Nahamia Dar, nijuzeni gharama za maisha

Nahamia Dar, nijuzeni gharama za maisha

Nawashukuru kwa ushauri wenu, kwa kweli mitaa ya dar mingi siifahamu yote , so cwezi sema nataka nyumba wapi Ila wazoefu ndo wanaweza kunisaidia kwa ushauri kwamba mitaa Fulani kuna nyumba za bei nafuu, na upande wa biashara kunalipa.
Sasa bei rahisi kwako sh ngap?


Mbagala...maramba mawili...gezaulole
 
''Yaani nimeangalia nyumba za kupanga insta kwenye Page za madalali yaani hakuna nyumba ya laki2 inayojitegemea zote ni kuanzia laki 4 kuendelea.''

KWANI NYUMBA ZA KUPANGA ZINAPATIKANA INSTA TU?
Hahaaaa huko Insta Anataka kwenda kupigwa tu ...subiri ajionee ukubwa wa jiji ulivyo
 
Hahaha umenifurahisha sana mkuu.
Kuna mtu aliniambia sokoni wanakata mboga za majani na nazi wanakuna kabisa ukifika nyumbani unachuja tu.

Dah, kweli bandari salama.
Hata iliyochujwa kabisaa ipo we ukinunua ukifika kwako unamwagia tu km ni mchuzini au vp
 
Duh. Basi sawa.
Nilivyo na kinyaa nitaanza kukagua mikono na kucha za waliochuja.

Kweli maisha ni mwendo kasi. Bush huku nazi unavuna mwenyewe, unafua, unakuna na kuchuja. Ya kuchujiwa mboga haitonoga.
Hata iliyochujwa kabisaa ipo we ukinunua ukifika kwako unamwagia tu km ni mchuzini au vp
 
Insta biashara wewe, nyumba hata ya elfu hamsini unapata!....njoo huku ukamuke jasho na madalali vitambi!
 
Nawashukuru kwa ushauri wenu, kwa kweli mitaa ya dar mingi siifahamu yote , so cwezi sema nataka nyumba wapi Ila wazoefu ndo wanaweza kunisaidia kwa ushauri kwamba mitaa Fulani kuna nyumba za bei nafuu, na upande wa biashara kunalipa.
Njoo kwetu mbagala mamii
 
Ungekuwa peke yako ningekupangisha kwenye servant quarters nyumbani kwangu, ambayo Ina sebule kubwa ambayo inaunganika na dinning room, chumba kikubwa cha kulala ambacho ni master,stoo, jiko, full tiles na sliding windows, A/C na inajitegemea Luku yake, Maji ya dawasco na kuna tanki la lita 1000 kwa reserve. Maeneo ya Mbezi ....na hii kwa wewe mgeni ningekupangisha kwa 150,000/- ..unilipe miezi mitatu mitatu tu.
Mkuu upon mbezi IPI ? Mimi nipo mkoani Ila nahitaji kupanga sehemu ambayo nitakuwa nafikia maana Mara kwa Mara nakuja dar ili kuepusha gharama za lodge kama hutojali tuwasiliane pm.
 
Back
Top Bottom