Nahisi mke wangu anani-cheat, nifanye nini kumkamata?

Nahisi mke wangu anani-cheat, nifanye nini kumkamata?

Hellow, Habari Wana JF. Sorry Mimi sio muandishi mzuri hua nachanganya capital letters katikati,

As normal Jf imekuwa na member bright sana ambao wengine washachomwa mishale mingi sana kwenye maisha ya mahusiano hivyo kuwafanya kuwa watu wenye experience kubwa katika kutatua changamoto yoyote ya kimahusiano inayowahusu kwa kutumia busara zaidi bila shari au hata kujaribu kuwashauri wale wenye uhitaji wa ushauri kutoka kwao ikiwemo mimi pia ambae nahisi bado kabisa ndo kama nachipukia kwenye hii kitu inayoitwa mahusiano ya mapenzi (I'm 21yrs).

Let's go to the point [emoji116]
Naishi na mwanamke huu mwaka wa pili Sasa(pika pakua) jinsi tulivyoanza kuishi nadhani Leo sio siku ya special ya kuelezea hilo, ila katika safari ya miaka hio miwili nimeshakutana na changamoto ya usaliti Kutoka kwake, Mwanzoni nilikuwa nikifuma messages za kunicheat katika cm yake alikuwa ni mtu anaejua kupoteza ushahudi sana, kwa mfano; Kuna siku nilifuma messages zake za WhatsApp akichart na jamaa fulani ambae kiukweli ndo kama alikuwa akimtongoza(it's normal kwa wanawake kutongozwa) ila kilichoniuma katika conversation yao alionekana kukubali Ile appointment ya jamaa(he! jamani hapa si alikuwa anaenda kuliwa kabisa???) kile kitu kilifanya nikapanick sana coz Ukizingatia ndo first time Dah!, Nilijikaza nikarudisha simu nikajikausha kama sijaona chochote aliporudi kufanya manunuzi ya vitu dukani akapika fresh tukaanza kula, Kidume nilijikaza nikawa najitia kula lakini chakula ngumu kumeza wakati huo mwenzangu anabugia matonge Tena na simu yake kama anachat hivi na katabasam kwa mbaliiii nikaona eh! uvumilivu unanishinda nikawaza ngoja nakiamsha hapahapa kama mbwai iwe mbwai.

Mimi;Mary em Simu yako
(akaniangalia kisha akafanya kama anasikitika fulani na kucheka kama dharau hivi Kisha akanipa Simu niliporudi kuzicheki zile messages ambazo ndo kama chanzo changu cha ushahidi wa kunikingia ubavu bwanae! sikuona chochote zilikuwa deleted tayari (Hawa viumbe ni waajabu sana yani wapo very sharp.... Sasa sijui alijuaje, na kumbe ndo maana hakusita kunipa simu yake) Ile kitu ilinikasirisha sana na ikanifanya nione kwamba kumbe mwanamke ninaeishi nae ni hatari hivi, Sikuonesha reaction yoyote nilijifanya tu kama nilitaka simu yake kwa lengo la kucaluculate kitu tu Ila roho haikutulia kabisa na chakula nilishindwa kukila kabisa,


