Nahisi dada wa kazi ana hisia na mume wangu

mwanauhime

New Member
Mar 3, 2020
4
54
Poleni na majukumu nyote...

Baada ya kufanya uchunguzi wangu kwa takribani mwezi sasa nyumbani kuhusu dada anayenisaidia kazi za nyumbani nimehisi kitu tofauti ambacho mpaka sasa sijui nianzie wapi kukitatua.

Nakiri mimi si muongeaji sana, asili yangu ni ukimya huwa kuna muda hata nahisi ndio mapungufu yangu pengine Mungu aliyonipatia.

Kifupi nimeanza kuishi na Dada wa kazi baada ya mwanangu kutimiza miezi sita kwa sababu niliihitajika kuendelea na majukumu yangu kibiashara na Niko nae nyumbani karibu mwaka na miezi miwili sasa. Nimeanza kuhisi pengine dada wangu huyu ana hisia na mume wangu kutokana na matendo na nyendo zake.

Katika mizunguko yangu siku zote huwa najitahidi muda wa jioni kuwahi ili kuandaa chakula cha jioni. Siku moja nimerudi naandaa chakula Mara dada ananiambia "mama acha kuandaa chakula nitaandaa mie natamani baba ale chakula changu". Kiukweli sentesi ile ilinishitua ila niliona ninyamaze nifanye kama sikumsikia.

Siku iliyofuata Mr wangu aliniambia nimuandalie mboga fulani chukuchuku. Kama kawaida niliwahi nikaandaa na chakula kingine nikaanda pia. Tuna kawaida ya kula chakula pamoja ila wakati tunakula Dada alichukua mboga kidogo niliyoandaa kwa ajili ya Mr ila baada ya kula kidogo aliinuka na kuanza kunawa huku anasema "mboga yenyewe chukuchuku mbaya bora ningeipika mie". Kiukweli nilibaki kumuangalia tu hata Mr ile hali aliishangaa alituacha pale akaenda kukaa kwenye TV.

Mr alianza kunilaumu kwanini hii tabia ya huyu kuongea maneno kama yale naiendekeza na imeanza lini? Akaongeza ni bora angesemea pembeni sio mbele yake.

Binafsi nilijisikia vibaya ila sikutaka kuonyesha action yoyote. Katika kipindi cha karibuni pia amebadilika zaidi, ninaweza kumuelekeza kitu akijibu kwa kukata tu kuwa anajua. Kuna muda mavazi yake yamekuwa ya kutatiza na ukijaribu kumuelekeza abadilishe kutokana na vazi lile kutokaa kiheshima anajibu amenunua yeye kwa pesa yake tena anajibu huku anaondoka.

Nakiri pengine vile nimempa sana Uhuru pale nyumbani sipendi na sikutaka ajihisi yeye kama mfanyakazi hapa nyumbani basi anajisahau.

Kuna muda nikirudi anaweza asiongee na mimi lakini akifika Mr hilo cheko lake hali inabadilika kuna wakati hata anaporudi Mr asiniongeleshe sana mimi ila kwa mume wangu ataongea nae mpaka basi. Kuna siku Mr aliniuliza kuwa mbona huyu Dada amezidisha mazoea na yeye hasa mimi nikiwa nyumbani. Sikutaka kumwambia chochote nilimjibu tu ni kawaida.

Nimefupisha tu hapa ila kuna mambo mengi sana yananitatiza juu ya huyu Dada. Nafikiria kumuondoa nimrudishe nyumbani ila huruma sababu kwao wanamtegemea. Nimejaribu kumuelewesha bila ya yeye kujisikia vibaya juu ya tabia yake lakini naona habadiliki.

Natamani kumuweka wazi Mr juu ya hii hali ila nawaza naanzaje ili Mr asinielewe tofauti nafikiria ile hali pengine asije kusema ni wivu tu Ila si hivi.

Kiukweli niko njiapanda.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Dada ananiambia mama acha kuandaa chakula nitaandaa mie natamani baba ale chakula changu" .......Wanaume ni dhaifu sana, usipochukua hatua ndoa inaenda kuingia kwenye misukosuko mikubwa muda siyo mrefu,unaenda kupinduliwa.Mfukuze(Kuna siku utaukumbuka ushauri huu usipochukua hatua)
 
Mawasiliano ndani ya ndoa ni kitu muhimu sana. Inaonekana ndoa yenu hamna mawasiliano mazuri. Inashindikana vipi kuongea na mme wako jambo kama hilo tena nae alishakuelezea kuwa huyo dada anaonyesha mazoea kwake sana lakini wewe unamfichia unayoyahisi moyoni. Humu tutashauri sana tu lakini lakurekebisha ni wewe kuongea na mme wako mfikie makubaliano ya pamoja kama kumfukuza au mme wako amuonye

Nyumba haiwezi kuyumbishwa na house girl
 
Binafsi naona hayo mazingira unayatengeneza wewe mwenyewe. Mwite mkalishe chini mkumbushe hali ya nyumbani kwao na jinsi wanavyomtegemea then shusha sheria zako ukiwa macho makavu. Mwambie in plain ukienenda tofauti na haya nikwambiayo sasa nitakurudisha nyumbani, mruhusu akaendelee na kazi.
Angalia kama hata badirika
N.b Ni vyema ukimshirikisha mumeo nae umpime mawazo yake, usikute ushaanza kuzungukwa kitambo bila wewe kujijua
 
Pole Aisee
It's true Sisi tusio weza kuzungumza Kun mda yanakukuta unajiuliza Au huu ni unyonge Wangu ?

Anywayzz, Hapo ni bora Mume wako anakuonesha Ushirikiano laiti Kama angekua anavunga Maswali yangekua Mengi kwako

Ni vizuri wadada wa kazi Wawe vibinti vidogo vidogo, Huy anaonekana Mkubwa na anayajua Vizuri
Wewe and Mumeo ndio wenye Maamuzi
Mtimueni
 
Pole sana.
Nashindwa kuelewa kitu fulani hapa. Umesema Mr. wako alishawahi kukuuliza kuhusu tabia ya huyo mfanyakazi, wewe ukakaa kimya na kuna wakati ulimjibu ni kawaida tu. Sasa unaposema utaanzia wapi kumweleza mr, wakati nafasi za kumweleza zinapojitokeza, wewe unanyamaza, basi niseme tu kuwa hizo nafasi ndizo ungezitumia kumweleza unayo yaona.

Pia Mambo kama hayo ni vizuri ukazungumza na mumeo na muweke mipaka kati yenu na huyo mfanyakazi.

Yeye kama Binadamu ambaye hana matatizo, kuwa na hisia na mwanamume si jambo baya, tatizo hizo hisia anazielekeza wapi. Wakati mwingine yawezekana hana wazo lolote baya na hajui kuwa anakosea kutokana na jinsi mnavyohishi

Kwa sababu unampenda, anza na mumeo kuwa apunguze mazoea kama si kuacha na huyo binti, pia mweleze huyo binti mipaka yake (Katika hali ya utulivu na ya kumshauri)
 
Eti unamuonea huruma ..Ndoa yako huionei huruma ?

Basi kama unataka usi affect chochote njia ni moja tu lakini ni ya kibaharia hzo nyengine hazitafanya kaz kama ataendelea kuwepo

Hivyo basi ukitaka aendelee kuwepo Fanya njia hii ya kibaharia zaidi

MPE Uhuru wa kutoka nje msifungie ndani ndo matokeo yake hayo akitoka nje akipata kijana wa kumchanganya mzee atakuwa safe



Au mwambie ndugu yako au mdogo wako kiume aje kukutembelea akae kama wiki kama ni mchangamfu kama ni mzto (mwanaume wa dar) akae mwezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom