Nagu 'amchezea rafu' Sumaye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nagu 'amchezea rafu' Sumaye

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Sep 9, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,789
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  • Jina lake lapenyezwa kinyemela
  • Sumaye azungumza

  Uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) si lelemama, sasa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Mary Nagu, anatajwa 'kucheza rafu' kumdhibiti bosi wake wa zamani, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

  Jina la Nagu, linadaiwa kupenyezwa baada ya Katibu wa chama hicho wilaya ya Hanang' kubadilisha muhtasari wa kikao cha kamati ya siasa ya wilaya.

  Kufanikiwa kwa njama hizo kunatajwa kuwepo ‘mkono' wa Nagu aliyekuwa mshirika wa karibu wa Sumaye kwenye kura za maoni, kuwania urais kupitia CCM mwaka 2005.

  Taarifa kutoka ndani ya ofisi ya Katibu wa CCM wilaya ya Hanang', zinadai kuwa Kiongozi huyo, Allan Kingazi, alibadilisha muhtasari wa kikao kilichomuengua Nagu kuwania nafasi ya mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM.

  Kwa mujibu wa marekebisho ya Katiba ya CCM, wajumbe wa Nec wanachaguliwa katika ngazi za wilaya, tofauti na mkoa ilivyokuwa awali.

  Nagu alienguliwa kuwania nafasi hiyo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kutokidhi kanuni za chama hicho.

  Uamuzi huo ulihusisha kanuni zinazokataa wajumbe wa nafasi hiyo, wasiwe wenye majukumu mengi ya kikazi kama ilivyo kwa Nagu ambaye ni Mbunge na Waziri katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

  Wakati jina la Nagu likielezwa kurejeshwa kinyemela ili likajadiliwe kwenye ngazi ya mkoa, taarifa zinazidi kuainisha kuhusu matumizi makubwa ya rushwa, yaliyofanikisha mpango huo.

  "Kiongozi wetu amepewa hongo ya Shilingi milioni mbili, kati ya hizo milioni moja na nusu azipeleke kwa (XXXXXX) anamtaja kiongozi wa ngazi ya mkoa) na Shilingi 500,000 abaki nazo," kilieleza chanzo chetu kutoka ndani ya CCM.

  Lengo la fedha hizo zinazopingwa kwa matumizi ya kufanikisha kuchaguliwa ndani ya CCM, linatajwa kushawishi yafanyike mabadiliko ya muhtasari na kukubaliwa katika ngazi ya mkoa, ili kufikia tarajio kusudiwa.

  CCM wilaya ya Hanang' ilipokea na kujadili majina ya wagombea watano waliojitokeza kuwania ujumbe wa Nec, ambapo majina ya Sumaye na Leonsi Marmo yalipitishwa baada ya kukidhi vigezo.

  Nagu alienguliwa licha ya wajumbe watano kati ya 12 waliohudhuria kikao hicho, kujipambanua kuwa watetezi wake, wakitaka jina la Waziri huyo liwasilishwe mkoani.

  Taarifa zaidi zilidai kuwa Kijazi, alionekana kumtetea Nagu ili apitishwe kwa madai kuwa, amepata agizo (barua) kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama.

  Agizo hilo linaelezwa kutaka wilaya ya Hanang' ilipitishe jina la Nagu kwa madai kuwa anaandaliwa kwa ajili ya kugombea urais mwaka 2015.

  Hata hivyo, ilidaiwa wajumbe saba kati ya 12 walibaki na msimamo wa kutaka kanuni za CCM zifuatwe na Nagu aenguliwe katika kuwania nafasi hiyo.

  Kura zilipigwa kufikia uamuzi huo, ndipo Nagu akapata tano wakati 12 zilitaka aenguliwe.

  Mwandishi wa habari hizi alipowasiliana naye kwa njia ya simu, Kingazi alikanusha na kusema taarifa za kamati ya siasa ni siri na kwamba mtu anayezitoa hatambuliwi kwa mujibu wa kanuni na taratibu za CCM.

  Aidha, alisema taarifa za waliopitishwa kugombea nafasi ya NEC zitatolewa baada ya kamati ya siasa ya mkoa kupitia majina yaliyopendekezwa.

  "Kwa hali hiyo taarifa zinazotolewa sasa sio sahihi," alisema Katibu huyo wa CCM wa wilaya ya Hanang'.

  Naye Katibu wa CCM mkoani Manyara, Nden'gaso Ndekubali, alipowasiliana na Mwandishi wa habari hizi, hakukataa wala kukubali kuhusika na hatua yoyote ya kufanikisha njama hizo.

  Hata alipoulizwa ikiwa anahusika kwa namna yoyote na tuhuma za rushwa inayodaiwa kuwasilishwa CCM mkoa wa Manyara, kushawishi kulikubali na kulijadili jina la Nagu, alimgeuzia kibao (Mwandishi) na kumhoji "wewe umehongwa ili uandike habari hiyo?"