Mara ya pili nilihisi tu kwamba kuna jamaa jirani yangu ambae ni fundi makenika kama vile yupo kwenye root za kumnyemelea mwanamke ambae ninaishi nae kama mke na mume, Nilihisi hivyo kwa kuwa alikuwa ni jamaa fulani kama anajishtukia sana tukionana macho kwa macho basi nikasema ngoja nifuatilie bhana we! kwani nilikosea basi??? Ni kitendo cha kucheki simu ya mwanamke nikaona kwenye call history Kuna namba inaonekana kumpigia sana wife ila haipo saved then ukiangalia kwenye history inaonekana wanaongea muda mrefu sana imagine 6dk-10dk alafu Namba ya wazazi wake naijua na ninayo pia, Ya Ndugu zake karibu wote ninayo na pia sio mwanamke wa kukaa na namba ambayo haipo saved kwenye Simu yake basi nikajiuliza huyu ni Nani anaongea nae kwa muda mrefu hivi? (Kumbuka wife ni mtu tunakutana jioni tu maana kutwa yupo kazini kwake na Mimi nipo kazini kwangu) nikachukua Ile namba nikaisave kwangu then nikaenda kuichungulia whatsapp He! jamani sura ya makenikia si hii hapo asee safari hii sikulaza damu nikakiamsha sana Ila baadae mwanamke alikiri kuwa jamaa ndo alikuwa akimtongoza lakini hakumkubali, Pale nikakosa nguvu ya kumuwajibisha kwa sababu sikuwa na ushahidi kama je, mwanamke alimkubalia??? maana ni kweli wanawake kutongozwa ni normal tu Yule makenika Nakumbuka siku iliyofuata nilipoona nae jicho kwa jicho kiukweli yule jamaa najisi alfahamu kabisa kwamba Mimi Kuna kitu nimegundua baada ya pale nahisi waliambiana nimewaahtukia yule makenika sikuwahi kumuona tena (Aisee Hawa wanawake kuwakamata vizuri hadi akose pa kutokea ni kazi ngumu sana.... hua nawakubaligi sana Wanaume wanaowafumania wake zao na ushahidi wa kutosha Aisee Hawa watu wanakuwaga maginious sana, Ukiona mwanaume kamfumania mwanamke ata akichukua maamuzi mabaya yaheshimu sana maana Hawa viumbe kuwafumania inahitajika akili iliyotulia hasa kwa wale watu wenye kuhitaji ushahidi wa kutosha) Tuachane na Hilo maana Hilo lilipita salama.

Tuje tukio Hili lililopelekea kuandika huu uzi, ni Kitu kama Cha week mbili zilizopita Kutoka Leo wife ameniambia kapanda cheo kidogo kazini kawa supervisor na kutokana na Hilo atakuwa analazimika kuchelewa kutoka kazini nikajibu "Alhamdulillah mke wangu MUNGU anasikia maombi yetu hongera sana) basi saa 3 usiku ndo akaanza kurudi nyumbani, Sio siri inaboa sana lakini no way ili tutimize malengo kila mmoja yabidi achacharike, Sasa jana muda yeye kashalala (Mimi hua nachelewa kulala sana maana napenda kuutumia usiku kupitia maswala ya biashara yangu) sijui kilinisibu nini nikajikuta nimeshika simu yake ambayo ni ndogo nikajikuta nimeenda sehemu ya kuhifadhi messages (inbox) ndipo nikakutana na ujumbe wa jamaa kamsave "Robert" umetumwa neno My love,, picha nitakuwekea hapo chini, Aisee huyu mwanamke hajawahi kunifuma mimi maana Sina tabia za kimalaya mbona aisee ni mimi Kila siku tu ndo naumia??? Basi kukusanya data kamili nikaanza kutafuta muendelezo, Kiukweli jamaa inaonekana ndo kama wameanzaanza, Nikapata kwenye call history nikakuta jamaa ametoka kuwasiliana nae ahsubh na wametumia sec kama 60 na mchana kama dk 2 hivi, nikachukua Ile namba nikaenda kucheki profile ya WhatsApp naona jamaa sio asili ya kitanzania, Anaonekana kama muhindi fulani hivi na pia nikagundua wanafanya kazi kampuni moja na kimuonekano Anaonekana ni boss nilijua Hilo baada ya kuona kitambulisho cha jamaa kipo the same na Cha wife, Sasa kiukweli I'm tired of this shit, Nataka nipate ushahidi wa kutosha kabisa ili siku namwambia it's over iwe inamake sense maana hawachelewi kusema nilimchoka tu, Please ambae anaejua jinsi ya mimi kufanya ili ikiwezekana nimfumanie vizuri hadi achanganyikiwe maana anajionaga ni mtu innocent sana alafu mjuaji sana huyu mwanamke kumbe ana tabia zake mbaya za chinichini, Sikatai mwanamke kutongoza kawaida ila Kukubali je, Mtu humtaki inasave namba yake ya Nini? unaahundwa hata kuiblock basi sawa ishieni kwenye chatting pekee he! call history inaonekana mnaongea Tena sana tu, Au ndo aliempa cheo? Au navyoniambia anachelewa kwaajili ya kazi usikute ndo muda wao wa kuenjoy?

Please kama Kuna mtu wa kunisaidia njia ya kumfunia huyu mwanamke naomba anisaidie tafadhali, Nimeacha na sina wala kushobokea mwanamke mwingine kwaajili yake, Inaniuma sana kwa mwanaume kujinyima kama hivi kwaajili ya pimbi kama huyu Inakuwaga na maumivu eti wazee Bora ningekuwa Malaya.View attachment 1921712
Kama hujajiandaa kumwacha baada ya fumanizi, TAFADHALI sana usipange kumfumania, maana hilo suala litakutesa maisha yako yote yaliyosalia. Ila kama unataka kumfumani ili upate ushahidi wa kumwacha, then go ahead bro. Have a nice day
 
Njoo pm nipe namba yake..akichomoka mitego yangu basi huyo hana shida
Nitakua naku update kila hatua
Ningefanya hivyo lakini sio sawa hapo nitakuwa nimeshiriki kumtafutia sababu, nadhani ni vizuri sababu itoke kwake mwenyewe
 
Mkuu uje nikufundishe mbinu nzuri kabisa!.Kosa lako unaharaka alafu unapanic haraka.Unatakiwa usionyeshe kwanza dalili za kumchunguza wala asikugundue mpaka pale utakapojiridhisha 100% kuwa na ushahidi wa kutosha.Kabla hajadelete message ilitakiwa iwe umepiga picha za kutosha alafu unakausha! Kwa maujanja zaidi nione pm
 
Pole sana mkuu, kwa jinsi ambavyo umeandika inaonesha kabisa unampenda sana huyo bibie na anajua hilo kwa 100% pia inaonekana hana hofu na wewe.

Mapenzi kwa sasa yamebadilika sana, wanawake wengi wanawapenda sana watu ambao ni unpredictable tofauti na wale watu ambao wapo straight katika mapenzi yao.

Ukitaka kukaa na mwanamke kwa sasa unatakiwa kuwa vuguvugu kiasi kwamba mda wowote unaweza kuwa moto na pia unaweza kuwa baridi at any point, hakuna kitu kibaya kama kukosa uwezo wa kuonya au kuwajibisha kwa wakati.

Naona kabisa ww si mtu wa ivo, kama umeona msg lakin umetafuta pumzi kulisema hilo hadi msg ikafutwa, kuna tatizo hapo kwako. Umeona msg hizo usiku lakin umemaliza umerudisha simu then ukageukia upandewwa pili kulala huku una ugulia ndani kwa ndani, kuna tatizo hapo.

Ushauri wangu kwako, mwanamke hupenda mtu mwenye msimamo na maamuzi, USIOGOPE KUACHANA NAE kuanzia sasa, kwanza kabisa kaa nae ongea nae mwambie yale yote ambayo unayajua kuhusu yeye, onesha kama unachukizwa na hayo mambo uliyoyaona pia mwambie ikitokea tena basi tusilaumiane then ishia hapo hapo hautakiwi kuongea sana.

Siku ikijirudia, fanya kitu kwa maana mbili moja ajue kama umechukizwa, mbili uwe tayari kwa lolote. Mwambie ambacho umeiona sio kukisikia na mtandike kofi moja matata sana alafu ondoka kama unaweza yaani unaruhusu ondoka nenda rudi mda umeenda kama ni usiku basi hama chumba kalale hata sebuleni, then uangalie reaction yake,

kama utakuwa umetoka akikutext na kukuomba msamaha basi umeanza kumu win, kama utahama chumba then akakufuata kukuomba msamaha basi ni jambo jema basi ikitokea ivo usionesha kusamehe haraka haraka nenda nae ivo hata kwa siku kadhaa ukiwa Un normal kwake usiwe muongeaji sana wala mchangamfu angalia juhudi zake katika kukurudisha katika hali ya kawaida.

