Nahisi mtalaka wangu bado ananiandama

Nahisi mtalaka wangu bado ananiandama

leah2

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2015
Posts
584
Reaction score
1,442
Wanajamvi habari za majukumu?

Nina mambo kadhaa yanayonisumbua akili yangu na kuninyima amani sana. Kwa wale wanaokumbuka tatizo nilopata la aliyekuwa mume wangu kumpa mimba mdogo wangu, hichi nadhani ndo kimekuwa chanzo cha kuniweka katika wakati mgumu.Tangu nilipoamua kuachana nae nimekuwa napitia matatizo tofauti hii inananifanya nihisi yeye ndiye muhusika wa yote.

Kwanini nasema hivi ni kwa sababu zifuatazo;

Nikiwa na wiki tatu tangu tuachane nilivamiwa nyumba na wanaume sita walikuwa wamevaa kininja bahati nzuri walinipita nje na kumkuta house girl wakaishia kumbaka na kumsababishia maumivu makali.Nililipoti polisi na nikafuata taratibu zote za kisheria ndipo nikampeleka hospital na kupatiwa matibabu.

Nilipomuhoji hg walichomwambia kabla ya kumbaka analinijibu walimwambia kuwa anaringa sana na hivyo vijisent vyake, baada ya kusikia vile nikajua mlengwa nilikuwa mimi na walidhani yeye ndiye mimi kwakuwa miili yetu ni kama tunalinga.Nilipoona vile nikaamua kuhamia nyumba yangu nyingine ambayo nilitaka kuipangisha.

Lakini napo baada ya wiki moja tangu nimehamia pale tena nilivamiwa na safari hii ikiwa ni usiku wa saa nane. Niliponea chupuchupu baada ya kujificha choo, safari hii wakabeba baadhi ya vitu vya thamani ikiwemo TV na laptop pamoja na simu. Wakati naendelea kutafakari hayo nikiwa njiani narejea nyumbani nikiwa naendesha gari ghafla ikatokea gari nyingine mbele yangu ikija kwa kasi sana huku ikiyumba pande zote za barabara nikaamua kusimama baada ya kuhofia kugongana.

Niliposimama tu ile gari ikaniblock ghafla wakatelemka wanaume wanne wakiwa wamevalia kininja wakaniamuru nishuke kwenye gari wakati nateremka ghafla ikatokea gari ya polisi wakiwa doria wale majambazi wakawa wamekimbia, ikawa salama yangu tena.

Ndipo nilipoamua kuhama tena na Leo hii nina siku kadhaaa tangu nimehamia hapa. Najiuliza nini sababu ya haya yote, naishia kuhisi huenda mtalaka wangu ndiyo muhusika mkuu bado sina hakika sana. Nawaza kumfuata nimwambie nimebaini kuwa yeye ndiye muhusika na wakati mwingine nawaza kumshitaki polisi, nipo njia panda naomba ushauri wenu please ili niishi kwa amani.

Asanteni.
 
Pole sana dada, itakuwa ni huyo mtalaka we chunguza zaidi
 
Njoo zanzibar nikuhifadhi kwa mda mpaka mambo yatulie
 
... Najiuliza nini sababu ya haya yote, naishia kuhisi huenda mtalaka wangu ndiyo muhusika mkuu bado sina hakika sana. Nawaza kumfuata nimwambie nimebaini kuwa yeye ndiye muhusika na wakati mwingine nawaza kumshitaki polisi, nipo njia panda naomba ushauri wenu please ili niishi kwa amani..

Wewe usimconfront. Nenda police ukatoe maelezo. Connect matukio yote. Police wana mbinu nyingi siku hizi na wanaweza hata kuaccess mawasiliano yake ya simu.
 
Duuuhh kazi kweli kweli.

Ni vizuri ukaripoti Polisi na kujieleza kinagaubaga.

Ni vizuri pia ukatafuta Muda mzuri wa kukaa pamoja na huyo "bwana" na kumueleza ukweli wa jambo hili. Lakini muweke wazi atambue katika maisha wakati mwingine ni vizuri kukubaliana kutokubalia ili kila mmoja awe na amani.
 
Dada una moyo kweli, Matatizo yote hayo bado hujatafuta msaada wa ulinzi wako? unasubiri nini? Nenda karipoti hilo mara moja na ikibidi hata hapo pia uhame tena usije ukapata shida.
 
Kila unapohamia hao majambazi wanajua ulipo! Nahisi kutakuwa na mtu wako wa karibu sana mwenye kutoa habari wapi ulipo. Chunguza house girl, ndugu yako au shoga zako. Siwezi kumuhusisha ex- Wako moja kwa moja ikiwa wewe mfanya bisashara. Hujamtenda(kumuimbia) mwezio? Pia badilisha cm card yako inawezekana kuna mtu anakutrack hatua zako zote.
 
kuzoea dezo mwanaume halafu ukazikatisha gafla sio rahisi akubali! inshort eleza police wasiwasi wako juu yake watamuweka kiti moto litalotokea juu yako linamhusu ataacha
 
Kwa usalama wako kabla hawajapajua home, badilisha hiyo gari, ikibidi kama una rafiki mbadilishane au iuze ili uwachanganye, usikute wanakufuata hadi kwako Kwa kuifatilia gari yako, pia ihusishe polisi watakusaidia, nahisi amepanga akutoe uhai, kama unaweza hamia hotelini yenye ulinzi wa uhakika Kwa muda, wakati ukijipanga kubadili Gari na polisi kufanya uchunguzi.
 
Nenda polisi katoe maelezo na mshuku wako wakwanza Ni huyo then kaa utulie
 
Back
Top Bottom