Nahisi anachofanya Tulia ni sehemu ya mbinu za uspika

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,657
20,940
Nakumbuka wakati wa Makinda Ndugai tulikuwa tunamuona mbabe na Makinda tulimuona ana busara na analimudu bunge. Sahizi Ndugai anaonekana anabusara na na Tulia kauzu. Ndugai amepata wapi busara za ghafla? inawezekana ni mbinu mmoja awe mkali na mwingine mpole wa kuokoa jahazi.

Polisi nao huwa wana kitu wanaita good cop, bad cop. wanapohoji mhalifu polisi mmoja anajidai mkali na kauzu (bad cop) huku mwingine akijidai mpole anakusaidia dhidi ya yule kauzu (good cop). Mwisho wa siku wanakumanage na unaonyesha ushirikiano kilaini. Inawezekana Tulia na Ndugai wanawachezea wabunge wa UKAWA good cop, bad cop.
 
Tulia ni mfano wa ubovu wa elimu na wasomi wetu nchini. For sure wasomi wa namna hii hawataweza kuitoa nchi hapa ilipo na kuipeleka popote kimaendeleo. Ni jambo la ajabu sana kuendesha Bunge katika mfumo huu ikizingatia huyu ni binti mdogo sana kiuongozi. Who knows kwamba Former Prime Minister Sumaye angekuwa alipo? Who knows kwamba Lowassa-very long serving Minister angekuwa hapo alipo. Kweli watu hawajifunzi tu kutoka kwa watu hawa? Msingi wa ustawi wa maisha ya dunia ni busara tu kutoa haki. This is very sad!
 
Hakuna kitu hapo,hana busara na wala sheria haijui kabisa. Hiyo PhD yake ya ualimu wa sheria tu inamsaidia nini?Huwezi kujidai huku ukijua nafasi yenyewe ya kupewa
 
Wewe acha uongo kipindi cha makinda Ndugai ndo alikua mstarabu kuliko maza bana acha kupotosha... makinda alikua nusu ya tulia but Ndugai is fair
 
Mkuu Mipangomingi, umesahau kuwa kuna ulinganifu tofauti sifa. Kwa mfano MBAYA,.... MBAYA SANA... na MBAYA ZAIDI KULIKO WOTE! Wote ni wabaya ila viwango vya ubaya vinatofautiana. Viwango vya ujinga, uzuri, n.k hutofautiana. Kwenye darasa la wajinga, wanapofanya mtihani kunakuwa na wa kwanza hadi wa mwisho!
 
Dr Tulia huyu dada yuko vizuri hatari ata ndugai hafikii
kwa kupindisha vifungu na kwanini anapokuwa anapingwa hataki apingwe, watu wanampinga kwa vifungu na wanampa vifungu lakini yeye anakwambia hawezi kujibu, ndo unamsema ati yuko vizuri, ajibu kwa vifungu, wanaulizwa maswali anamkingia waziri asijibu sasa ndo uzuri gani, labda umemaanisha uzuri kwingine lakini sio akiwa bungeni, na akiendelea hivi bunge anazidi kuligawa, bunge lililopita limeenda vizuri bila mikwaruzo, la kwanza alilivuruga akitegemea wapinzani kinachowapeleka bungeni ni njaa, watu wanaenda kutetea maslahi ya wananchi wao waliowachagua na sio maslahi kwa aliyekuteua
 
kwa kupindisha vifungu na kwanini anapokuwa anapingwa hataki apingwe, watu wanampinga kwa vifungu na wanampa vifungu lakini yeye anakwambia hawezi kujibu, ndo unamsema ati yuko vizuri, ajibu kwa vifungu, wanaulizwa maswali anamkingia waziri asijibu sasa ndo uzuri gani, labda umemaanisha uzuri kwingine lakini sio akiwa bungeni, na akiendelea hivi bunge anazidi kuligawa, bunge lililopita limeenda vizuri bila mikwaruzo, la kwanza alilivuruga akitegemea wapinzani kinachowapeleka bungeni ni njaa, watu wanaenda kutetea maslahi ya wananchi wao waliowachagua na sio maslahi kwa aliyekuteua
Kakamatwa lissu ni maslai ya wananchi???
 
Kama Ndugai na busara yake aliwatimua siku ya ufunguzi wa bunge nadhani shida itakuwa hao jamaa ndiyo hawana busara.

Na kwa nini tutake busara upande mmoja tu wa spika ilhali upande wa pili hawatumii busara?

Kama issue ni busara then wote hawana budi kuitumia otherwise eye for an eye ndiyo inafaa sababu hakuna mtoto wala kichaa bungeni wa kupewa special treatment.
 
Wewe acha uongo kipindi cha makinda Ndugai ndo alikua mstarabu kuliko maza bana acha kupotosha... makinda alikua nusu ya tulia but Ndugai is fair
Makinda alijenga "Chemistry" na upinzani, na waliweza kufanya kazi pamoja katika baadhi ya maeneo. kuna wakati Makinda alimtumia sana Tundu Lissu katika hoja za kisheria, akimuunganisha na Andrew Chenge, na kumuweka pembeni George Masaju ambaye ndio mwanasheria mkuu wa Serikali. na alifanya hivyo kwa kuzingatia weledi tu, kwamba George Masaju alikuwa anapwaya katika hoja za kisheria. Pia kumbuka wakati wa hoja ya Escrow, upinzani na CCM walikuwa na makubaliano na ndipo kwa pamoja waliwatimua Muhongo na wenzake.

Ilikuwa kawaida kuona Tundu Lissu na Anna Makinda wanacheza muziki pamoja na mikwala ya bungeni. siwezi kujenga picha Tundu Lissu acheze muziki na Tulia!

Makinda ni kweli aliwabana sana wapinzani, lakini ndivyo alivyotumwa kufanya. cha tofauti ni kwamba kuna wakati alitumia busara yake (stori ya mbayuwayu) na kutafuta namna ya kufanya kazi pamoja na wale jamaa, wakati sasa hivi ni kublock wapinzani moja kwa moja. Tulia anacheza mchezo wa serikali ki-amateur mno, na hataweza kufaulu kwa njia hii at the end of the day. in short term, serikali inafurahia kwamba anafanya kazi nzuri, lakini hatimaye watagundua kwamba anawagharimu
 
Tatizo siyo yeye, tatizo ni waliomuweka pale! Ndo wanaomtuma.
 
Back
Top Bottom