Ukiona juhudi zake kwa siku hizo kadhaa basi una act kurudi hapo yeye ataona kabisa alikukwaza na imemchukua juhudi kukuweka sawa.

Ila upande wa pili, kama utamtandika kibao na kuondoka au kuhama chumba kwa mda huo lakin asikuombe msamaha my friend, jua kabisa hapo huna mtu, jiandae kisaikolojia kabisa na kama ulikuwa unamsikiliza sana punguza hilo hali na anza kuwa bize na mambo yako na kujijali zaidi mwenyewe.

Inaweza saidia kumuweka sawa. Wanawake wengi kwa sasa wanawapenda watu ambao jamii inaona kama wanawanyanyasa kutowajali na huwasumbua sana wale ambao huwapenda sana na kuwajali zaidi.

Inahitaji roho ngumu na akili kubwa kuishi na mwanamke ana akuelewe. Sema kitu kwa mda muafaka, chukia kila ambacho umechukizwa kwa wakati muafaka, mwisho kabisa, jipende zaidi mwenyewe na jithamini zaidi mwenyewe.
 
Don't play dangerous game unless you're willing to loose....
 
Achana na ufala wa kutafuta evidence, piga chini huyo mwanamke. Mahusiano ambayo hayakupi amani ya moyo ni ya kuyaepuka, mwambie unamuacha kwa sababu huna imani nae.
 
At only 21 years old tayari unaanza kuandika magazeti ya kuumizwa?

Yaani you have your entire life ahead of you ujue? Na hapo umeshajichanganya mapema kwa mwanamke amvae atakusumbua sana huko baadae na utazidi kujichanganya usipochukua uamuzi mgumu.

Why nasema hivi I am at that point in life where you realise just how much time you spent on alot of nonsense.

Pole and good luck. You are going to need it especially when you love them too deep.
21years bado ni mdogo sana kwenye ndoa
 
Mkuu uje nikufundishe mbinu nzuri kabisa!.Kosa lako unaharaka alafu unapanic haraka.Unatakiwa usionyeshe kwanza dalili za kumchunguza wala asikugundue mpaka pale utakapojiridhisha 100% kuwa na ushahidi wa kutosha.Kabla hajadelete message ilitakiwa iwe umepiga picha za kutosha alafu unakausha! Kwa maujanja zaidi nione pm
nakuja
 
Mtoa mada muulize mkeo anakosa nini mpaka anafanya hivyo
 
Mambo kama hayo mara nyingi lazima yatokee katika mahusiano yoyote ya ndoa ama ya namna nyingine.

Cha kufanya ndugu mleta mada acha kutengeneza mazingira ya kufumaniana ili yenye kupitia yapite.
Funikika kombe mwana haramu apite.
 