  Naye Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Wilson Mukama, alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kujibu madai ya wajumbe kuwa, alitaka wajumbe hao kupitisha jina la Nagu kwa kuwa anaandaliwa kugombea Urais, alijibu kwa kifupi " sihusiki na lolote linalotokea au kuendelea kutokea Hanang'.

  Sumaye alipowasiliana na NIPASHE Jumapili jana, alisema hana taarifa zozote kuhusu majina hayo, kwa madai kuwa taarifa za kikao zinakuwa siri.

  "Hata mimi ninazisoma sana taarifa hizo kwenye magazeti, lakini sina uhakika kwa maana ninasubiri uamuzi wa vikao husika," alisema.

  Nagu alipotafutwa kujibu madai hayo simu yake ilionyesha kuwa inatumika kwa muda mrefu.

  Alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno hakujibu hadi tulipokuwa tunakwenda mitamboni.

  CHANZO:
  NIPASHE JUMAPILI

  Kweli urais umekuwa EASY hata Mary Nagu anaota kuwa Rais?
   
 2. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Acha wafu wawazike wafu wenzao
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  JK amefanya urais uonekane ni rahisi sana.....kweli hata kilaza Nagu nae anaota "urahisi"
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nagu hawezi kupita....
   
 5. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  mimi mwenyewe nauwaza huo urais
   
 6. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Kwani urais wa Tanzania ni cheo cha majaribio?...
   
 7. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tunasubiri matanga tule birian ng'ombe
   
 8. n

  ngangali Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kabisa mkuu.
   
 9. H

  HByabatto jr Senior Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM kwa uchu wa madaraka bwana! Nyie malizaneni tu sisi yetu macho...!
   
 10. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,775
  Trophy Points: 280
  teh teh teh teh!! Yani hadi mary nagu anautaka urais???
  Aisee Tanzania imekua nchi ya mchezomchezo.
   
 11. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mbowe aliwahi kusema 'Siongozi kundi la wasaka urais', Kwahiyo wengine wanaongoza makundi yanayopigana vikumbo kuingia Ikulu.
   
 12. LESIRIAMU

  LESIRIAMU JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 4,003
  Likes Received: 2,222
  Trophy Points: 280
  Hebu wadau tujiulize kama wao kwa wao wanachezeana rafu za namna hii, inakuwaje wanapokutana na mpinzani wa upande wa pili????
   
 13. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  From Nipashe Jumapili 9/9/2012 Title Nagu 'amchezea rafu' Sumaye

  Mh Nape hawa CDM kama hatuta mwambia Mzee wetu Tendwa kuwafuta watatupeleka pabaya. Wameanza kuua watu, then wamemuua Mwandishi kwa bomu la mkono walilolitupa na sasa wanatoa Rushwa kumzuia Sumaye. Unajua Mh Sumaye aligombania Urais 2005 pamoja na Mwenyekiti, sasa CDM wanaona ni tishio 2015
   
 14. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ukweli mimi namuunga mkono Fredy Sumaye kuwa Rais wa Nchi hii, ninazo sababu nyingi lakini kubwa ni kuwa ni mtu mwenye uvumilivu wa kisiasa tofauti na akina lowasa et la. Sumaye ni vema akafikiria kuitimiza ndoto hiyo kupitia cdm manake huko ccm mh!
   
 15. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  CDM kufutwa, Who is this solid gamba called Nape? What the hell about bomu la kutupwa kwa mkono? oh yes yes...you mean grenade? why not flying object because it seems hata bomu ni flying object?.aaaaaaaaaaaaugh!!sasa naanza kukuelewa!
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Hahahahha! Kweli Nape anyokazi kubwa!
   
 17. l

  langtan Member

  #17
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Pamoja na yote kuhusu chadema kuwa chama makini lakini ukweli huyu Sumaye anafaa kabisa kushika nafasi hiyo anayoitaka na uwezo anao kabisa kuitoa nchi hii ktk laana inayoikabili yaani rushwa,ubadhirifu wa mali ya umma na ufisadi unaosumbua nchi hii.Nakumbuka walipomuengua ktk kinyanganyiro hicho kule dodoma nilisikitika sana*2,ila bado nina matumaini nafasi hiyo anayo na siku moja atakuwa rais wa nchi hii tu.
   
 18. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  akili ndogo kuongoza kubwa!
   
 19. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ningeruhusiwa kumtukana mleta maada ningefanya hvyo maana kuchukua muda wangu kusoma upumbavu wake nimepoteza mood
   
 20. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  kwani kikwete ana kitu gni cha ziada kiuongozi ambacho mary nagu hana? urahisi tanzania hata mi ukiniweka magogoni mbona nauweza tu...kuhudhuria misiba na kusafiri nje ya nchi kwani nani asiye weza? kama watz wakicharuka mitaani nauchuna na kusubiria upepo ipite...upepo ukipita naendeleze mtoko tena out ya tz...life goes on! mwacheni nagu agombee umagogoni!
   
Loading...