Nafasi 50 za kazi ya muda mfupi

HEHEHE....ILA TUTOE PONGEZI KAMA MTANZANIA KAWEZA KUTOA AJIRA KWA VIJANA 50 NDANI YA SIKU 20..NI JAMBO ZURI..KIKUBWA ATAFUTE NAMNA YA KUWAAJIRI PERMANENT NA PIA KUONGEZA MASLAHI YAO BADALA YAKUWATUMIA KAMA TISSUE PAPER.FORM FOUR KUPATA KAZI SIKU HIZI NI BAHATI LABDA ULINZI HUKO..WENYE NYUZI TU WAPO MITAANI WANAUA MBU MWAKA WANNE AU WATANO HUU.KWAHIYO VIJANA CHANGAMKIENI FURSA
 
Developer, Tunaomba feedbacks. Au kama kuna alie-apply akapigiwa simu au kurudishiwa email aje atoe ushuhuda hapa.
Kwa uzoefu wa hapa, siku hizi watu wanaweka tu matangazo mradi wahanga wa ajira watume CV na kuanza kuwatapeli.

Hata watoa matangazo ya ukweli, mkishamaliza usaili au kutimiza idadi ya applicants, ni uungwana kurudi hapa na kuwatangazia wengine ili kuondoa usumbufu kwa waliochelewa.

Hili tangazo nimeliweka ijumaa...

Jumamosi na jumapili unajua ni weekend

Kuanzia kesho muda wowote wiki ijayo kulingana na mipangilio ya kazi nitawajulisha niliowachagua 50 kwa simu.
 
Hallow habarini wakuu,

Tuna nafasi 50 za kazi ya muda mfupi kwa vijana. Kazi hii ni ya kupiga chapa (kuprint) documents. Itafanyika kwa siku 20.

Tunahitaji vijana angalau (at least) waliomaliza kidato cha nne na wenye cheti cha kompyuta (certificate of computer applications).

Kama una cheti, stashahada au shahada na hauko engaged na kazi yoyote kwa sasa pia tunakukaribisha.

Malipo ni sh 9500/= kwa siku bila benefit nyingine yoyote.

Sehemu ya kazi ni maili moja kibaha.

Usafiri wa kutoka ubungo mpaka maili moja utatolewa kwa kila siku ya kazi (Kwenda na kurudi).

Tuma maombi tu kama unaishi dar au kibaha.

Andika barua ya maombi pamoja na CV kwa lugha uipendayo, kiswahili au kiingereza.

Kutuma maombi: printingjobvijana50@gmail.com

Mwisho wa kupokea maombi ni 19/06/2017.

Tuma mapema kwa sababu maombi yatafanyiwa kazi kadri yanavyokuja.

Karibuni.
Je kwa asiye na cheti cha computer lakini anajua kutumia anaweza kupata nafasi?
 
Vipi kama tutakubaliana broo, mie nipo Dodoma lkn niko vizuri sana kwenye computer, Nina laptop binafsi, nipe kazi nikuchapie kisha unitumie changu
 
Mi Nina vijana wangu site, wanalamba 15000 per day na msosi juu hawana hata cheti cha chekechekea iweje hao Wa vyeti uwape 9500!. Acha unyonyaji kwa kisingizio cha uhaba Wa ajira.....
Inshu gani hiyo mkuu tupegawane utajiri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom