NAFASI ZA KAZI YAS - DIRECT SALES AGENTS

NAFASI ZA KAZI YAS - DIRECT SALES AGENTS

srinavas

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2011
Posts
4,270
Reaction score
4,182
Habari wakuu,

Kama kichwa kinavyojielezea hapo juu,

Ninahitaji vijana kwa ajili ya kufanya mauzo ya Ku Push products za Yas Business kama Vile Yas Routers, SME and Individual Bundles, Home Fiber, Mjasirianali Box, SME KINARA na zingine nyingi.. Zote hizi ni bidhaa za Yas Business

Ajira hii ni Fursa kwa vijana wachakarikaji ambao wapo tayari kujiendeleza na kukua zaidi kwenye Sales, kwani huku utakutana na watu mbalimbali na mafunzo mbalimbali vitakavyokupelekea wewe kukua zaidi Career wise. Wapo watu wengi wameanzia huku na wapo watu wengi wapo mpaka sasa hvi na wanajipatia kipato kikubwa sana ambacho huwezi kidhania wala kutegemea

Malipo ya kazi hii ni kama ifuatavyo, Transport Allowance (Pesa ya usafiri), Commision na Muda wa Maongezi.

ZINGATIA:
Kazi Hii sio zile za wale Ma Freelancer wanaotembea Barabarani kuuza Laini za Simu. HAPANA,

KAZI HII INAFANYIKA IN A PROFESSIONAL WAY, Unakuwa kama sales Professional kwanzia kwenye kuwatafuta wateja mpaka kuwapata, So ita involve Cold Calls, Appointment Arrangements, Na Namna nyingine kwani wateja wanaotakiwa hapa ni wateja wenye uwezo kama Makampuni au watu wenye uwezo wa kulipia huduma za Postpaid.

Kwa ambao wapo tayari au ambao wana uzoefu zaidi wanaweza kunicheki kupitia namba 0717016789 (Call/Whatsapp) au kupitia Email - norkim1991@gmail.com

Mkinicheki kupitia whatsapp inakuwa bora zaidi

Asanteni sana na karibuni sana wapambanaji tukatengeneze pesa na kujenga Uchumi wetu.
 
Attachments

  • IMG-20251204-WA0000.jpg
    IMG-20251204-WA0000.jpg
    86.5 KB · Views: 22
Weka na allowance ya viatu maana hiyo kazi msako wake wa wateja ni sako kwa bako.
Hii sio ya kutembea barabarani na kwenye Mabaa mkuu. Hii inahitaji mkakati, kwa i wateja wake sio kila mtu anaweza kuwa mteja
 
Hii sio ya kutembea barabarani na kwenye Mabaa mkuu. Hii inahitaji mkakati, kwa i wateja wake sio kila mtu anaweza kuwa mteja
Ukiitwa kwenye fursa wewe ndio fursa......watakuja vijana uwatumie kama ngazi.
 
Mjasiriamali box ndo nini?
Mjasiriamali Box inakuwezesha kama Mjasiriamali, kwa kukupatia mahitaji yote ya mawasiliano kiurahisi kupitia Yas. Kwanzia Internet ya kutosha , Dakika, SMS na kadhalika. Na pia huduma ya kupigiana Bure kwenye kundi lako yaani CUG.

Kwa maelezo zaidi unaweza kunicheki mkuu, namba yangu hiyo hapo
 
Ukiitwa kwenye fursa wewe ndio fursa......watakuja vijana uwatumie kama ngazi.
MKuu kwani wewe huko unapofanyakazi hawakutumii?? Au hapo ulipojiajiri mwenyewe hiyo ajira haikutumii.. Ukiona umeajiriwa popote pale, Kua kwamba wewe ndio Fursa, Na ndio maana unalipwa
 
Kwahiyo kuuza routers hakuhitaji kutembea? Labda kama una ofisi ushawaandalia waje kukaa ila kama unawakabidhi mzigo wakatafute wateja ongea tu ukweli wa mambo sales zozote kwa sasa kutembea kumfuata mteja ni lazima ukikaa wenzio wanamfuata
 
MKuu kwani wewe huko unapofanyakazi hawakutumii?? Au hapo ulipojiajiri mwenyewe hiyo ajira haikutumii.. Ukiona umeajiriwa popote pale, Kua kwamba wewe ndio Fursa, Na ndio maana unalipwa
Ndio Watanzania hao wana roho za kukunja sana mtu unatangaza kazi kwa Vijaya anatokea mtu anakupinga na wala hana msaada wowote kwa hao Vijaya Nchi ina watu makatili sana hiyo sishangai kwa yanayotokea..
Mimi nakushukuru Mkuu ongeza Vijana wengine ukipata nafasi..
 
Kwahiyo kuuza routers hakuhitaji kutembea? Labda kama una ofisi ushawaandalia waje kukaa ila kama unawakabidhi mzigo wakatafute wateja ongea tu ukweli wa mambo sales zozote kwa sasa kutembea kumfuata mteja ni lazima ukikaa wenzio wanamfuata
Kutembea ni sehemu ya kazi unataka mtu apate hela bila kutembea watu wanasinzia kwenye engine za meli na makelele yote yale sembuse kufanya kazi mtaani..
 
Kutembea ni sehemu ya kazi unataka mtu apate hela bila kutembea watu wanasinzia kwenye engine za meli na makelele yote yale sembuse kufanya kazi mtaani..
Sasa mbona unasema hawatatembea mtaani rekebisha ulipoandika uandike tena
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom