Nafikiri Biblia na Qur'an ni project zilizofanywa na wanadamu - Prove me wrong!

Yes, Kwanini Mungu atuumbe na kutuweka mitiani ambayo anajua kabisa kuna wengi wetu itatushinda, Je alikuwa hawez kuumba Dunia ambayo tuko free kuish na kumsifu tu yeye?
Ndugu Fabian, Muumba wetu hafikirii kama tunavyofikiri sisi binadamu.

Yes, Kwanini Mungu atuumbe na kutuweka mitiani ambayo anajua kabisa kuna wengi wetu itatushinda, Je alikuwa hawez kuumba Dunia ambayo tuko free kuish na kumsifu tu yeye?

Ndugu Fabian, Muumba wetu hafikirii kama tunavyofikiri sisi binadamu.
Kwanza uwezo wetu wa kufiri uko limited (1 Wakorinto 13:9); pili kutaka kumjua Muumba kwa kutumia akili zetu ni upuuzi na ujinga.
 
pili kutaka kumjua Muumba kwa kutumia akili zetu ni upuuzi na ujinga.


Kwa hiyo akili zako zina upuuzi na ujinga katika kumjua mungu???

Hizo akili kakupa nani??-- au kakupa shetani??!

Akili zina kazi gani?? au ni za kutongozea??!!.

Be careful of your talks.😒
 
Kweli kabisa tukubali uumbaji katika Biblia? Adam na Eva walikuwepo kweli? Ni kwa nini aanze na mwanaume na kumsahau mwanamke? Mungu hakutaka 50 kwa 50? Ni hadithi zilizotungwa na wajanja? Eti mpe Mungu sadaka! Ana shida na "vipesa " vyako? Naunga mkono hoja!
 
Kwa hiyo kundi fulani la watu wakakaa chini na kuandika vitabu ili kumsifia Mungu ambaye hawamjui wala hawajui kama yupo.Ili iweje? na lengo la wao kufanya hvyo ni nini hasa?,na ili wapate faida gani??.
 
Nilikuwa na maana yangu nzuri tu. Hatubabaishi ndugu kama unavyodhani.
Ratiba ama shughuli ya kusulubishwa Yesu ilianza saa tatu hadi saa tisa. Japo mwili wake uliondolewa punde tu kabla ya saa 12 jioni. Yesu alikata roho saa tisa ndivyo inavyosema Biblia. Matukio yaani msululu wa matukio ulianza saa tatu asubuhi na kuishia saa tisa kwa kifo cha Yesu yaani kukata roho. Soma vielelezo hapo chini.

Luka 23: 44 - 46
44Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda, * 45jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati. * 46Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.


Hapa Luka ameandika kwa ufupi sana tukio hili ametupa katikati mwa tukioa na moja kwa moja ametupa tukio la mwisho bil kubaini ni muda upi hasa ifo hicho illitokea.

Math 27:45 - 50
45Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. 46Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? * 47Na baadhi yao waliohudhuria, waliposikia, walisema, Huyu anamwita Eliya. 48Mara mmoja wao akaenda mbio, akatwaa sifongo, akaijaza siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha. * 49Wale wengine wakasema, Acha; na tuone kama Eliya anakuja kumwokoa. 50Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.

Mathayo ametupa kipindi cha kati pia cha saa sita na kile cha mwisho cha kifo cha yesu cha saa tisa.

Marko 15:25
25Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha. 26Palikuwa na anwani ya mashitaka yake iliyoandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDI.

Marko 15:33 - 37
33Na ilipokuwa saa sita, palikuwa na giza juu ya nchi yote, hata saa tisa. * 34Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? * 35Na baadhi yao waliosimama pale, walisema, Tazama, anamwita Eliya. 36Na mmoja akaenda mbio, akajaza sifongo siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha, akisema, Acheni, na tuone kwamba Eliya anakuja kumtelemsha. * 37Naye Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho.

Marko anatupa yote ya saa tatu (Mk 15:25), saa sita na saa tisa (Mk 15: 33-37). Saa tatut wanaanza kumsulibisha kumgongomelea kwenye mbao shina. Kumwinua na matukio mengine yanayoelezwa kwenye maandiko ikiwemo mazungumzo msalabani na majibizano baina ya wale majambazi na jibu lake kwa mmoja wao. Marko anatueleza pia baadhi ya matukio ya saa sita giza katika nchi na kumalizia na matukio ya saa tisa kukata roho kwa Yesu.

Hatubabaishi.Nawasilisha.
Jamaa anataka muda kamili yaani saa.dakika,sekunde.Hapo hapo anasahau kwamba mfumo wa kutizama muda kamili ulianza kwenye karne za karibu baada ya Yesu,wakati wa Yesu watu walikuwa wakitizama saa kupitia position ya Jua lilipo.Hata sasa hivi ukiangalia position ya jua unaweza kujua ni saa ngapi,ila hutoweza kujua ni dakika ngapi.
Anajitoa ufahamu tu au hajui anauliza nini.
 
