Nahisi mpenzi wangu hajui kusoma

Nahisi mpenzi wangu hajui kusoma

ana wivu sana hapendi kuona simu zikiingia nyakati za usiku
Mwambie umuhimu wa kuwa na simu bana simu zingine huwezi kuzi ignore avumilie tu ataweza na atakuelewa! Ila duh miezi miwili tayari mnalala mnaamka????
 
mwenzangu hata mimi nilidate na mtu wa hivo
alikua ananipenda
mtu smart maisha vizuri tu
kazi alikua ananificha..


lakini hajibu sms
tumekaa mwaka na nusu hajawahi kujibu sms
ukituma sms anapiga ,anauliza ulikua unasemaje
ukimwambia asome anakwambia aaah achana nayo niambie..

nikamchunguza nikaona atakua hajasoma
sasa nikamtumia sms ya matusi siku moja...

akakaa sijui akatafuta mtu akamsomea
nikampigia akasema umentukana..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nikamwambia hivo hivo...

huyo dada hajasoma
 
Anakupima huyo..we jidanganye hajui kusoma itakula kwako.......mtumie tigo pesa uone atasemaje.
 
Eti kwa kuwatia moyo hahaha mkuu asa anajiongezaje kama hajiwezi na hakuweza hapo nyuma
mbona inawezekana, kipindi cha nyuma nikiwa home, tuliishawahi kuwa na housegirl hajui kusoma, tukumnunulia vitabu na kumpa intro tu ya kuandika na kusoma mfano : ka ke ki ko ku, ba be bi bo bu, nk, so siku ukimwandikia neno "kaba" wala hahangaiki kulisoma maana ni just kuunganisha hizo sijui ndui silabi, so alikuwa anajiongeza mwenyewe, na alijua fasta.
 
Kudadadeki.

Mzee kama kwenye Chemistry hii ingeitwa "litmus test" ya kujua kama kuna alkali au tindikali
Ha ha ha ha kwel K abisa mkuu..... anamalizia na Hence proved
 
Mbona kusoma Na kuandika sio tija hta Kama hajui Anapelekwa course tuu mkuu

Jiulize wewe unampenda Na je Una malengo nae pia Ana qualification za mwanamke unayemtaka Kama ndio muulize tuuu
 
Usiishie kuhisi mpe msg maneno akusomee akizuga mwambie kiupole awe wazi kwako kwamba uko tayari kumfundisha lols
 
Wapo....kuna mwanaume me namjua hajui kusoma kabisaaaa....wala hasev namba...ila ukipiga anajua huyu ni nani kwa kuangalia namba za mwisho....na ukituma mesej anakupigia... atazuga hajaiona au alikua bize....
Hahahaha...dah!
 
Unataka ajue kusoma kwani Unaoa Hakimu au Mwalimu? Oa mchuchu huyo maadam atakupa tulizo la moyo! Watu wa namna hio wnakuaga na Nidhamu Sana na ni watafutaji balaa ili kuji cover
 
Hapendagi tu kuandika meseji na kusoma sidhan kama ulimwengu wa leo mtu yupo town asijue kusoma na kujibu msg tena mwanaume, apo ni mtego ww rukaaaaaa
Wapo kibao,jirani hapa hajui kusoma wala kuandika mume anachat na hawara hapo!!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] looooohhh!!

Mungu anakuona!
Ha ha ha mim n meuliza tu ki ukwel maana ni msg muhimu sana hyo
 
Rafiki zangu walimfundisha mama yao kusoma na sikuhizi anasoma Bible vizuri tu. Hakupata nafasi ya kwenda shule alipokuwa mdogo, na mzee alipoanza kazi alirudi kijijini kutafuta mchumba, posa ilipelekwa kwa binti mrembo na akawa mke wa kibosile baadae. Alipopata watoto, baba akawa anawafundisha wanae nyumbani jioni kusoma na kuandika na mama anajoin in.
 
Nilisha wahi kuwa na demu anaitwa Mariam demu alikuwa hajui kusoma wala kuandika! Nikamwambia nakupeleka shule anajibu hawezi kukaa na watoto wakati ana miaka 15 fasta nikampiga chini
 
Back
Top Bottom