Pole sana mkuu, kwa jinsi ambavyo umeandika inaonesha kabisa unampenda sana huyo bibie na anajua hilo kwa 100% pia inaonekana hana hofu na wewe. Mapenzi kwa sasa yamebadilika sana, wanawake wengi wanawapenda sana watu ambao ni unpredictable tofauti na wale watu ambao wapo straight katika mapenzi yao. Ukitaka kukaa na mwanamke kwa sasa unatakiwa kuwa vuguvugu kiasi kwamba mda wowote unaweza kuwa moto na pia unaweza kuwa baridi at any point, hakuna kitu kibaya kama kukosa uwezo wa kuonya au kuwajibisha kwa wakati. Naona kabisa ww si mtu wa ivo, kama umeona msg lakin umetafuta pumzi kulisema hilo hadi msg ikafutwa, kuna tatizo hapo kwako. Umeona msg hizo usiku lakin umemaliza umerudisha simu then ukageukia upandewwa pili kulala huku una ugulia ndani kwa ndani, kuna tatizo hapo. Ushauri wangu kwako, mwanamke hupenda mtu mwenye msimamo na maamuzi, USIOGOPE KUACHANA NAE kuanzia sasa, kwanza kabisa kaa nae ongea nae mwambie yale yote ambayo unayajua kuhusu yeye, onesha kama unachukizwa na hayo mambo uliyoyaona pia mwambie ikitokea tena basi tusilaumiane then ishia hapo hapo hautakiwi kuongea sana. Siku ikijirudia, fanya kitu kwa maana mbili moja ajue kama umechukizwa, mbili uwe tayari kwa lolote. Mwambie ambacho umeiona sio kukisikia na mtandike kofi moja matata sana alafu ondoka kama unaweza yaani unaruhusu ondoka nenda rudi mda umeenda kama ni usiku basi hama chumba kalale hata sebuleni, then uangalie reaction yake, kama utakuwa umetoka akikutext na kukuomba msamaha basi umeanza kumu win, kama utahama chumba then akakufuata kukuomba msamaha basi ni jambo jema basi ikitokea ivo usionesha kusamehe haraka haraka nenda nae ivo hata kwa siku kadhaa ukiwa Un normal kwake usiwe muongeaji sana wala mchangamfu angalia juhudi zake katika kukurudisha katika hali ya kawaida. Ukiona juhudi zake kwa siku hizo kadhaa basi una act kurudi hapo yeye ataona kabisa alikukwaza na imemchukua juhudi kukuweka sawa. Ila upande wa pili, kama utamtandika kibao na kuondoka au kuhama chumba kwa mda huo lakin asikuombe msamaha my friend, jua kabisa hapo huna mtu, jiandae kisaikolojia kabisa na kama ulikuwa unamsikiliza sana punguza hilo hali na anza kuwa bize na mambo yako na kujijali zaidi mwenyewe. Inaweza saidia kumuweka sawa. Wanawake wengi kwa sasa wanawapenda watu ambao jamii inaona kama wanawanyanyasa kutowajali na huwasumbua sana wale ambao huwapenda sana na kuwajali zaidi. Inahitaji roho ngumu na akili kubwa kuishi na mwanamke ana akuelewe. Sema kitu kwa mda muafaka, chukia kila ambacho umechukizwa kwa wakati muafaka, mwisho kabisa, jipende zaidi mwenyewe na jithamini zaidi mwenyewe.
ahsante sana kwa point hizi na kunipa muda wakowingi kuandika, nakushukuru sana
 
Achana na ufala wa kutafuta evidence, piga chini huyo mwanamke. Mahusiano ambayo hayakupi amani ya moyo ni ya kuyaepuka, mwambie unamuacha kwa sababu huna imani nae.
Kabisa
 
Mtoa mada muulize mkeo anakosa nini mpaka anafanya hivyo
hapo majibu yanaweza Kuwa hela za kumpa, na Mimi Sina za kukidhi mahitaji yake yote Cha muhimu anakula vizuri tu.
 
Mambo kama hayo mara nyingi lazima yatokee katika mahusiano yoyote ya ndoa ama ya namna nyingine.

Cha kufanya ndugu mleta mada acha kutengeneza mazingira ya kufumaniana ili yenye kupitia yapite.
Funikika kombe mwana haramu apite.
Kwahio nivumilie?
 
Hellow, Habari Wana JF. Sorry Mimi sio muandishi mzuri hua nachanganya capital letters katikati,

As normal Jf imekuwa na member bright sana ambao wengine washachomwa mishale mingi sana kwenye maisha ya mahusiano hivyo kuwafanya kuwa watu wenye experience kubwa katika kutatua changamoto yoyote ya kimahusiano inayowahusu kwa kutumia busara zaidi bila shari au hata kujaribu kuwashauri wale wenye uhitaji wa ushauri kutoka kwao ikiwemo mimi pia ambae nahisi bado kabisa ndo kama nachipukia kwenye hii kitu inayoitwa mahusiano ya mapenzi (I'm 21yrs).

