Nafikiri nilikosea kusoma degree ningeishia form four

Tatizo sio wewe Wala jamaa zako kusoma degree, sioni kama kusoma Kuna shida ,shida ni mzazi wako alibidi akuandalie mazingira ya ajira
 
Simply Taaluma ni zile zenye kufuata mlolongo rasmi uliowekwa na taasisi husika za elimu, lakini kwenye ujuzi ni tofauti kidogo inaweza kuwa hakuna mlolongo maalum na mtu akapata ujuzi! Mfn. Anayejua Kuendesha gari ana ujuzi lakini walio wengi unakuta alijifunzia kitaa! Lakini Huwezi kumkuta Daktari au Mwalimu kajifunzia kitaa hiyo taaluma yake na aka-practice to the excellence. Nimejaribu hivyo
Shukrani mkuu
 
Nna miaka 30 kuna mtu pia ana miaka 33.

WOte wamemaliza degree 2017/19 hawa watu wanapiga mishe za hapa na pale mitaani (vibarua) wakisubiri ajira za ualimu waajiriwe.

Kuna jamaangu mmoja leo kaamka kapita kunisalimia agongee chai
akaanza hoja, Dah maisha sijui nliyakosea wapi. Yani mishe haziendi kabisa hadi kupata elf2 ndani ya saa24 ni mtiti.

Namsikiliza tu. Kaongea mengi kweli ila kwa ujumla akasema amepoteza jumla ya miaka 2 ya form 5&6
Miaka 3 degree
Miaka 8 kupiga vibarua vya laki 1 na laki 2 za kufundisha na kujitolea mashule 12 aliyofanya kazi

Jamaa ana familia leo kaja kunywa chai geton kwangu sijui home kwake mke na watoto wamekula nn asbh. Mwingine mlokole namjua ila mpk leo ana siku ya 16 anafunga kubana bajet ale usiku tu alale

Nafikiri shule sikuhizi haina umuhimu. Mladi tujue kusoma na kuandika kisha twende veta kusomea ufundi turudi mtaani kujiajili ila haya ya form 1-4, 5&6, degree labda hizi zinafaa marekani na dubai sisi tanzania technical skills ndio zinatufaa
Huyo jamaa ajira hana kiasi kwamba kula yake tu shida, sasa ameoa ili iweje?

Watu kama hawa wake zao wakiwasaliti wanawaona wabaya kumbe chanzo cha tatizo ni yeye mwenyewe.
 
Physiotherapy haitakuja kukosa soko.
Watu kila siku wanauguza magonjwa yanayo hitaji huduma za hao wataalamu na wengi wanahitaji hizo huduma wakiwa nyumbani.
Watu watajiajiri kwa hiyo taaluma.
Ukosefu wetu wa umakini ajali kila siku, ulaji wetu mbaya magonjwa yanayo sababisha stroke sijui kiharusi ni mengi sana watu wanahitaji physiotherapist.
Chef je? Mana kila siku watu wanakula.. lakin hakuna machef hawana ajira?
 
Tatizo sio wewe Wala jamaa zako kusoma degree, sioni kama kusoma Kuna shida ,shida ni mzazi wako alibidi akuandalie mazingira ya ajira
Wazaz maskini hawana huo uwezo. Jkichunguza vizur utajua kuwa jobless kama status ni forcefully idleness... Unemployment kama tatizo ni suala la kuangalia sana professionals ambao hawana kazi za kufanya (jobless) au wanafanya kazi nje ya specialisation zao.

Leo hii ukisome engineer na ukaishia kuwa bar man au bodaboda sio kwqmba wewe ni jobless. Na sio kama tatizo la ajira halipo. Na tatizo hili la ajira halina uzito sawq kati ya mtu na mtu na jamii na jamii. Kuna sehem hili ni kubwa zaidi, mathalan kuna watu wnafahamika leo hii ukimwambia umpeleke ualim au upolisi atakataa kwa kigezo cha kuwa haoni maendeleo kwenye kaz hizo. Lakin kuna watu wanazisotea hizohizo mwaka wa 10 now. Hii kitaalam inaitwa "Social imequality"

