Nahamia Dar, nijuzeni gharama za maisha

Nahamia Dar, nijuzeni gharama za maisha

Nyumba nimejenga kwa jasho langu mkuu. Kwa heshima na taadhima akatafute nyumba ya kulipa mwezi mmoja mmoja sehemu nyingine..
Mabanda ya kuku tu huwezi kupata ya kulipia mwezi mwezi.
Kwahiyo unapingana na kauli halali kabisa ya serikali?
 
Sio kweli mkuu, wanaume wa dar ni wastaarabu mno. Alafu wanaupendo sna
Wastaarabu enhee!!!Ngoja ukifika tunakupa miezi miwili ya kukuchungulia ugumu na urahisi wako wa kupigwa sound.
 
Dalali kazini
Si kila mtu ni dalali kuna mwingine anataka kumsaidia tu kama binadamu mwenzake.Tatizo akili ndogo kila mtu unadhani ni dalali kuna watu humu ni matajiri haswa hawana njaa ila amependa tu kumsaidia.
 
Kwahiyo unapingana na kauli halali kabisa ya serikali?
Ninapingana kwa staili gani wakati ninalipa Kodi na tozo Stahiki katika nyumba husika!? Hii ni kauli yangu mimi ambaye nilijenga hii nyumba kwa jasho langu. Hii sio nyumba ya serikali.
 
Ungekuwa peke yako ningekupangisha kwenye servant quarters nyumbani kwangu, ambayo Ina sebule kubwa ambayo inaunganika na dinning room, chumba kikubwa cha kulala ambacho ni master,stoo, jiko, full tiles na sliding windows, A/C na inajitegemea Luku yake, Maji ya dawasco na kuna tanki la lita 1000 kwa reserve. Maeneo ya Mbezi ....na hii kwa wewe mgeni ningekupangisha kwa 150,000/- ..unilipe miezi mitatu mitatu tu.
Hicho ntamuungabishia jamaa yangu mkuu
 
Inshu ni kupata nyumba at least ya vyumba viwili na sebule na inayojitegemea kila kitu.

Na sehemu yenye biashara SNA, maana huku nilipo Nina biashara yangu.
Hizo nyumba za hivyo kwa bei hiyo zinapatikana chanika, ukonga na bunju bunju hivi
 
''Yaani nimeangalia nyumba za kupanga insta kwenye Page za madalali yaani hakuna nyumba ya laki2 inayojitegemea zote ni kuanzia laki 4 kuendelea.''

KWANI NYUMBA ZA KUPANGA ZINAPATIKANA INSTA TU?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] maisha ya digital hayoo
 
Nawashukuru kwa ushauri wenu, kwa kweli mitaa ya dar mingi siifahamu yote , so cwezi sema nataka nyumba wapi Ila wazoefu ndo wanaweza kunisaidia kwa ushauri kwamba mitaa Fulani kuna nyumba za bei nafuu, na upande wa biashara kunalipa.
Huyo MR.unayemfuata si ndio jukumu lake hili? Wanawake wa zama hizi kwa nini tunajibebesha majukumu mazito? Ama kweli siku hizi tunazaa kwa uchungu na tunatafuta kwa jasho kwa upumbavu wetu.
 
Hapa jirani kuna nyumba ni 200,000
Vyumba vitatu sebule
Jiko choo

Ila sehemu ya parking hamna

Karibu
Sinza palestina au? Kuna nyumba nzuri sana ila kuingia kwake vikona vingi na hakuna parking
daa wala huhitaji kuhangaika

1. maharage yaliyochemshwa yanauza kazi yako kuyaunga tu na nyanya
2. hata mgeni unamwambia ngoja nikutengenezee juice kisha unaenda nunua chumba cha jirani aloitengeneza
3. umeme ndo wala usiwaze mwenyenyumba anazima saa 1 asubuhi mpaka saa 3 usiku ndo anawasha
 
Back
Top Bottom