Nafsi inaniuma kwa kushindwa kumssidia asiibiwe

273

Member
Sep 12, 2017
63
82
habari wakuu,

nimeona ni vyema kama nikishea na ninyi mkasa huu mfupi wa wizi nilioushuhudia siku kadhaa zilzopita. wanawake kuweni makini sana na mikoba yenu mnapokua mpo kwenye daladala hasa pale unapokua mmesimama(mmeshika chuma)

nilipanda gari ya segerea maeneo ya ubungo darajani nkielekea external, wakat konda akisubiri abiria wajae wakapanda jamaa wawili ambao ukiwaangalia kwa umakin unagundua si watu wazur(either wateja au wezi) maana wana alama za kujeruhiwa maeneo ya usoni na macho ya uteja.

bas mmoja akawa amepata seat amekaa ila huyu mwingine akawa amesimama, tulkua kama abirua watatu tumesimama. gari ilivofika riverside wakapanda wamama wawili mmoja akapita kwenda kusimama nyuma kabisa mwingine (ambae ndo aliibiwa) akawa kasimama karibu na mlango,,,,,,huyu mwizi akawa nyuma yake na mm ndo nikawa nafuatia

ghafla huyu mwizi akaingiza mkono kwenye mkoba wa hyu mama sa sijui huyu mama hakufunga zipu cjui huyu mwizi aliifungua kiujanja, baada ya kuingiza mkono akachomoa pochi ndani ya ule mkoba na kuichomeka ndani ya boksa

nikiri kuwa tukio zima nilishuhudia japo ilikua haraka sana. kuacha mm kuna abiria kama watatu hiv naamin na wao walishuhudia tukio hili ila cha kushangaza si wale abiria wala mm alifungua mdomo wake, wote tulibaki kimya tukiangaliana kitu ambacho nkikumbuka nafsi inaniuma sana kwa kushndwa kuwa responsible mungu anisamehe.

yule mwiz akashukia hostel akatokomea uku nikimuona. na mm hadi nashuka yule mama alkua hajagundua kama kaibiwa cjui baada ya kugundua alkua katka hali gan mungu amfanyie wepesi

mytake,
wanawake muwe makini sana na pochi zenu na mikoba, hasa mnapokua mmesimama kwenye daladala.....pia kwa vijana wenzangu wizi sio mzuri hata kdgo, ile fedhea anayoipata mtu aloibiwa itakusumbua naisha yako yote.

asanteni,
 
Kuna kitu kinaitwa bystander effect. Kinatokea kitu kinahitaji responsibility lakini kila mtu anaacha kukifanya akitarajia mwingine awe responsible.

Ungemwambia yule mwizi "Hoya unafanya nini?" Ungeshangaa idadi ya support ambayo ungeipata.

Hata hivyo haihalalishi wewe kua irresponsible.
 
Kama we ni mwanaume hii ni aibu sana ni bora hata usingethubutu kuhadithia upuuzi kama huu,ulipaswa kumwambia mwizi rudisha kimyakimya asingekataa angeona noma na kwa hofu ya kupigwa angerudisha angalau ungekua umemsaidia huyo mama kuliko kuja kueleza vitu kama hivi
 
Labda niulize kwanini hukufanya kitu kuzuia wizi huo? Uliogopa usalama wako au

Umeonyesha irresponsibility kama watanzania wengine ambao bus inakimbia hawasemi kitu ila ajali ikitokea ndo wanasema dereva alikua anakimbia sana.
 
Umezingua mtoa mada. There was no threat to your life katika hayo mazingira hivyo ulitakiwa ureact. You had the upper hand.

Kinachofuata: wanaume wa dar
 
Hivi huoni aibu kwa kuwa muoga kiasi hicho? yani unaogopa teja? huna hata mkanda wa suruali wenye chuma? we ni pumbafu sana mwanaume gani sasa wewe? mimi wanaume togwa kama wewe hata ppch hupewi..eti roho inakuuma..so what? ungemkabili na kusema huyu ni mke wangu rudisha hiyo pochi Nitakuchinja na jamaa zako na gari haisimami mpk polisi
 
Mmh. Yaani kuna wanaume ni waoga sijawahi ona itakuwa uliogopa kuchanwa chanwa na viwembe kwa kuwa chaumbea.

Ila ulikosea kwa kuwa ilikuwa ndani ya daladala ungesema tu na hapo abiria walio wengi wangekuwa upande wako na huyo mama angepata vitu vyake .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom