Nahisi nilipenda nisipopendwa

Nahisi nilipenda nisipopendwa

Zawadia

Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
20
Reaction score
9
Mimi ni mdada mwajiriwa wa serikali.Nilitokea kuwa na mahisiano na mwanaume mmoja ambae hajaajiriwa na yupo chuo kikuu flani cha afya jijini Mwanza,alinitambulisha kwa baadhi ya ndugu zake akiwepo baba na shangazi yake pamoja na baadhi ya marafiki zake.Nilikuwa tayari kwa chochote licha ya dini zetu kuwa tofauti nilikuwa tayari kubadili hata Kama wazazi wangu pamoja ndugu zangu wangenipinga.Wazazi wake wametengana hawaishi pamoja.Na hili jambo ndugu wa baba walikubali lakini ndugu wa mama walipinga hivyo yule kijana akaamua kusitisha Mipango yote na Mimi,Pia ndani ya mwezi mmoja alitangaza ndoa na mwanamke mwingine.Niliumia Sana na kwa jinsi ambavyo nilijitoa kwaajili yake na ndugu zake wengine ni Mungu pekee ndiye anaejua.Ndoa yao imeshapita.Naamini Mungu ni mkubwa siku moja na Mimi atanipatia wanguambae atanipenda kwa dhati na hatimae kuwa mke halali na nikasahau machungu yote ninayopitia.
 
Pole sana.. Usijali ma sr bachelor tupo wengi na tunahitaji watu determined kama wewe unaoneka upo poa sana
 
.Naamini Mungu ni mkubwa siku moja na Mimi atanipatia wanguambae atanipenda kwa dhati na hatimae kuwa mke halali na nikasahau machungu yote ninayopitia.

Pole. kwa kuweka wazi dukuduku lako naamini imepunga machungu japo kidogo.
 
pole sana na karibu pia. humu wapo wengi tu wanatafuta wachumba wa kuoa.
 
Inaumiza sana ukiwa na mategemeo na mtu kumbe yy anakuweka wa akiba,, ipo siku utamuona na atajuta kwa alilofanya
 
Mimi ni mdada mwajiriwa wa serikali.Nilitokea kuwa na mahisiano na mwanaume mmoja ambae hajaajiriwa na yupo chuo kikuu flani cha afya jijini Mwanza,alinitambulisha kwa baadhi ya ndugu zake akiwepo baba na shangazi yake pamoja na baadhi ya marafiki zake.Nilikuwa tayari kwa chochote licha ya dini zetu kuwa tofauti nilikuwa tayari kubadili hata Kama wazazi wangu pamoja ndugu zangu wangenipinga.Wazazi wake wametengana hawaishi pamoja.Na hili jambo ndugu wa baba walikubali lakini ndugu wa mama walipinga hivyo yule kijana akaamua kusitisha Mipango yote na Mimi,Pia ndani ya mwezi mmoja alitangaza ndoa na mwanamke mwingine.Niliumia Sana na kwa jinsi ambavyo nilijitoa kwaajili yake na ndugu zake wengine ni Mungu pekee ndiye anaejua.Ndoa yao imeshapita.Naamini Mungu ni mkubwa siku moja na Mimi atanipatia wanguambae atanipenda kwa dhati na hatimae kuwa mke halali na nikasahau machungu yote ninayopitia.
Cont..Bila aibu akaja kuniomba na mchango wa harusi yake.Nilitaka kumpa lakini badae nikabadili mawazo akasema anajua ni wivu unanisumbua ila sikumjibu kitu chochote.
 
Dah! Unaongea kwa huzuni kweli dada. Pole, utapata tu wako wa kukupenda kama utakavyompenda wewe. Kuwa na subira. Pia unapopata muda uwe unaenda tembea tembea maeneo muafaka, kama ni kwenye masemina, mikutano ya dini (kama ni mkristo),nk. Point yangu ni upate mtu ambaye mna common interest. Pole na Mungu akusaidie.
 
Cont..Bila aibu akaja kuniomba na mchango wa harusi yake.Nilitaka kumpa lakini badae nikabadili mawazo akasema anajua ni wivu unanisumbua ila sikumjibu kitu chochote.

Huyu mbona kama alikuwa na lengo la kukuumiza tu kwa maelezo yako. Au kuna tusilolijua?
 
pole sana jamani
relax jiandae kumpokea wako
kisichorizki hakiliki
 
Pole sana dadaangu, lakini amini kuwa kila mtu na mtuwe, basi jua kuwa hakuwa mtu wako mungu yupo aliyekuandalia muda tu haujafika, vuta subira!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom