Nahisi dada wa kazi ana hisia na mume wangu

"Dada ananiambia mama acha kuandaa chakula nitaandaa mie natamani baba ale chakula changu" .......Wanaume ni dhaifu sana, usipochukua hatua ndoa inaenda kuingia kwenye misukosuko mikubwa muda siyo mrefu,unaenda kupinduliwa.Mfukuze(Kuna siku utaukumbuka ushauri huu usipochukua hatua)
Hii dhana ya kupinduliwa huwa siielewagi.
Ina mana huyu binti ana utaalam extra ambao mke hana au?!
 
Ningekua mm nafanya mawili namrudisha kwao natafuta mwengne mbona wamejeaa watu wa kazi

Au natafuta sehem ambayo nitampeleka mtoto wangu kulelewa mchana nikitoka kama nina mda wa kutosha kumpeleka na kumchukua sitafuti dada mwengne nitafanya kazi zangu zote nikirudi

Siipendi kudharauliwa na mtu niliempa heshima
Sipendi kuona mtu anajaribu kuniibia mume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akimrudisha kwao au kumfukuza ndio watakuja wale wanaharakati wa kutetea mabinti wa kazi kwa kisingizio kuwa wanaonewa.
Wakat unaona kabisaa haus girl anavyoitingisha ndoa yako aharibu mustakabal9i wa maisha yenu.

Hili nilishalikataa.Nitafukuza mahaus girl kila siku
Kwani wamesaini mkataba wa miaka mingapi??? Samahani kwa kweli wamchukue wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni na majukumu nyote...

Baada ya kufanya uchunguzi wangu kwa takribani mwezi sasa nyumbani kuhusu dada anayenisaidia kazi za nyumbani nimehisi kitu tofauti ambacho mpaka sasa sijui nianzie wapi kukitatua.

Nakiri mimi si muongeaji sana, asili yangu ni ukimya huwa kuna muda hata nahisi ndio mapungufu yangu pengine Mungu aliyonipatia.

Kifupi nimeanza kuishi na Dada wa kazi baada ya mwanangu kutimiza miezi sita kwa sababu niliihitajika kuendelea na majukumu yangu kibiashara na Niko nae nyumbani karibu mwaka na miezi miwili sasa. Nimeanza kuhisi pengine dada wangu huyu ana hisia na mume wangu kutokana na matendo na nyendo zake.

Katika mizunguko yangu siku zote huwa najitahidi muda wa jioni kuwahi ili kuandaa chakula cha jioni. Siku moja nimerudi naandaa chakula Mara dada ananiambia "mama acha kuandaa chakula nitaandaa mie natamani baba ale chakula changu". Kiukweli sentesi ile ilinishitua ila niliona ninyamaze nifanye kama sikumsikia.

Siku iliyofuata Mr wangu aliniambia nimuandalie mboga fulani chukuchuku. Kama kawaida niliwahi nikaandaa na chakula kingine nikaanda pia. Tuna kawaida ya kula chakula pamoja ila wakati tunakula Dada alichukua mboga kidogo niliyoandaa kwa ajili ya Mr ila baada ya kula kidogo aliinuka na kuanza kunawa huku anasema "mboga yenyewe chukuchuku mbaya bora ningeipika mie". Kiukweli nilibaki kumuangalia tu hata Mr ile hali aliishangaa alituacha pale akaenda kukaa kwenye TV.

Mr alianza kunilaumu kwanini hii tabia ya huyu kuongea maneno kama yale naiendekeza na imeanza lini? Akaongeza ni bora angesemea pembeni sio mbele yake.

Binafsi nilijisikia vibaya ila sikutaka kuonyesha action yoyote. Katika kipindi cha karibuni pia amebadilika zaidi, ninaweza kumuelekeza kitu akijibu kwa kukata tu kuwa anajua. Kuna muda mavazi yake yamekuwa ya kutatiza na ukijaribu kumuelekeza abadilishe kutokana na vazi lile kutokaa kiheshima anajibu amenunua yeye kwa pesa yake tena anajibu huku anaondoka.

Nakiri pengine vile nimempa sana Uhuru pale nyumbani sipendi na sikutaka ajihisi yeye kama mfanyakazi hapa nyumbani basi anajisahau.

Kuna muda nikirudi anaweza asiongee na mimi lakini akifika Mr hilo cheko lake hali inabadilika kuna wakati hata anaporudi Mr asiniongeleshe sana mimi ila kwa mume wangu ataongea nae mpaka basi. Kuna siku Mr aliniuliza kuwa mbona huyu Dada amezidisha mazoea na yeye hasa mimi nikiwa nyumbani. Sikutaka kumwambia chochote nilimjibu tu ni kawaida.

Nimefupisha tu hapa ila kuna mambo mengi sana yananitatiza juu ya huyu Dada. Nafikiria kumuondoa nimrudishe nyumbani ila huruma sababu kwao wanamtegemea. Nimejaribu kumuelewesha bila ya yeye kujisikia vibaya juu ya tabia yake lakini naona habadiliki.

Natamani kumuweka wazi Mr juu ya hii hali ila nawaza naanzaje ili Mr asinielewe tofauti nafikiria ile hali pengine asije kusema ni wivu tu Ila si hivi.

Kiukweli niko njiapanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Endelea kumvumilia tu......kwahiyo tabia yake nakuhakikishia akifanikiwa kumvulia tu pichu mume wako anaweza kukufukuza kwenye mji wako!
 
Huruma huzaa dhambi, mweleze mambo yote ambayo wewe binafsi hupendi kutoka kwake, mpe muda wa kubadilika na umweleze hadi muda huo asipobadilika utamrudisha.
Na ufanye hivyo kama unaona atakuwa amekudharau, hiyo itampa funzi kwa wakati mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app

Napinga hoja mm kama mshauri napendekeza amrudishe KWAO wadada wapo wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyuu mumewe anamlaaa huyo dada wa kazi ndo maana anapata jeuri iyooo na mzee anajikaushaa kama hajui kitu..! Jamaa hana nguvu ya kumzingua house girl tatizooooo kubwa sanaa ilii..

JAMAA ANAMLAAA beki 3 ila anazuga tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilitaka kusema hii kitu, jamaa ananla huyo Dada na ndio maana Dada ana jeuri, jamaa anachokifanya ni kucheza na akili ya mkewe ionekane kama hafurahii tabia ya Dada lkn jamaa na Dada lao moja.
Na usikute jamaa lilishamwambia Dada napenda chakula unachopika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huruma itakuponza! Mrudishe binti kwao, jukumu la kuilea familia yao hujampatia wewe. Aliempatia atajua anaileaje!

Unataka kuniambia kabla ya kumpa kibarua huyo Binti, nyumbani kwao walikuwa hawaishi?

Kikubwa ni pumzi tu, hayo ya familia kumtegemea atajua aliemuumba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni na majukumu nyote...

Baada ya kufanya uchunguzi wangu kwa takribani mwezi sasa nyumbani kuhusu dada anayenisaidia kazi za nyumbani nimehisi kitu tofauti ambacho mpaka sasa sijui nianzie wapi kukitatua.

Nakiri mimi si muongeaji sana, asili yangu ni ukimya huwa kuna muda hata nahisi ndio mapungufu yangu pengine Mungu aliyonipatia.

Kifupi nimeanza kuishi na Dada wa kazi baada ya mwanangu kutimiza miezi sita kwa sababu niliihitajika kuendelea na majukumu yangu kibiashara na Niko nae nyumbani karibu mwaka na miezi miwili sasa. Nimeanza kuhisi pengine dada wangu huyu ana hisia na mume wangu kutokana na matendo na nyendo zake.

Katika mizunguko yangu siku zote huwa najitahidi muda wa jioni kuwahi ili kuandaa chakula cha jioni. Siku moja nimerudi naandaa chakula Mara dada ananiambia "mama acha kuandaa chakula nitaandaa mie natamani baba ale chakula changu". Kiukweli sentesi ile ilinishitua ila niliona ninyamaze nifanye kama sikumsikia.

Siku iliyofuata Mr wangu aliniambia nimuandalie mboga fulani chukuchuku. Kama kawaida niliwahi nikaandaa na chakula kingine nikaanda pia. Tuna kawaida ya kula chakula pamoja ila wakati tunakula Dada alichukua mboga kidogo niliyoandaa kwa ajili ya Mr ila baada ya kula kidogo aliinuka na kuanza kunawa huku anasema "mboga yenyewe chukuchuku mbaya bora ningeipika mie". Kiukweli nilibaki kumuangalia tu hata Mr ile hali aliishangaa alituacha pale akaenda kukaa kwenye TV.

Mr alianza kunilaumu kwanini hii tabia ya huyu kuongea maneno kama yale naiendekeza na imeanza lini? Akaongeza ni bora angesemea pembeni sio mbele yake.

Binafsi nilijisikia vibaya ila sikutaka kuonyesha action yoyote. Katika kipindi cha karibuni pia amebadilika zaidi, ninaweza kumuelekeza kitu akijibu kwa kukata tu kuwa anajua. Kuna muda mavazi yake yamekuwa ya kutatiza na ukijaribu kumuelekeza abadilishe kutokana na vazi lile kutokaa kiheshima anajibu amenunua yeye kwa pesa yake tena anajibu huku anaondoka.

Nakiri pengine vile nimempa sana Uhuru pale nyumbani sipendi na sikutaka ajihisi yeye kama mfanyakazi hapa nyumbani basi anajisahau.

Kuna muda nikirudi anaweza asiongee na mimi lakini akifika Mr hilo cheko lake hali inabadilika kuna wakati hata anaporudi Mr asiniongeleshe sana mimi ila kwa mume wangu ataongea nae mpaka basi. Kuna siku Mr aliniuliza kuwa mbona huyu Dada amezidisha mazoea na yeye hasa mimi nikiwa nyumbani. Sikutaka kumwambia chochote nilimjibu tu ni kawaida.

Nimefupisha tu hapa ila kuna mambo mengi sana yananitatiza juu ya huyu Dada. Nafikiria kumuondoa nimrudishe nyumbani ila huruma sababu kwao wanamtegemea. Nimejaribu kumuelewesha bila ya yeye kujisikia vibaya juu ya tabia yake lakini naona habadiliki.

Natamani kumuweka wazi Mr juu ya hii hali ila nawaza naanzaje ili Mr asinielewe tofauti nafikiria ile hali pengine asije kusema ni wivu tu Ila si hivi.

Kiukweli niko njiapanda.

Sent using Jamii Forums mobile app

MAMBO KAMA HAYA NI VIZURI SANA KUWASHIRIKISHA MODS ILI KUPATA BUSARA ZAO.

AU MODS MNASEMAJE?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom