Nahisi nilimegewa



Narudisha kauli Mkuu!

Kwa kuwa mwanzo wewe hukujieleza namna hii!

Hivyo binafsi ulinipotosha nilielewa kuwa umetumia zaidi Uanaume wako katika kuamua hili na si mapenzi!

Ila sasa napata picha kuwa toka mwanzo kuwa huyo dada ni opportunist; sijui uliliona hilo tangu mwanzo she stayed with you with hopes kuwa things will work out in her favour! In the end ameamua kuendeleza uhusiano wa zamani!

Hapo sikulaumu hata mimi would have done the same!
 

Hahahahaaa....unaona sasa? Haya hebu niambie weye, ingekuwa wewe ungemzuiaje demu aisende? Maana watu wananilaumu mimi kwa 'kumwachia' aende? Na wamekimbia kabisa hawataki kuja hapa na kutoa maoni yao ya jinsi gani ningemzuia zaidi ya kile nilichokifanya.

Kwa maoni yangu, mtu yoyote mwenye chembe ya busara za kawaida angefanya kama mimi nilivyofanya. Sasa huenda kuna njia nyingine ambayo ningeweza kutumia kumzuia asiende. Can you think of any?
 
Hahaha hiyo kali...kweli umpelekee simba nyama aitazame hata kama hana njaa ataichezea
 
Mkuu ulikuwa sahihi kabisa....Nimesoma tena na tena nadhani uwamuzi wako ni wa kiume na sahihi.....Swali> Je baada ya mdada kurudi na kukataa kuendeleza uhusinao nini kinaendelea
 
Mkuu ulikuwa sahihi kabisa....Nimesoma tena na tena nadhani uwamuzi wako ni wa kiume na sahihi.....Swali> Je baada ya mdada kurudi na kukataa kuendeleza uhusinao nini kinaendelea

She's now my booty call.....

Kumbe na wewe umeona eeh? Yaani uamuzi wangu ulikuwa zaidi ya sahihi! Nashukuru kwa wewe nawe kuliona hilo.
 
aaaaaah Brasilian friend kumbe uliuvunja uhusiano wenu ..pole sana ila ulitakiwa uwaze mara mbili mbili..mie sina hakika sana kama walimegana
 
Baada ya kurudi nilimwuliza kama alimegwa na yeye alikataa katakata. Mimi kwa upande wangu sikumwamini hata kidogo na nikamwacha.

Kumbe mnasomaga vitu nusunusu halafu mnarukia mahitimisho eeeh? Hiki kipande ni kutoka bandiko langu la mwanzo. Hukuona kuwa nilisema nilimwacha?

aaaaaah Brasilian friend kumbe uliuvunja uhusiano wenu ..pole sana ila ulitakiwa uwaze mara mbili mbili..mie sina hakika sana kama walimegana

Lakini wewe unakwepa swali langu. Wewe ulisema/ulihoji kuwa kwa nini nilimruhusu au kwa nini nilimwachia aende. Nikakujibu kuwa zaidi ya kupinga kwa maneno kile alichokuwa anataka kufanya hakuna jingine zaidi ambalo mimi ningeweza kufanya. Sasa wewe unadhani ningemzuiaje kwenda zaidi ya kumweleza kuwa sikupendezewa na hilo wazo la yeye kwenda? Acha kucheza mchiriku, jibu swali langu tafadhali.
 

Ok ok thank you Brasil nimekuelewa vema sana siulizi tena
 


remember old is gold
 
Sidhani kama hapa kuna la kuumia maana makosa ya kumruhusu tayari yalishafanyika. Kama vile ulivyopiga moyo konde pale ulipoamua kuishi naye na kuanza kummega wakati ulijua kuwa tayari alishamegwa! Rudia tena kuupiga konde moyo na songa mbele. Usimwache kama bado.
 
Sidhani kama hapa kuna la kuumia maana makosa ya kumruhusu tayari yalishafanyika.

Ok, let me try to make sense out of this nonsense. Hayo makosa ya "kumruhusu" alifanya nani? Unajaribu kusema mimi ndiye niliyoyafanya? Kama ni hivyo nilimruhusu kivipi wakati mimi niliweka wazi pingamizi langu na yeye akaamua kwenda licha ya hilo pingamizi langu. Ningefanya nini zaidi? Nijuze tafadhali

Kama vile ulivyopiga moyo konde pale ulipoamua kuishi naye na kuanza kummega wakati ulijua kuwa tayari alishamegwa!

