Nafanyaje kupata Hati ya Kusafiria (Passport) kwa haraka?

Kila la kheri mkuu. bahati kama hiyo niliwaikuipata mimi , ila kwa upande wangu ilikuwa pande za Australia . Ile familia waliniambi nikitaka barua ya mwaliko niwaambie na hata kazi waliniambia watanitafutia , nikawajibu kwanza sina passport. wakaniuliza kupata passport inagharimu kiasi gani ? nikawajibu si chini ya 150,000 nikatumiwa kama AUD 200 hivi kwa ajiri ya huo mchakato....
kaka ulipata wapi iyo Familia ebu tupeane mchongo kaka
 
Changamkia fursa hiyo mkuu, hapo kwenye 'kitabu' hakuna shida kabisa hakikisha unapata namba ya NIDA kwanza na kama docs nyingine zote zipo basi lishaisha hilo ukiwa na mtu wa kukushika mkono unapata kitabu ndani ya siku tatu, na ukifuata taratibu za kawaida its almost siku 10...
Hiyo ya Germany tabu yake nini mkuu?
 
Tafta kitambulisho cha taifa passport now ni km kusukuma mlevi km auna kitambulisho sema nikuelekeze njia nyepesi na ya haraka vinginevyo utakaa sana.
Mkuu.. mimi nilikwenda uhamiaji, na doc's zote zinazohitaka, wakanichukua fingerprints na nikalipia kila kitu..

sasa bado nipo ndani ya siku 14 nilizoambiwa kusubiri, ombi langu limetumwa Dar.. ila nina hofu kweli kweli..
nahofia kuchinjiwa baharini.
na hii ni mara yangu ya kwanza kuomba paspoti.

Kwani kwa uzoefu wako, ni kipengere kipi ukishakivuka unakuwa na uhakika 99% wa kupata pasipot?.

Nisaidie maelezo kidogo, sometimes nakoswa hadi usingizi.
 
Kama kuna mapungufu yoyote au wanahitaji nyongeza watakupigia simu siuliweka mawasiliano yako
 
Wadau wa JF salamu kwenu.

Moja kwa moja kwenye swali, je ni utaratibu gani lazima niufuate ili kupata passport?

Nataka kufahamu

1. Vigezo vinavyohitajika
2. Aina za passport
3. Miongozo na taratibu (terms and conditions) ya kuifuata
4. Mchanganuo wa gharama mpaka naipata na muda.
Naomba kuwasilisha.
 
Katika idara inahitaji utumbuzi Basi ni uhamiaji,, jamaa wanapenda rushwa balaa,

Niliwanyima rushwa zote waliniweka miezi 2 na nusu ndipo kunipa passport

Gharama za kulipia serikalini ni 150,000, ila kuna gharama za nauli kuzungukia ofisi zao kama uko wilayani nauli itaongezeka, printing na mwanasheria,

Vigezo vya muhitaji wa passport kutegemea na aina ya safari yake viko ofisi za uhamiaji, fika kwenye ofisi zao,

vigezo vinatofautiana kutokana na aina za safari
 
Nenda uhamiaji utapata taratibu huko , wanaishirkisha na NIDA ili wajiridhishe uraia wako.

Odhis *
 
Mkuu.. mimi nilikwenda uhamiaji, na doc's zote zinazohitaka, wakanichukua fingerprints na nikalipia kila kitu..

sasa bado nipo ndani ya siku 14 nilizoambiwa kusubiri, ombi langu limetumwa Dar.. ila nina hofu kweli kweli..
nahofia kuchinjiwa baharini.
na hii ni mara yangu ya kwanza kuomba paspoti.

Kwani kwa uzoefu wako, ni kipengere kipi ukishakivuka unakuwa na uhakika 99% wa kupata pasipot?.

Nisaidie maelezo kidogo, sometimes nakoswa hadi usingizi.
Ulifanikiwa mkuu??
 
Back
Top Bottom