Mimi nitoe rai kwa commentators wote, tatizo la ajira haliwez kuwa kigezo cha kuupima ubora wq elim iliyopo kama inafaa au haifai. Elimu kama taasisi inazalisha watu wenye taaluma au ujuzi fulani ili kutumia ipasavyo taasisi fulani kukidhi mahitaji ya jamii. Wataalam hao kuzalishwa then kukuta nafas chache eti wengine wafanye kazi zingine ni suala la pyramidal scheme lililopo kwenye mfumo wote wa maisha ya kisasa

Wasomi waliokosa cha kufanya sio wajinga au mibichwa yao ina makomwe, la hasha. Ni wahanga wa mfumo uliopo kama ilivyo maskini au waliofeli darasa la saba, form four au kudisko chuo na kuna wengine wanafeli kwenye saili. Lengo la usail ni kuendeleza kupunguza watu kama mitihani iliyopunguza watu form four, ikiaminika kuwa bado watu ni wengi
a nafas ni chache. Mbaya zaidi mfumo huohuo hautoi suluhu kwamba huyu aliefeli kufika juu aidha kwa kufeli la saba, form four au kukosa ajira afanywe nini mana mfumo huo huo ndio uliowapunguza technically.

Kwa kuzingatia aya ya juu kama "swali" basi jibu ni kwamba waliokuwa juu ya mfumo ambao ni wanasiasa ni jukumu lao kuweka mikakat wezeshi kusaidia hawa wahanga aidha kwa kuongeza nafas ha kuwaajiri au kuweka mikakati nje ya mfumo na kuwapeleka huko. Kuna miradi ya kuwezesha vijana kifedha na kirasilimali, uwepo wa elim mbadala na mikopo ya vikundi manispaa ili wachague njia mbadala

Cc. Lamomy
 
Degree in social work and environment hustle hii inapatikan chuoni kwetu ila vijana hawataki kuisoma
 
Umetoa dini lenyewe kabisa, Igweeeeeeeee 😍
 
Chef je? Mana kila siku watu wanakula.. lakin hakuna machef hawana ajira?
Watu binafsi hawaitaji chef kuwapikia labda kwenye matukio maalum mfano sherehe au misiba au mikutano ambapo bado huko wanagombania nafasi na wapishi wa mitaani wasiokuwa na vyeti vya culinary art (cooking).
Kwenye fani ya physio watu wa kawaida hadi masikini akihitaji recovery sijui rehabilitation kwa wanamichezo nao lazima apate certified professional. Huyo mtaalamu utaona hagombanii kazi na wasio somea.
Mwamko wa michezo nchini unaenda kuongeza ajira kwa physiotherapists.
 
Watu binafsi hawaitaji chef kuwapikia labda kwenye matukio maalum mfano sherehe au misiba au mikutano ambapo bado huko wanagombania nafasi na wapishi wa mitaani wasiokuwa na vyeti vya culinary art (cooking).
Kwenye ya physio watu wa kawaida hadi masikini akihitaji recovery sijui rehabilitation kwa wanamichezo lazima apate certified professional hagimbanii kazi na wasiosomea.
Mwamko wa michezo nchi unapenda kuongeza ajira kwa physiotherapists.
Be exposed
 
Tatizo sio marekani na dubai shida ni Elimu yetu haimwandai mtu kujiajili
Mimi ningekuwa waziri wa Elimu au Raisi imekuwa chuo ni miaka 4 miaka 1 dalasani miaka 2 mafunzo kwa vitendo kwaka wa mwisho ni project
ELIMU haina shida kabisa... Shida ni wewe na familia yako... Kusoma hakuna anaelazimishwa ni wewe na umasikini wako.
 
Huenda ungeishia form 4 na bado maisha yakakupiga vile vile…huenda ungeenda Veta na ukaja kitaa life likakunyoosha…Haya mambo hayanaga formula,kama ulipata nafasi ya kusoma huna haja ya kujutia kupata maarifa ya hio taaluma ulosomea
 
Shida ni pesa ajira na makolokolo mengine ni sababu tu watu tunataka pesa tena pesa nyingi sio vipesa
 
Back
Top Bottom