Akaunti fake ilivyorudisha mahusiano yangu na mpenzi wangu kwa haraka sana

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Habari wanajamvi,

Bila kupoteza muda, hivi karibuni nimejikuta kwenye mateso ya kimapenzi baada ya kuhitilafiana na mpenzi wangu.

Jinsi ilivyokuwa
Nina mpenzi wangu ambaye tumekuwa kwenye mahusiano ndani ya miezi kadhaa iliyopita, anakaa mtaa wa pili kutoka mtaa ninaokaa. Wiki moja iliyopita niliingia kwenye mgogoro mkubwa wa kimapenzi ambapo ulivunjika ila baadae nikaurudisha kwa kutumia ubunifu wa hali ya juu ndani ya siku tatu. Ni baada ya kunifumania nikiwa katika harakati za kumgegeda mwanamke mmoja ambaye nafanya naye kazi

Kiukweli huyo mpenzi wangu ambaye nampa jina la Stella (ila siyo lake) alikuja kwangu bila taarifa akanikuta live nikila mate na Fatuma na tukiwa tupo vifua wazi na huyo dada wa ofisini ambaye nampa jina la Fatuma.

Ilikuwa ndio siku ya kwanza kutaka kumgegeda Fatuma baada ya kumfukuzia kwa muda wa mwezi mmoja huku akipiga chenga na kunifanyia utafiti kama nina mpenzi mwingine. Kwa uwezo wangu wote nilijitahidi kumficha Fatuma kama nina mpenzi mwingine muda huo ananifanyia uchunguzi mpaka siku ya tukio.

Wakati namuandaa Fatuma tukiwa sebuleni sikufunga mlango, niliwaza kuwa ngoja nimuandae akiwa tayari, nitafunga mlango wa sebuleni kisha nishike mkono nimpeleke chumbani kwa ajili ya kazi, kumbe ndio Stella anaingia bila hodi.

Niliishiwa pozi, Stella akitetemeka aliuliza huyu ni nani? Nikaishiwa pozi na Fatuma akashindwa, kuongea na akahamaki. Fatuma aliamka kutoka pale kwenye sofa akasimama akavaa blazia na blauzi yake na kuchukua mkoba na kuondoka bila hata kuongea neno.

Stella alinigombeza akaniambia mimi na wewe mapenzi basi na kuondoka, nilibaki nimeduwaa, na kujilaumu nimefanya nini hiki, muda huo ilikuwa saa 12 jioni. Nilinyanyuka kwenye sofa baada ya kufikiria kama dakika 45 na kwenda kuoga.

Nilijaribu kumpigia Fatuma ili nimuombe msamaha kwa lililotokea hakupokea simu, nikampigia Stella akawa ameisha niblacklist, akaniblock WhatsApp, nikachoka mwili mzima. Kiukweli nilikuwa bado namhitaji Stella, na bado nilikuwa nampenda sema tu ni ile hali ya tamaa za wanaume.

Usiku huo nilienda kwa Stella kuomuomba msamaha lakini niliambulia maneno makali ya dirishani na mlango haukufunguliwa na sikupewa hata nusu dakika ya kujitetea. Nikaamua kurudi kwangu nikiwaza kweli Stella ataniacha, nifanyeje asiniache, bado nakupenda Stella, niliwaza usiku kucha.

Siku iliyofuata ilikuwa siku ya weekend hivyo nilibaki ndani nikiwaza kuhusu tukio la jana na Stella kuniacha. Wakati nawaza nikapata mbinu ya kumfanya Stella arudishe mapenzi yake kwangu, asiniache.

Kipindi cha nyuma wakati naanzisha mahusiano na Stella, aliniuliza kama nina mtu mwingine, nikasema "Kwa vile nakupenda nitakwambia ukweli, nilikuwa naye ila sikutembea naye na mpango wa kutembea naye sina." Hayo majibu hayakuwa ya kweli, ukweli ni kuwa katika kipindi hicho sikuwa na mtu.

