Nahisi mfanyakazi mwenzangu ana njama za kuniroga, naombeni ushauri wenu

muafi

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
2,115
4,802
Kuna jamaa mmoja ni mfanyakazi mwenzangu japo hatufanyii kazi sehemu moja na hatukua na mazoea sana japo tulifahamiana maana mara kwa mara tumekua tukikutana kwenye vikao vya pamoja ambavyo hutokea mara chache tu kwa mwaka,

Sasa ilikua Ijumaa iliyopita yule bwana tulikutana tena hapa ilikuwa ni kwenye kikao tena,

Sasa mida ile tunaondoka tukapanda gari moja kurudi makwetu nikajikuta napiga nae stori mbili tatu hadi nikamkaribisha nyumbani kwangu apaone,

Na yeye hakusita kweli akaja kwangu sasa ajabu alipofika ndani akakaa kidogo akatoka nje akaniita nilipotoka nje akaniambia hapa nyumbani kwako ni pachafu sana!

Mimi nikashangaa nilikuwa sijamuelewa nikamwambia labda waifu leo hakufanya usafi, jamaa akaniambia hamaanishi hivyo ye anamaanisha nyumbani kwangu pametegwa madawa ya kichawi duh nilishangaa kusikia hivyo,

Jamaa akaniambia ila nikihitaji msaada atanisaidia tukarudi ndani, tumekaa tena kama dakika kumi akasema tena humu ndani ni pazito hadi jasho limenitoka ni pazito sana hapa inabidi pazindikwe,

Duh story zikaendelea baada ya mda akaniambia nimuoneshe chooni anataka kwenda nikamielekeza alipotoka chooni akarudi ananiambia chooni kwako ni pachafu sana kuna vitu umetegewa!

Kwakweli mi sikumuelewa but ile namsindikiza akaniambia eti nataka kunisaidia anipe dawa ya kuoga nyingine ya kuweka ndan, nyingine anichanje halafu anipe hirizi nifunge ndani,

Duh kwakweli mimi nikamkubalia kinafiki lakini moyo wangu ulisita maana mambo ya kufuga hirizi mi kwakweli hapana sijawai kuyafanya tangu kuzaliwa kwangu,
Halafu then ninunue wembe kabisa jamaa aje anichanje chale? Nikaona hii hapana

Sasa jamaa tangu siku hiyo ananisumbua sana kila mda ananitafuta eti anataka aje kunitengenezea madude,
Amenikomalia sana aisee na hata leo jioni kanitafuta anataka aje nikamwambia nimetoka sipo!

Sasa mi najiuliza huyu anataka kunisaidia au kunipandikizia vitu vyake?

Ushauri wenu jamani huyu mtu nimfanyeje au nimpe mabango asinirudie tena?


NB: huyu jamaa alihamishwa kwenye kituo chake cha kwanza cha kazi maana alikua hapatani na wafanyakazi wenzake walikua wakimshutumu kuwa ni mchawi! Sasa nikilinganganisha tuhuma zake za awali nahisi kabisa jamaa anataka kunipandikizia vitu vyake
 
Achana nae huyo kenge tu "kuna bibi mmoja maika ya nyuma alikuja kwa bi mkubwa akamwambia kauli kama hizo, sasa bi mkubwa akasoma mchezo akamwambia usiniletee mambo yako hapa, baada ya wiki mbili yule mama mganga alikufa, tukahisi yalikuwa yanamshinda akatafuta sehemu ayaweke yatuangamize

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana nae huyo kenge tu "kuna bibi mmoja maika ya nyuma alikuja kwa bi mkubwa akamwambia kauli kama hizo, sasa bi mkubwa akasoma mchezo akamwambia usiniletee mambo yako hapa, baada ya wiki mbili yule mama mganga alikufa, tukahisi yalikuwa yanamshinda akatafuta sehemu ayaweke yatuangamize

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwakweli hata mi nilishtuka mtu ananikomalia anifungie hirizi ndani, tangu kuzaliwa kwangu hirizi nazisikiaga tu leo hii mtu aniwekee kwangu?
 
Mwambie umeshaita mchungaji/shekh amefanya maombia na mambo saaa hivi yapo sawa... Kisha usimlete tena kwako maana atakuambia bado madude hayajatola vizuri inabidi yeye afanye tena hiyo kazi...
Yani mpaka sasa nafanya kazi ya kumkwepa ila jamaa kila mda ananipigia simu aje!
Nahisi kifuatacho ataanza ziara za kushtukiza kwangu
 
Kuna jamaa alimwambia mshikaji wangu kuwa kama mke wake hatulii ampeleke Msata kwa mganga amtulize, juzi kati nimeambiwa na jamaa kuwa yule mshikaji aliyetaka anipeleke kwa mganga naye mkewe kamkimbia

Haya mambo huwa ya hovyo sana

USSR
 
Yani mpaka sasa nafanya kazi ya kumkwepa ila jamaa kila mda ananipigia simu aje!
Nahisi kifuatacho ataanza ziara za kushtukiza kwangu
Acha kumchekea mzingue kwa ukali sana naona kama unampa ushirikiano kiaina hivi ,ningekuwq mimi siku ya kwanza urafiki ungeisha na kumblock mazima

Huwa nikikwama naenda kanisani tu na mambo yangu yanakwenda ,nawashukuru wazazi wangu kunifunza hivi


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana na laana hizo na utajuta maisha yako yote
Jua unataka kuanza kukaribisha mikosi
We si umkatalie kwani unaogopa nini?
 
Back
Top Bottom