Habari wakuu,
Leo ngoja niwashirikishe jambo hili lililonitokea miaka kadhaa nyuma.
Mwaka 2008 nilipomaliza kidato cha 6 nikiwa katika kipindi cha kusubiria kujiunga na chuo nilikutana na binti mmoja tukaanzisha mahusiano. Nakumbuka tulikutana kwa bahati tu kwa maana nakumbuka ilikua siku ya birthday ya rafiki yangu akawa anatoka outing na girlfriend wake akaniambia nimpe company kwani girlfriend wake atakuja na rafiki yake.
Bila hiana nikajumuika nao kusherehekea nakumbuka tulienda beach flani huko Kigamboni DSM. Ili kuwapa privacy jamaa yangu na mpenzi wake ikabidi mimi na yule rafiki wa mpenzi wa jamaa yangu tuwaache tuanzishe ratiba zetu. Hapo ndio na sisi utakaanza kutongozana na kukubaliana hivyo mpaka tukaondoka tukawa couple mbili.
Mapenzi yetu ya kaendelea kwa kipindi kama mwezi mmoja hivi, selection za chuo zikatoka na mimi nikaenda masomoni mkoa wa kaskazini huko. Ila siku chache kabla sijaondoka tulikorofishana hivyo tukawa hatuongei mpaka nikasafiri.
Wakati nipo chuoni tukarudisha mawasiliano, wakati mapenzi yameanza upya kuna siku akaniambia napita hapo mkoani kwenu tukakubaliana ashuke katika basi tuonane kisha ataunganisha basi aendelee na safari.
Kweli ikawa hivyo na siku hiyo nikatoka chuoni mapema nikaenda kumpokea stendi tutaenda mpaka nilipopanga kwani nilikua sikai chuoni. Nakumbuka tukakutana kimwili siku hiyo na ilikua ndio mara yetu ya kwanza. Baada ya hapo jioni nikamsindikiza akapanda basi kuendelea na safari.
Baada ya muda akaniambia hajapata siku zake na anahisi siku ile alishika ujauzito. Nikamwambia kama kweli autos siwezi kuwa baba kwani ndio kwanza nimeanza chuo na sina lolote hakujibu kitu na hatukuongea kwa muda baada ya maongezi hayo. Baada ya muda kupita akaniambia amepata mchumba anataka kumuoa ila anasubiri ajifungue kwanza, nilimuuliza ni mimba nyengine au ile aliyo niambia yangu hakunijibi na hakutaka tuwasiliane tena, na hakupatikana tena kwa namba ninayoifahamu na wala yeye hakunitafuta.
Ni miaka 12 sasa imepita kama ni mwanangu basi ni mkubwa na ningetamani japo kumuona.
Kama upo humu na ukisoma kwa machache nilivyo andika utajijua na utanikumbuka. Nipe jibu kama ni yeye au sio yeye sitokuingilia na maisha yako kwani najua usha-move on kama mimi nilivyoamua kuendelea na maisha yangu.