Let's go to the point [emoji116]
Naishi na mwanamke huu mwaka wa pili Sasa(pika pakua) jinsi tulivyoanza kuishi nadhani Leo sio siku ya special ya kuelezea hilo, ila katika safari ya miaka hio miwili nimeshakutana na changamoto ya usaliti Kutoka kwake, Mwanzoni nilikuwa nikifuma messages za kunicheat katika cm yake alikuwa ni mtu anaejua kupoteza ushahudi sana, kwa mfano; Kuna siku nilifuma messages zake za WhatsApp akichart na jamaa fulani ambae kiukweli ndo kama alikuwa akimtongoza(it's normal kwa wanawake kutongozwa) ila kilichoniuma katika conversation yao alionekana kukubali Ile appointment ya jamaa(he! jamani hapa si alikuwa anaenda kuliwa kabisa???) kile kitu kilifanya nikapanick sana coz Ukizingatia ndo first time Dah!

Nilijikaza nikarudisha simu nikajikausha kama sijaona chochote aliporudi kufanya manunuzi ya vitu dukani akapika fresh tukaanza kula, Kidume nilijikaza nikawa najitia kula lakini chakula ngumu kumeza wakati huo mwenzangu anabugia matonge Tena na simu yake kama anachat hivi na katabasam kwa mbaliiii nikaona eh! uvumilivu unanishinda nikawaza ngoja nakiamsha hapahapa kama mbwai iwe mbwai.

Mimi;Mary em Simu yako
(akaniangalia kisha akafanya kama anasikitika fulani na kucheka kama dharau hivi Kisha akanipa Simu niliporudi kuzicheki zile messages ambazo ndo kama chanzo changu cha ushahidi wa kunikingia ubavu bwanae! sikuona chochote zilikuwa deleted tayari (Hawa viumbe ni waajabu sana yani wapo very sharp.... Sasa sijui alijuaje, na kumbe ndo maana hakusita kunipa simu yake) Ile kitu ilinikasirisha sana na ikanifanya nione kwamba kumbe mwanamke ninaeishi nae ni hatari hivi, Sikuonesha reaction yoyote nilijifanya tu kama nilitaka simu yake kwa lengo la kucaluculate kitu tu Ila roho haikutulia kabisa na chakula nilishindwa kukila kabisa,


Mara ya pili nilihisi tu kwamba kuna jamaa jirani yangu ambae ni fundi makenika kama vile yupo kwenye root za kumnyemelea mwanamke ambae ninaishi nae kama mke na mume, Nilihisi hivyo kwa kuwa alikuwa ni jamaa fulani kama anajishtukia sana tukionana macho kwa macho basi nikasema ngoja nifuatilie bhana we! kwani nilikosea basi?

Ni kitendo cha kucheki simu ya mwanamke nikaona kwenye call history Kuna namba inaonekana kumpigia sana wife ila haipo saved then ukiangalia kwenye history inaonekana wanaongea muda mrefu sana imagine 6dk-10dk alafu Namba ya wazazi wake naijua na ninayo pia, Ya Ndugu zake karibu wote ninayo na pia sio mwanamke wa kukaa na namba ambayo haipo saved kwenye Simu yake basi nikajiuliza huyu ni Nani anaongea nae kwa muda mrefu hivi? (Kumbuka wife ni mtu tunakutana jioni tu maana kutwa yupo kazini kwake na Mimi nipo kazini kwangu) nikachukua Ile namba nikaisave kwangu then nikaenda kuichungulia whatsapp He! jamani sura ya makenikia si hii hapo asee safari hii sikulaza damu nikakiamsha sana Ila baadae mwanamke alikiri kuwa jamaa ndo alikuwa akimtongoza lakini hakumkubali,

Pale nikakosa nguvu ya kumuwajibisha kwa sababu sikuwa na ushahidi kama je, mwanamke alimkubalia??? maana ni kweli wanawake kutongozwa ni normal tu Yule makenika Nakumbuka siku iliyofuata nilipoona nae jicho kwa jicho kiukweli yule jamaa najisi alfahamu kabisa kwamba Mimi Kuna kitu nimegundua baada ya pale nahisi waliambiana nimewaahtukia yule makenika sikuwahi kumuona tena (Aisee Hawa wanawake kuwakamata vizuri hadi akose pa kutokea ni kazi ngumu sana. hua nawakubaligi sana Wanaume wanaowafumania wake zao na ushahidi wa kutosha Aisee Hawa watu wanakuwaga maginious sana, Ukiona mwanaume kamfumania mwanamke ata akichukua maamuzi mabaya yaheshimu sana maana Hawa viumbe kuwafumania inahitajika akili iliyotulia hasa kwa wale watu wenye kuhitaji ushahidi wa kutosha) Tuachane na Hilo maana Hilo lilipita salama.

