Nafikiri MESSAGE ameipata, Lipumba alidhani umma uko upande wake.

Nafikiri MESSAGE ameipata, Lipumba alidhani umma uko upande wake.

Hii ni message kubwa sana kwa Lipumba mwenyewe, wafuasi wake na serikali ikiwakilishwa na msajili wa vyama, kuwa, pamoja na yote yanayofanywa na serikali kwa mgongo wa msajili na vyombo vya dola kumsaidia Lipumba kuihujumu CUF, lakini leo UMMA wa watanzania umekataa umewaambia wazi kuwa jamii inaona na inajua nani mkorofi ndani ya CUF.

Kwa Umoja wao wananchi wamekataa uonevu, bila kujali vyama vyao wamesimama upande wa HAKI wa viongozi halali wa CUF, wameulinda uongozi halali kwa hali na mali kwa kuwapa kisago kitakatifu vibaraka wa prof. Lipumba mwenyekiti aliyejiuzulu na baadaye kufukuzwa uanachama. Sijui kama watarudia tena.
View attachment 499658

Hongera sana wananchi wa Mabibo Kinondoni kwa kweli leo mmenifurahisha sana na mmekonga nyoyo za wapenda amani wengi, bila ninyi huenda madhara makubwa yangetokea.
Baba Mwajabu kapewa kisago kikali sana , ameitia aibu familia yake .
 
nahisi bashite atakuwa na mkono pia kwenye uhalifu huu. Kama kawaida take time bounce tena. zero ni zero tu
 
Nimefurahi sana kibaraka wa lipumba alivyokula kipigo cha mwana ukome sijui kama atakubali tena kutumiwa na Lipumba a.k.aBwana yule
Huyu prof hafai hata kidogo, ona sasa baba wa watu kisigino kimelika cjui atamlipa nini?
Babu mzima na elimu yake anafanya hovyo kisa uroho wa madaraka anafikiria atazikwa na hicho cheo, Mungu anamuona ipo cku atahukumiwa na damu za hawa vibaraka wake.
 
Huyo ni mhalifu kama mhalifu mwingine na hivyo alitakiwa aadhibiwe vilivyo na sio kumtekenya kama walivyofanya hao wananchi. Kama wakipelekwa polis wanaachiliwa bila kushitakiwa sasa SI wangemalizana nae tu hapo ili kutoa fundisho kwa wahalifu wengine wenye Tabia za kihayawani kama j
hizo? Kama watu wamevamia Eneo tena wakiwa na silaha maana Yake walidhamilia kumwaga damu!
 
Anaandika Julius Mtatiro (Facebook page yake)

TAARIFA ZA HIVI PUNDE:
Najulishwa kwamba, mtu aliyetoa BASTOLA wakati wa uvamizi wa mkutano wa CUF kwenye hotel ya Vina, Mabibo - Dar leo hii ni Ofisa wa Usalama wa Taifa. Watu waliolifuatilia gari mojawapo kati ya yale yaliyowabeba MUNGIKI wa Lipumba (na kuwaondoa Vina Hotel baada ya kupiga, kuumiza na kupora waandishi na viongozi wa CUF), wamenipa ushahidi unaoonesha kuwa mtu huyo ni Askari wa vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama. Natoa wito kwa waandishi wote wa habari waliokuwepo kwenye eneo la tukio watukabidhi picha zote za video na mnato ili tumsake mhusika na kuiweka picha yake hadharani. UOVU hauwezi kudumu na kamwe hatuwezi kuukalia kimya. Leo nimekaa na kujiuliza, hivi kwa mfano njama za kuisambaratisha CUF zinazoongozwa na dola zikishafanikiwa, Tanzania itakuwa na viwanda? Ajira zitapatikana? Kina mama wataacha kujitwisha ndoo za maji vijijini? Kilo ya Unga itashuka bei? Kwamba kuna uhusiano gani kati ya dola kutumia nguvu kubwa sana kukisambaratisha chama kimoja badala ya kutumia nguvu hizo kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja? Too shameful!
[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG].
 
Katajwa Lipumba ndiye huwafadhili kufanya haya! Kwanini asikamatwe akahojiwa na yeye ili kuujua ukweli? Hii hali ikiachiliwa IPO siku itasababisha mauaji. MTU anavamia mkutano na silaha mchana kweupe HALAFU polis wapo na Inteligensia yao imeshindwa kufanya kazi?
 
Duuuuuh. Kudundana twapeana hongera badala ya pole. Siasa uchwara mbaya sana. Nafuu JPM kaamua kufanya yake na wanasiasa waendelee na ya kwao. Maana akianza kuwafuatilia wafanyayo wanaweza kumuondoa kwenye barabara na kukuta anaingiza porini Lori.
Nyie huku twanganeni na hakuna wa kuamulia hadi wenyewe mpate akili. Dadadeki.
This reply is deliberately constructed to favor certain figures
 
Wamekupa ushahidi gani?
Huu hapa tena live bila chenga.
image.jpeg
 
Chadema acheni kuiharibu CUF narudia kusema

Hivi kikao chandani cha CUF kinauhusiano na Chadema,mbona unaakili za kukaliwa na Lipumba??

Uhaini wa Lipumba mko busy na Chadema.Duh kweli Chadema imewafanya vibaya siyo utani.
 
Chadema mmepoteza image yenu ya chama cha wapinga ufisadi, chama cha wapenda haki na pia mmejisahau sana mpaka kufikia kukumbatia maovu na madudu ya ccm ya enzi zile.

Ungekuwa na akili hata za kupewa ungeweka mwingine kuhusu Chadema lakini kwenye hili UVCCM limewashinda mnabaki nyuma meno tu.
 
Chadema mnaiharibu CUF sio mambo hayo na hii dhambi inawahusu sijui kama mtasalimika 2020

Badala ya kujenga Viwanda mko busy kuua Upinzani kama mlitegemea Chadema kufa basi mjue muda wenu wa kuishi pia umekwisha.
 
Watu wa dar bana!!! Yaan wameisha mchakaza mtu then wanamuweka mtu kati nakuanza kumshangaa au ndio wanaanza kumsema sasa
Sasa ulitaka wafanyaje wakati wameshamdhibiti?Huoni kwamba ukweli ulikuwa unatafutwa ambao ndio source ya hii habari?
 
Lipumba anaujua ukweli kwamba yeye ndio anayeleta chokochoko kwenye chama.
 
Lipumba anaujua ukweli kwamba yeye ndio anayeleta chokochoko kwenye chama.
Muda wake ndani ya CUF ni mfupi sana, inaonekana mission aliyotumwa ameshindwa kuitimiza soon ataachwa ajifie kifo cha mende, CCM haina rafiki kama adhanivyo.
 
Hii ni message kubwa sana kwa Lipumba mwenyewe, wafuasi wake na serikali ikiwakilishwa na msajili wa vyama, kuwa, pamoja na yote yanayofanywa na serikali kwa mgongo wa msajili na vyombo vya dola kumsaidia Lipumba kuihujumu CUF, lakini leo UMMA wa watanzania umekataa umewaambia wazi kuwa jamii inaona na inajua nani mkorofi ndani ya CUF.

Kwa Umoja wao wananchi wamekataa uonevu, bila kujali vyama vyao wamesimama upande wa HAKI wa viongozi halali wa CUF, wameulinda uongozi halali kwa hali na mali kwa kuwapa kisago kitakatifu vibaraka wa prof. Lipumba mwenyekiti aliyejiuzulu na baadaye kufukuzwa uanachama. Sijui kama watarudia tena.
View attachment 499658

Hongera sana wananchi wa Mabibo Kinondoni kwa kweli leo mmenifurahisha sana na mmekonga nyoyo za wapenda amani wengi, bila ninyi huenda madhara makubwa yangetokea.
CUF bahna! chama mmekiuza wenyewe kwa mamvi kwa bei rahisi ya mwezi mmoja wa October mmeshasaau mnataka kumuangushia zigo Lipumba peke yake.
Kumbukeni mlivyokiuza na pesa alizopewa madevu wa visiwani ile ndio laana inayowatafuna.
 
Back
Top Bottom