Nahisi mtalaka wangu bado ananiandama

Nahisi mtalaka wangu bado ananiandama

Wanajamvi habari za majukumu?

Nina mambo kadhaa yanayonisumbua akili yangu na kuninyima amani sana. Kwa wale wanaokumbuka tatizo nilopata la aliyekuwa mume wangu kumpa mimba mdogo wangu, hichi nadhani ndo kimekuwa chanzo cha kuniweka katika wakati mgumu.Tangu nilipoamua kuachana nae nimekuwa napitia matatizo tofauti hii inananifanya nihisi yeye ndiye muhusika wa yote.

Kwanini nasema hivi ni kwa sababu zifuatazo;

Nikiwa na wiki tatu tangu tuachane nilivamiwa nyumba na wanaume sita walikuwa wamevaa kininja bahati nzuri walinipita nje na kumkuta house girl wakaishia kumbaka na kumsababishia maumivu makali.Nililipoti polisi na nikafuata taratibu zote za kisheria ndipo nikampeleka hospital na kupatiwa matibabu.

Nilipomuhoji hg walichomwambia kabla ya kumbaka analinijibu walimwambia kuwa anaringa sana na hivyo vijisent vyake, baada ya kusikia vile nikajua mlengwa nilikuwa mimi na walidhani yeye ndiye mimi kwakuwa miili yetu ni kama tunalinga.Nilipoona vile nikaamua kuhamia nyumba yangu nyingine ambayo nilitaka kuipangisha.

Lakini napo baada ya wiki moja tangu nimehamia pale tena nilivamiwa na safari hii ikiwa ni usiku wa saa nane. Niliponea chupuchupu baada ya kujificha choo, safari hii wakabeba baadhi ya vitu vya thamani ikiwemo TV na laptop pamoja na simu. Wakati naendelea kutafakari hayo nikiwa njiani narejea nyumbani nikiwa naendesha gari ghafla ikatokea gari nyingine mbele yangu ikija kwa kasi sana huku ikiyumba pande zote za barabara nikaamua kusimama baada ya kuhofia kugongana.

Niliposimama tu ile gari ikaniblock ghafla wakatelemka wanaume wanne wakiwa wamevalia kininja wakaniamuru nishuke kwenye gari wakati nateremka ghafla ikatokea gari ya polisi wakiwa doria wale majambazi wakawa wamekimbia, ikawa salama yangu tena.

Ndipo nilipoamua kuhama tena na Leo hii nina siku kadhaaa tangu nimehamia hapa. Najiuliza nini sababu ya haya yote, naishia kuhisi huenda mtalaka wangu ndiyo muhusika mkuu bado sina hakika sana. Nawaza kumfuata nimwambie nimebaini kuwa yeye ndiye muhusika na wakati mwingine nawaza kumshitaki polisi, nipo njia panda naomba ushauri wenu please ili niishi kwa amani.

Asanteni.
Hii story umecopy kwenye move inaitwa perfect man.
 
Kama unahela kwnn usitafute ulinzi hasa wa nyumba kuna kampuni nyingi mjini zinatoa huduma hiyo weka hata security g hata 3 wenye silaha
 
kama ni kweli naona mwisho usio mzuri. Toa taarifa kitu cha polisi cha karibu kuhusu
matukio yote, waeleze kuhusu mtu unae mshuku, tembea na watu wawili au watatu na tafuta mlinzi nyumbani, badili ratiba yako.Mungu akujalie uzima
 
najitolea kukulinda kwa mda wa mwezi mmoja uko tayari? nimefatilia sana story yako.
 
Katoe taarifa polisi! Au nenda kwa bibi amwoteshe busha mtu hapo
 
Tatizo lako hukuwaeleza ukweli polisi, ulificha mambo yako mengi sasa ulidhani au unadhani polisi watakusaidiaje?

Nenda polisi tena utoe taarifa ya kina toka mwanzo hadi mwisho mwa tukio then watakusaidia.
 
ripoti polisi, then tafuta mlinzi binafsi....wapo askari wastaafu wa jeshi ndo dili zao hizo,,, aidha chunguza kujua mhusika then anza mashambulizi kwake......kuna ma-private investigeta cku hz.....
 
polisi unaenda kuripoti kupotelewa simu au.....kanyooshe maelezo, kingine huyo jamaa atakuwa bwege kabisa
 
Huu ni mtihani mkubwa sana kwako;
mwisho wataondoka na roho yako;
tafuta tu suluhu, kubali yaishe;
uko kwenye hatari kubwa sana
kama uliyoyaandika ni kweli;

Mfuate kwake myamalize;
ukute na yeye ni hao hao mmmh.
 
TE="Consultant, post: 17059994, member: 11015"]Wewe usimconfront. Nenda police ukatoe maelezo. Connect matukio yote. Police wana mbinu nyingi siku hizi na wanaweza hata kuaccess mawasiliano yake ya simu.[/QUOTE]

Kama alivyoshauri mjumbe hapa..DO NOT COMFRONT HIM AT ALL,kuna mambo mengine yaweza jitokeza ambayo unaweza yaepuka kama huto-mkomfront ana kwa ana..(infact ndicho anachotaka/anachotegemea ww umfuate)
Report entire story,.na mtiiriko wa matukio yote na kwanini una sababu za kushuku kuwa mtalaka wako ndie anaefanya hayo yote.
 
Uwe very serious na hii ishu aisee.usichukulie poa jammaa inabid ahojiwe polisi na polisi wamtengeneze mazingira ajuwe kabisa anafatiliwa na polisi.polisi pia wanaweza kutumia mbinu za kiintelligencia kumfatlia
 
Walinipita nikiwa nje ya nyumba niliyokuwa naishi pana salon nilikuwa pale sikujua kama wanakwenda kwangu so nikaendelea na kusukwa baada ya kumaliza yao ndo hg akanipigia simu nilipokwenda mbio nikaitambua ikimalizikia kuwa ndiyo ile iliyonipita nje nikiwa salon

Pole sana dada yangu.
Hukuweza hata kukariri sura? au ni watu wageni kabisa machoni pako
 
...sounds like a baked story, wakati huyo hg anabakwa, yeye alikuwa nje, hakuchukua hatua yoyote wakati wanaume sita wakimbaka? Wanaume sita kubaka mwanamke mmoja takes long, kuna ukakasi hapo.

Lakini hata tukio la pili la kuvunjiwa nyumba, huku akiponea chupuchupu huko chooni lina ukakasi, lakini pia hata hilo la kublokiwa na hao maninja then polisi wakapita na jamaa kukimbia lina ukakasi.

It must be ''well baked''
 
Wanajamvi habari za majukumu?

Nina mambo kadhaa yanayonisumbua akili yangu na kuninyima amani sana. Kwa wale wanaokumbuka tatizo nilopata la aliyekuwa mume wangu kumpa mimba mdogo wangu, hichi nadhani ndo kimekuwa chanzo cha kuniweka katika wakati mgumu.Tangu nilipoamua kuachana nae nimekuwa napitia matatizo tofauti hii inananifanya nihisi yeye ndiye muhusika wa yote.

Kwanini nasema hivi ni kwa sababu zifuatazo;

Nikiwa na wiki tatu tangu tuachane nilivamiwa nyumba na wanaume sita walikuwa wamevaa kininja bahati nzuri walinipita nje na kumkuta house girl wakaishia kumbaka na kumsababishia maumivu makali.Nililipoti polisi na nikafuata taratibu zote za kisheria ndipo nikampeleka hospital na kupatiwa matibabu.

Nilipomuhoji hg walichomwambia kabla ya kumbaka analinijibu walimwambia kuwa anaringa sana na hivyo vijisent vyake, baada ya kusikia vile nikajua mlengwa nilikuwa mimi na walidhani yeye ndiye mimi kwakuwa miili yetu ni kama tunalinga.Nilipoona vile nikaamua kuhamia nyumba yangu nyingine ambayo nilitaka kuipangisha.

Lakini napo baada ya wiki moja tangu nimehamia pale tena nilivamiwa na safari hii ikiwa ni usiku wa saa nane. Niliponea chupuchupu baada ya kujificha choo, safari hii wakabeba baadhi ya vitu vya thamani ikiwemo TV na laptop pamoja na simu. Wakati naendelea kutafakari hayo nikiwa njiani narejea nyumbani nikiwa naendesha gari ghafla ikatokea gari nyingine mbele yangu ikija kwa kasi sana huku ikiyumba pande zote za barabara nikaamua kusimama baada ya kuhofia kugongana.

Niliposimama tu ile gari ikaniblock ghafla wakatelemka wanaume wanne wakiwa wamevalia kininja wakaniamuru nishuke kwenye gari wakati nateremka ghafla ikatokea gari ya polisi wakiwa doria wale majambazi wakawa wamekimbia, ikawa salama yangu tena.

Ndipo nilipoamua kuhama tena na Leo hii nina siku kadhaaa tangu nimehamia hapa. Najiuliza nini sababu ya haya yote, naishia kuhisi huenda mtalaka wangu ndiyo muhusika mkuu bado sina hakika sana. Nawaza kumfuata nimwambie nimebaini kuwa yeye ndiye muhusika na wakati mwingine nawaza kumshitaki polisi, nipo njia panda naomba ushauri wenu please ili niishi kwa amani.

Asanteni.
pole dada njoo nikupe hifadhi mimi nina manati ya kizungu bastola nitakuwa bodyguard wako popote utakapokwenda,sure you need a bodyguard nipe hiyo kazi mpaka tuwajue hawa watu
 
Hujaamua kujilinda, upo nyoronyoro sana.
 
Back
Top Bottom