Akaniuliza "Kwa nini unataka kumuacha unanitaka mimi?" Nikamwambia, "Huyo mwanamke ananitongoza mwenyewe, na mimi simpendi, ananilazimisha tu lakini namkwepa, ila uzuri ni kuwa sijawahi kutembea naye, ila kwako nimedata." Hayo maneno hayakuwa ya kweli, lengo ni kutaka kumuaminisha kuwa na mimi naweza kupendwa na kutongozwa na mwanamke, huyo mwanamke nikampa jina la Haika.

Ili nimuaminishe zaidi nikafungua akaunti fake Facebook, nikatafuta picha ya mwanamke mrembo miongoni mwa marafiki zangu nikaiweka kwenye profile hiyo, nikaomba marafiki wachache lakini baada ya saa moja nikawa na friendrequst zaidi ya 1000, wengi wao wakiwa wahindi nikazikubalia request zote.

Kisha nikaingia messenger nikaanza kuchati na Stella kwa jina hilo la Haika John. Nikamwabia samahani dada, wewe ni kweli ni mke wake Maga? Stella akajibu "kwa nini uulize hivyo?" Nikamwambia huyu kaka Maga nilikuwa naye kwenye mahusiano lakini sasa hivi amebadilika na kuniambia ana mke tayari anaitwa Stella kama vipi mtafute FB atakwambia ukweli, ndio nimekutafuta."

Stella akasita kuwa wazi akajibu, mmmh mimi sidhani, Stella akauliza kwani mmekuwa naye kwa muda gani? Nikajifanya Haika nikajibu, "Wiki mbili". Akauliza je, umewahi kutembea naye? Nikajibu hapana, kisha Stella akasema ni kweli alichokwambia mimi ndiye mkewe.

Nikajibu asante dada, maisha mema, kumbe huyu kaka alikuwa ananidanganya, nikalog out, dakika chache tu Stella akanipigia, akaniulizia kuhusu huyo Haika, nikamwambia baada ya kuona ananisumbua nilimwelekeza FB akutafute ili ukufaham kuwa wewe ndiye mke wangu asiwe ananisumbua, vipi amekuambiaje?

Stella akajibu "Ameniliuza tu kuwa wewe ni mke wa Maga nikasema, muulize yeye atakwambia mimi sina majibu." Nikacheka moyoni, nikajisemea ungejua kuwa uliyechat naye ni mimi usingesema hivyo". Pia nikajisemea moyoni hapa kazi imeisha, Stella amesema vile kwa akaunti ya Haika basi kazi imeisha.

Baada ya siku mbili tukaanza mapenzi na Stella, baada ya siku mbili zingine nikafungua akaunti nyingine, nikaipa jina Joyce Sera, nikamfuata Stella inbox nikachat nikilaumu Haika alivyo na mpango wa kumnyang'anya mpenzi, anavyotamba kuwa atakunyang'anya Maga hawezi akakubali kiurahisi.

Stella naye akajibu, "Imekula kwake atafute tu mwingine, Maga nimeisha mmiliki." Pia kupitia hiyo akaunt ya Joyce nikajifanya adui namba moja wa Haika. Stella alifurahishwa na Joyce kwa kumpinga Haika, huyu Joyce alijitambulisha kama mdogo wake Haika, basi Stella akamuona Joyce kama mtu wake wa karibu sana hivyo akamuomba namba ya simu ili wawe wanawasiliana na kuwa mashoga.

Baada ya Stella kuomba namba nikafikiria namba ya simu nitaitoa wapi, nikapata wazo la kumuomba dada mmoja kama ana line ambayo haitumii kwa bahati nzuri alikuwa nayo, nikachukua namba za simu, nikamtumia pia naye Stella akaweka namba yake pale inbox.

Ile line ya simu nilichokifanya nikaifungulia akaunti WhatsApp, kisha nikaitunza mahala. Simu yangu nikaiwekea double space WhatsApp ,upande mmoja ni mimi upande wa pili ni Joyce. Nikawa nachat na Stella kwa upande wa pili wa WhatsApp kama Joyce nikimpondea Haika na pia nikajifanya namfahamu Maga, nikamsifia maga kwa maneno mazuri mazuri kibao.

Uzuri ni kuwa Stella hakuwahi kupiga hiyo simu kuongea kwa njia ya sauti, yeye alijikita kuchat nayo WhatsApp, hayo ndiyo yaliyokuwa yametokea kipindi hicho namtongoza Stella.

Baada ya hili fumanizi akili ikanituma kuanza ule mchezo wa Haika na Joyce. Siku hiyo nikaanza kuchati na Stella kwa WhatsApp kwa akaunt ya Joyce kama shoga yake. Vipi Stella hujambo? Akajibu "Sijambo, vipi mwenzangu kulikoni na Maga mbona ameniomba namba za Haika, pia ananiomba nimuombee msamaha, kwa kumkataa Haika ambaye alikuwa anampenda kiasi kile," Stella akachelewa kujibu, ila baadae akamwambia mpe tu.

Nikasemea moyoni "Duh, ngoma bado ngumu", basi nikaendelea kuchati naye nampondea Haika, baadae nikajifanya kimya kidogo kuwa kama vile naongea na Haika kuhusu ombi la Maga, kisha nikanza kuchat tena, "Unajua shoga ni nini cha ajabu, Haika kakubali, jamani shoga unamuachia Haika mume? Stella hakujibu.

Nikajifanya kutulia, ilipofika jioni, nikaanza kuchat naye, "Shoga vipi, naona Haika anaandaa safari kwenda kwa Maga kesho kwa hiyo ndio anaenda kuyajenga hivo, kaishatumiwa nauli shosti. Hapo Stella akaanza kujibu "Kweli shoga?". Nikajibu ndiyo, tena asubuhi atakuwa amefika kwa Maga. Hakujibu akapiga kimya, basi na mimi nikaona haya mambo ni mazito.

Ikawa saa saba za usiku nikasikia message inaingia, kuangalia ni Stella akiniambia njoo sasa hivi hapa kwangu naumwa sana unipeleke hospital. Nikaamka kitadani paap nikasimama, na kuanza kucheka, mimi ndio Maga kwa kweli, kazi imeisha.

Nikavaa fasta nikaenda mpaka kwake, akafungua nikaingia chumbani, akanza kulia kwa nini namtesa, basi nikamtuliza, nikamuomba msamaha yakaisha, tukalala mpaka asubuhi, ila hakuniulizia kuhusu safari ya Haika.

Kesho yake akaniambia ataenda kwangu kushindiapo, hataenda kazini kwake, hivyo nimuachie ufunguo pale ninapoweka, nikasema haina shida, nikaenda kwangu kwa furaha nikaoga nikaenda kazini.

Stella alienda kwangu ile asubuhi na kufanya usafi, kupika na kuingia kitandani kupumzika, kisha akatext WhatsApp akimuuliza Joyce kuhusu safari ya Haika kwa Maga, nikamjibu wamezenguana asubuhi hivyo hana tena mpango. Nikacheka mpaka wenzangu wakaniuliza vipi bro umepata Tatu Mzuka nini?

Mwisho hii stori si ya kutungwa ni ya kweli, vijana unapaswa utumie ubunifu katika mapenzi kuliko kutumia nguvu kubwa kwa mambo kama haya.

Asanteni.
 
Hawa viumbe bila kutumia akili nyingi watakuoshea sana kama le mutuz. Ukijifanya Good boy kuwaambia ukweli watakuburuza sana. Dawa yao ni kuwadanganya tu
 
hizi akili ungetumia kwenye uvumbuzi na teknolojia ama kutafuta salary mkuu ungekuwa unamfukuzia mmiliki wa fb kwa mkwanja


ila una akili nyingi sana, nimekubali mbinu zako
 
kwakuwa usha rudiana na huyo demu embu sasa ivi mpotezea kujifanya joyce kabla hajakustukia na je demu mwingine ndo uto mgegeda tena
 
Back
Top Bottom