Hapa ndio kabisa sielewi hata ulichokuwa unamaanisha ni nini. Watu wazima wanaokutana ukubwani na kuanza uhusiano wa kimapenzi mara nyingi wanakuwa tayari wameshamega na kumegwa. Sasa hoja yako hapa hasa ni ipi? Wewe hujawahi kumega (au kumegwa) mtu ambaye keshamegwa na wengine kabla yako? Mantiki zingine bana aaah...zinaweza kukufanya uanze kunyofoa nywele zako kama yule mwendawazimu Juma Kilaza.

Rudia tena kuupiga konde moyo na songa mbele. Usimwache kama bado.

Matatizo ya kukurupuka na kusoma vitu kwa juu juu bila kuvielewa ndio haya sasa. Unatoa rai eti nipige moyo konde na nisonge mbele wakati nimesema tokea mwanzo kuwa hili jambo lilitokea miaka kadhaa iliyopita (mwanzoni mwa muongo huu kwa usahihi zaidi). Umeanzia wapi kuisoma hii mada?
 
Yaani ningekuwa karibu na wewe ningekupa bonge la HUG!duuh kumbe wengine hatujakua-kiukweli naomba uwe my online sissy. Mimi pia ningekula mzinga. Kwa hiyo dada Noname una maana kikawaida huyo dada kamegwa?i.e labda huyo dada si kama tunaowaona maofisini na njiani ndio anaweza kuwa salama?Duuuu:crying:?
 

Duu mkuu Brasil-habari za Ikungulyabashashi?Nakusifu kwa kuwa watu wengi walisema uliwezaje kumuachia m laddy wako kwenda huko kwenye simba mla watu?Lakini walikuwa hawajui kuwa mawazo yako na wao ni sawa i.e aliondoka akijua kuwa contract imekwisha!
Ungekuwa kijini kwetu ingebidi ukaoshwe usije ukaangukiwa na mkasa kama huo tena maishani/au uksaliwe msikitini au kanisani-duuuu ulichokiona ndio 100% compatible kinaondoka unakiona hivi hivi?Ila ngoja tumsikie dada Fladdy atueleze mwanamke akitaka kuondoka unamzuiaje-huo utaalamu tunausubiri.Akisahau m PM na mm unitumie hiyo risepta. Na mwisho sasa huyod ada bado yuko humu mitaani nijaribu kama naweza kumdhibiti?Maana nasikia kuna mitishamba ungemuwekea kwn maji asigeweza kuondoka angekuwa anaona vinyota tu,nitupie kontakti nimjaribu :amen:
 

Za Ikungu mhola kabisa! FL1 kashindwa hoja na kaja na viroja vya eti kanielewa vema na hataniuliza tena as if kusema hivyo ni kujibu swali nililomwuliza. Na hakuna hata mmoja wao hawa great thinker aliyekuja na pendekezo la jinsi gani ningemzuia kwenda zaidi ya yale vile nilivyofanya mimi.

Mtu mzima akiamua kufanya jambo atafanya tu. Labda umvalishe straight jacket na kumfungia selo. Na ukifanya hivyo hayo siyo mapenzi tena.
 
Mayyyne, i need to find time to go thru the entire thread... kinda touchy issue!
 

Ngoja nikusanye list ya kina dada -bahati mbaya dada FL1 labda amegadhibika,tuwatumie PM,mmoja baada ya 1 huenda tukapata muungwana akatuambia njemba yake ilivyomzuia. Nilipokuwa DAR nilikuwa naona vibao vimeandikwa dawa ya kumvuta mpenzi wako-hata kama yuko nchi nyingine,labda kuna mtu atatuambia zinafanya kazi,kama ungemuweka hiyo labda asingeondoka au kama si hivyo labda jamaa aliisha apply kule kwa hiyo shemeji(who was supposed to be)alikuwa anavutika kama mbwa na mdomo wa chatu. Pole ndg yangu-lakini sasa umekuwa kama mtu aliyen'gatwa na nyoka eeeeeeh?:A S-confused1:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…