Tuje tukio Hili lililopelekea kuandika huu uzi, ni Kitu kama Cha week mbili zilizopita Kutoka Leo wife ameniambia kapanda cheo kidogo kazini kawa supervisor na kutokana na Hilo atakuwa analazimika kuchelewa kutoka kazini nikajibu "Alhamdulillah mke wangu MUNGU anasikia maombi yetu hongera sana) basi saa 3 usiku ndo akaanza kurudi nyumbani, Sio siri inaboa sana lakini no way ili tutimize malengo kila mmoja yabidi achacharike,

Sasa jana muda yeye kashalala (Mimi hua nachelewa kulala sana maana napenda kuutumia usiku kupitia maswala ya biashara yangu) sijui kilinisibu nini nikajikuta nimeshika simu yake ambayo ni ndogo nikajikuta nimeenda sehemu ya kuhifadhi messages (inbox) ndipo nikakutana na ujumbe wa jamaa kamsave "Robert" umetumwa neno My love,, picha nitakuwekea hapo chini, Aisee huyu mwanamke hajawahi kunifuma mimi maana Sina tabia za kimalaya mbona aisee ni mimi Kila siku tu ndo naumia??? Basi kukusanya data kamili nikaanza kutafuta muendelezo, Kiukweli jamaa inaonekana ndo kama wameanzaanza

Nikapata kwenye call history nikakuta jamaa ametoka kuwasiliana nae ahsubh na wametumia sec kama 60 na mchana kama dk 2 hivi, nikachukua Ile namba nikaenda kucheki profile ya WhatsApp naona jamaa sio asili ya kitanzania, Anaonekana kama muhindi fulani hivi na pia nikagundua wanafanya kazi kampuni moja na kimuonekano Anaonekana ni boss nilijua Hilo baada ya kuona kitambulisho cha jamaa kipo the same na Cha wife, Sasa kiukweli I'm tired of this shit,

Nataka nipate ushahidi wa kutosha kabisa ili siku namwambia it's over iwe inamake sense maana hawachelewi kusema nilimchoka tu, Please ambae anaejua jinsi ya mimi kufanya ili ikiwezekana nimfumanie vizuri hadi achanganyikiwe maana anajionaga ni mtu innocent sana alafu mjuaji sana huyu mwanamke kumbe ana tabia zake mbaya za chinichini, Sikatai mwanamke kutongoza kawaida ila Kukubali je, Mtu humtaki inasave namba yake ya Nini? unaahundwa hata kuiblock basi sawa ishieni kwenye chatting pekee he! call history inaonekana mnaongea Tena sana tu, Au ndo aliempa cheo? Au navyoniambia anachelewa kwaajili ya kazi usikute ndo muda wao wa kuenjoy?

Please kama Kuna mtu wa kunisaidia njia ya kumfunia huyu mwanamke naomba anisaidie tafadhali, Nimeacha na sina wala kushobokea mwanamke mwingine kwaajili yake, Inaniuma sana kwa mwanaume kujinyima kama hivi kwaajili ya pimbi kama huyu Inakuwaga na maumivu eti wazee Bora ningekuwa Malaya.

View attachment 1921712

Aisee Mtoto mdogo hivyo una mke?!
Maana mdogo wa mwisho kwangu ni mkubwa kwako na aisee huwa namwambia usikubali mwanamke akuzingue katika umri huo unatakiwa kufurahia maisha yako na kupambana kutimiza ndoto zako
Sijui hata nikushauri nini lakini pole
 
Ngoja kwanza..umesema una miaka 21 na umeishi nae miaka miwili means ulianza kuishi nae ukiwa na miaka 19 je yeye ana umri gani...amekuzidi,na je wewe ni tegemezi kwake au alikusupport mtaji? ukijibu haya ndio tapata pazuri pa kuanzia kukushauri..pole sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom