Msaada: Namna ya kupata hati ya kusafiria (passport)

Diwani

JF-Expert Member
Oct 25, 2014
2,672
2,697
Habari ya muda huu wa kuu, nina ugeni kidogo na hatua za kufuata kupata hati ya kusafiria. Naomba anayejua anisaidie mimi na wenzangu tusiojua ABC za namna ya kupata passport.

NB; daraja lolote.

Natanguliza shukrani.
 
Kama unaenda nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Msumbiji, Malawi, Burundi, Zambia au DRC lala tu kesho amka na kitambulisho chako na elfu 15,000 na 5000 ya kumpoza anayekushughulikia hapo uhamiaji na utapewa kesho hiyo hiyo. Ila kama unaenda tofauti na nchi hizo taratibu na kalenda utazikuta migration
 
Kwanza fuata ushauri wa Ng'wanapagi hapo juu.

Hakikisha una kitambulisho cha taifa (NIDA) au ile namba.

Ingia kwenye tovuti ya uhsmiaji, nenda sehem ya kujaza form za maombi ukikamilisha utalipia malipo ya awali na kuprint application yako utakayowasilisha uhamiaji na kulipia 140,000/- kama sikosei.

Hakikisha nyaraka za vyeti vya kuzaliwa zako na wazazi unazo soft copy.

Ukiona mzunguko mrefu, nenda kwenye steshenari zozote karibu na ofisi za uhamisji watakufsnyia huo mchakato wa awamu ya kwanza na huenda wakakuunganisha na watu wa kukupatia msaada zaidi uhamiaji kupata hati upesi.

Barikiwa
 
Nashukuru
 
Kama huna pesa za kubrashia viatu kama ki laki moja na tuelfu hamsini kaa nyumbani kwa kutulia
Kama ana kila kitu kinachohitajika wakati wa kujaza fomu ya kuombea passport wala hahitaji kutoa hela, atapewa tu passport yake bila shida
Aandike barua ya maombi ya passport,
Ajaze fomu vizuri,
Aambatanishe vitu vyote vinavyohitajika basi.
 
Back
Top Bottom