Eti luka kaandika kwa kifupi! We unaona maneno ya Mungu ni ya kuandikwa kifupi kama barua ya mchumba! We sema SAA ngapi? Mambo ya shughuli ya kusulibiwa haina tija hata kama ingeanza juzi yake, swali alikufa SAA ngapi? Luka kasema yake, Marko yake, mathayo yake Yohana yake, bado unaona ni sawa? Unakuja na mapendekezo yako eti "Shughuli" ya kufa ilianza SAA 3, ina maana huyo Mungu alishindwa kuwapa upako hao waandishi waandike sawa sawa?
Mbona unaongea kwa jazba,au ndio nyie wafia dini ushakaririshwa kwamba dini fulani ni ya uongo,tuliza akili soma elewa.
44Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda, * 45jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati. * 46Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.
Unaelewa maana ya hayo maneno hapo?,ngoja nikutafsirie.
1.kenda=9,hili ni neno la kiswahili fasaha tu,hata ukienda BAKITA watakwambia ni 9
2.Jua huwa linapungua nuru kuanzia saa 9.Hii ukitaka kuthibitisha kaa nje angalia nguvu ya miale ya jua huwa inapungua saa ngapi utagundua ni sa 9.
3.Mikononi kwako naiweka roho yangu,hayo maneno yanamaanisha alikuwa anaelekea kukata roho.
Kingine unatakiwa uelwe kwamba,zamani kulikuwa hakuna utaratibu wa majira kama unayoyaona kwenye saa ya mkononi,watu walijua saa kupitia position ya jua lilipo,Hata kipindi cha mtume Muhammad (S.A.W) nauhakika saa bado zilikuwa hazijagunduliwa,walikuwa wanatumia mfumo huo huo wa kutizama jua.Ni sawa na leo mtu aje akuulize Mtume Muhammad alifariki saa ngapi exactly,atakuwa anauliza swali la kijinga sana na kukosa reasoning.
 
Bible and Quran ni vitabu vitakatifu vya Mwenyenzi Mungu
Injili na Quran ndio vitabu vya Mungu.Injli(Gospel)ni yale aliyohubiri Yesu

Biblia sio kitabu cha Mungu,Biblia imeandikwa na watu.zaidi ya 40

Mark,Mathew nk sio waliondika hivyo vitabu,asili mia 70 yaliyoandikwa kwenye Biblia ni maneno ya Paul aka Soul
Kitabu cha Injili kimepotea,hakiko duniani

Pale unaposikia Quran imeshuka kutoka mbinguni haina maana kuwa kartasi zimeteremka kutoka mbinguni

Malaika aitwae Gibril (Gabriel),ndie alikuwa akimpa maneno Muhamad ili ayatangaze kwa wanadamu,Gibril alitumwa na Mungu kutoka mbinguni

kuna vitabu 4 vitakatifu katika hii dini aliyokuja nayo Abraham navyo ni:-Tautat cha Musa,Zabur cha Daud,Injil cha Yesu aka Isa,Furkan(Quran) cha Muhamad

Dini aliyoanzisha Ibrahim ina sera mojo
kama kitabu cha mwanzo(taurat) kinavyosema agano la kale deuteoromy 6:4-14 "oooh wana wa Israe bwana Mungu wetu ni mmoj",

Yesu nae alisema kaama inavyonukuliwa kwenyw Marko 12:29 "ooh wana wa Israeli Bwana Mungu wetu ni mmoja"

Kama anavyonukuliwa Muhammad katika Quran sura ya Ikhlas "Sema Mungu ni mmoja"..

Mungu ni mmoja

Its not that difficult to understand...even a fool can catch that
 
I think ni kundi la watu au mtu mmoja aliyewashinda uwezo wa kufikiri jamii za kipindi hicho hivyo akaamua kuandika kitu ambacho kitamshika kila mtu na kuweka defense ya usihoji chochote au utakuwa unakufuru.
 
Maasikofu Catholic Church wa wakati huo ndiyo walichora hiyo kitabu kutengeneza balance ya kilichokuwa kinaendelea wakati huo.Think,creat then overcome.
 
Maasikofu Catholic Church wa wakati huo ndiyo walichora hiyo kitabu kutengeneza balance ya kilichokuwa kinaendelea wakati huo.Think,creat then overcome.
Ndo maana mimi nimeamua kubaki na mungu moyoni,,
 
Naamini Mungu yupo, na ndo ametujaalia akili na utashi wa kupambanua mambo. Mara zote linapokuja suala la kuhoji origin ya hivi vitabu vitakatifu, viongozi wetu wa dini wanakimbilia neno moja tu, "AMINI", Kwamba tuamini kwamba hivi ni vitabu vitakatifu vya mwenyezi Mungu.

Kwenye biblia tunaambiwa iliandikwa na watu KWA MWONGIZO WA ROHO MTAKATIFU, swali langu ni je? Mimi nikikaa mezani kwangu nikaanza kuandika kitabu, wewe uliyeko jirani yangu utajuaje kwamba ninachoandika ni kwa uwezo wa roho mtakatifu au kwa uwezo wangu mwenyewe. Nikisema kwamba kuna group la watu kwa interest zao, waliamua kuanzisha hiyo project na wakaihalalisha kwa kusema ni neno la Mungu na tuliamini nakosea?

Mimi sio Muislam, hivyo sijui sana kuhusu origin ya Qur'an but, naskia kwamba Qur'an ilishushwa kutoka mbinguni, sijui ni ushahidi gani uliopo wa kuthibitisha hilo au pengine ni dhana ambayo imelalia kwenye imani zaidi. Lakini nikisema kuna watu walitengeneza hayo yote na ili kuyahalalisha wakayaweka chini ya miliki ya Mungu, nitakuwa nakosea.

Tafadhali, usiniambie niamini, nipe sababu za msingi za kwanini nisiamini kuwa biblia na qur'an hazikutengenezwa na kundi flani la watu kwa manufaa yao.





Ndio umeshtuka leo? Nilishagundua kitambo
 
Back
Top Bottom