Nahisi Mpenzi wangu ana HIV/AIDS

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
430
Wana jamvi nina mpenzi wangu mara kwa mara amekuwa akisema ana umwa. Mara nyingi amekuwa akisumbuliwa na kichwa pia maumivu tumboni na maeneo ya mbavu. Kila nikiwambia tukapime anadai eti ni hali ya kawaida huwa inamtokea na kuisha. Napenda kujua yafuatayo

1. Ni dalili zipi za awali kabisa za mtu mwenye HIV/AIDS
2. Nini ushauri wenu katika hali kama hii?
 
Aaaah! WOWOWOOO, kapime kwanza. Ukipata majibu yalete jamvini ili tukushauri vizuri.
 
usiwe na wasiwasi wowowo hizo haziwezo kujitoshereza kusema ana HIV/AIDS cha msingi msihi akapime maana anaweza hata kuwa na pneumonia.
 
Dalili za mwanzo za HIV ni maradhi ya mara kwa mara na kila ukila dawa hauponi. Kinga za mwili zinazidiwa na vijidudu vya maradha hata malaria husumbua. Kupima kuna faida kubwa zaidi madaktari watakuambia. Anza wewe kupima kwani inawezekana umemuambukiza kwani kama umefanyanae ngono zembe (bila condom au kwa haraka haraka na ukasababisha michubuko sirini)
 
Mkuu nenda kapime halafu pia unatakiwa kumshawishi mwenzako.Mbona siku hizi masuala ya maradhi si ya kuficha kabisa. Ngoja ngoja itawaletea madhara.
 
  • Thanks
Reactions: rom
WOWOWO dalili ya ngoma huzijui? Hebu google utazipata, msiwawazie wenzenu mabaya....
 
Last edited by a moderator:
Acha kujitia woga utakufa kabla ya siku zako,nenda kapime wewe na huyo mwenzio,kama anasita kaanze wewe then umshauri na yeye akapime,huna haja ya kuogopa hata kama unao huo sio mwisho wa maisha yenu tena itakuwa umewahi kukiko kusubiri uanze kukugalagaza.
 
"ni hali ya kawaida kuumwa kichwa,mbavu na tumbo"?hivi kuna ugonjwa ambao ni hali ya kawaida? Mpeleke hospitali yawezekana anajijua anachoumwa ndo mana haendi hospitali!
 
Kuumwa sio kwamba una ugonjwa wa ukimwi cha muhimu kwenda kupima ns kupata tiba sahihi. Kuna watu waoga kwenda hospital waweza mshawishi kidogo kidogo hadi kuridhia kwenda
 
ukiogopa ugonjwa utakufa siku si zako............. kapime kwanza wewe achana nae... ukipata majibu utajua hali yake ikoje, maradhi yapo mwengi sana duniani na kila ugonjwa una dawa yake.
 
tatizo watanzania huwaga tunajua kupima ukimwi na malaria tu, tukijitahidi sana ni typhoid, kuna magonjwa mengi sana ndugu yangu ambayo dalili hufanana, ila kikubwa na cha msingi ni kufanya vipimo vikubwa..i once had a urination problem nikafikiri ni kisukari..kwenda kupima magonjwa yote nikakuta ni UTI lakini dalili zoote zilionesha kama kisukari vile, tuache utamaduni wa zamani wa kuhisi mambo na kwenda hospitali kupata tiba sahihi..
 
Wakuu asanteni kwa ushauri wenu. Jana Asubuhi nimeenda Kituo cha AMREF pale Mnazi mmoja nikiwa na mwenzangu. Tulifika mida ya saa 4.30 Asubuhi hivi tukaambiwa tumechelewa kwani huduma hiyo inasuasua sana kutokana na vipimo kuwa vichache hivyo wao siku hizi wanalazimika kupokea watu 25 tu kwa siku. Nilipatwa na mshtuko, kwamba vipimo vya ugonjwa kama huo ambao tumeshautangaza kuwa janga vinakuwa vya kubahatisha kiasi hicho. Muhudumu aliyekuwepo alitushauri tuwahi leo (Alhamisi) kabla ya saa 3.00 Asubuhi.

Pamoja na tatizo la foleni kwenye mji wetu, leo Asubuhi nilikuwa AMREF Mnazimmoja. Nilifika mida ya saa 2.59 Asubuhi lakini nimekumbana na hali kama ya jana. Sijafanikiwa kupima tena.

Najiuliza tena kwa huzuni kubwa, inakuaje huduma kama hii inakua ya kusuasua? Kama hali inakuwa hivyo hapa Dar mikoani inakuaje?

NOTE:
Wasiwasi wangu unakuwa mkubwa kutokana na ukweli kwamba, huyu demu niliyenaye ni wa kwanza kufanya naye ngono zembe na nilikosea sikupima kabla ya kuanza naye..
 
wowowo, kama unajua kanisa la roman catholic pale chang'ombe karibu na kituo cha polisi wanapima, huwa watu si wengi. Hakuna raha kama kujua afya yako ikoje.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom