Nahisi mpenzi wangu hajui kusoma

Nahisi mpenzi wangu hajui kusoma

estlyjonathan

Member
Joined
May 26, 2016
Posts
84
Reaction score
122
Habari zenu wana,

Nina mahusiano yapata miezi miwili (2) huyu mpenzi wangu nampenda sana, tatizo nikimtumiaga mesage huwa hajibu, hukimbilia kunipigia simu lakini hilo siyo tatizo kubwa sana kwangu, nilichoshangaa jana tukiwa tunakula kuna rafiki yangu wa kike kanipigia simu nikavunga nikajifanya sitaki kupokea akamaindi.

Baada ya muda simu ikakata akaichukua simu akawa mkali ikabidi nimuachie kufungua, nikamuuliza nani kapiga alishindwa kuisoma lile jina, akaanza kuuliza missed call ilioingia sasa hivi ni ipi, ndo nikamuonyeshea.

Napatwa na wasiwasi sana kuhusu hili na kuhusu elimu yake ameishia kidato cha pili, ila kuandika namba anajua tatizo meseji kujibu pindi mnapo chat hapo ndo tatizo, nifanyaje ili nijue ukweli au anafanya kusudi.

Naombeni ushauri wenu.
 
Hapendagi tu kuandika meseji na kusoma sidhan kama ulimwengu wa leo mtu yupo town asijue kusoma na kujibu msg tena mwanaume, apo ni mtego ww rukaaaaaa
 
Hapendagi tu kuandika meseji na kusoma sidhan kama ulimwengu wa leo mtu yupo town asijue kusoma na kujibu msg tena mwanaume, apo ni mtego ww rukaaaaaa
Wapo....kuna mwanaume me namjua hajui kusoma kabisaaaa....wala hasev namba...ila ukipiga anajua huyu ni nani kwa kuangalia namba za mwisho....na ukituma mesej anakupigia... atazuga hajaiona au alikua bize....
 
Atakuwa kweli hajui kusoma kwa ufasaha hata mimi kuna mtu wangu wa karibu yuko hivyo ilituchukua muda kugundua. Naye alikuwa ana act hivyo
 
Kwa hali ya kawaida unalizungumziaje hili maana limekua ni tatizo kubwa
Wapo....kuna mwanaume me namjua hajui kusoma kabisaaaa....wala hasev namba...ila ukipiga anajua huyu ni nani kwa kuangalia namba za mwisho....na ukituma mesej anakupigia... atazuga hajaiona au alikua bize....
Sina uhakika sana, huyo jamaa anaishi mjini au yupo kijijini?

Mazingira yanaweza kuwa changamoto pia
 
Kuna jamaa mmoja fundi akiitwa karakacha jamaa anajua namba tu kusoma hajui ni mtu mzima namba za simu umuandikie akitaka kukupigia anajua kuzishika cha kushangaza..... Kama ndio huyo usikhofu kubali hali yake
 
Kama unampenda hutojal kuhusu yy kujua kusoma, upendo wa kwl ndo mpango wa town, zingine ni mbwembwe tu we mkamatie tu handsome wako uyo we jichanganye ss et hajui kusoma mara hajibu text zako, ujue mtu asiyejua kusoma ni mzuri maana ni mwoga kutongoza kwingine maana kutongoza kunahusisha text pia, wenzio wanakuchora tu ukilitupa tu tonge wenzio wanalidaka na kubugia
 
Mbali na hilo la mpenzi wako kutokujua kusoma kuna tatizo lingine linalokukwaza?
 
Back
Top Bottom