishe biashara, mke wangu akakataa.

Nikajaribu hata kumwambia afungue salon awe anasimamia akakataa. Kila kitu yeye ni mpinzani kwangu na kila ninachofanya yeye anapinga. Nikijaribu ku-support huduma za kijamii anakuja juu kama mbogo. Hakutaka hata nichangie harusi ya ndugu yangu na nilipochanga hakuhudhuria harusi ile. Naishi maisha ya kujitenga na jamii mpaka najiona mpweke. Nimempa hela akafungue akaunti benki ili niwe namuwekea hela ya matumizi huko lakini fomu zina miaka miwili ndani hazijajazwa.

kila kitu anapinga? kwahiyo hata ukimwambia muachane bado atapinga? maana ushauri wangu ni muachane, akipinga na hilo la kuachana basi muache wewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom