Naendelea vizuri baada ya kuonesha dalili zote Covid 19

Naendelea vizuri baada ya kuonesha dalili zote Covid 19

Midazolam

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
807
Reaction score
1,349
Naomba nilete kwenu haya maumivu, tujiadhari Watanzania.

Nimekuwa ni miongoni wa watu wanaohudumia Watanzania wenye matatizo ya upumuaji, na kila kazi inachangamoto wake.

Baada ya kujiona siko sawa na kuanza kujisikia vibaya niliomba siku za kupunzika kidogo, nyumbani naishi peke yangu japo nina majirani pembeni, kwa hiyo nimejitenga kwa mda tu ndani.

Kikubwa ambacho naona kimenisaidia sana ni mtindo wangu wa mazoezi, nafanya sana mazoezi, huwa nabeba vitu vizito, wazee wa gym wanafahamu.

Na huu ugonjwa ukikukamata ni vizuri usilale sana ndani kama unaona unafuu fulani, humo humo ndani fanya mazoezi. Piga sana push up za uhakika, ili kuruhusu mfumo wa hewa kupenya vizuri.

Kunywa sana maji ya moto, changanya tangawizi, kula limao, machungwa, ndizi, nanasi, kitunguu swaumu + kitunguu maji

Na usisahau imani yako kwa Mungu.

Kiukweli naendelea vizuri. Kesho napanga kurudi mzigoni nikaendelee kupambana zaidi kwa wengine.

Muhimu: Barakoa ni muhimu vaaa
 
Pole! mimi nauguza mtu ambaye nahisi ni hiyo kitu! je unashauri nini ili yasinikute!
 
Mitano Tena si mnasema covid 19 haipo Sasa tuvae chupi za nn
Labda hujaelewa nani amesema covid 19 haipo we huoni hadi Leo hi wazungu hawajai uwanjani kuangalia mpira? Maana yake ni kwamba covid 19
 
Two weeks ago nilipitia hali isiyo ya kawaida, niliamka kichwa kinanigonga sana kila nikijaribu kusimama nilihisi kupepesuka. Nilimeza panadol na kuingia zangu town posta ofisini, nilifika ofisn mwili na viungo vingine vya mwili vinauma sana, hivyo nikaamua kurudi tena home kupumzika.

Kama unavyojua maisha ya dsm... Majirani wapo ila hakuna mwenye habari na wewe kila mtu yupo busy na maisha yake... Nakumbuka mchana wa siku hyo niliumwa sana ndani.. sikua na msaada coz naishi peke yangu. Bahati nzuri mpenzi wangu aishiye Morogoro alinipigia kunijulia hali, alivyonisikia tu the way nilivyokua naongea alijua something wrong hivyo akaomba ruhusa job kwao na kupandisha dar... Alifika usiku sana akiwa na machungwa,limao, tangawizi nk..

Namshukuru mungu naendelea vizuri, japo sikuenda hospitali ku cheki ila dalili zote zilikua ni covid 19...

Ukweli usio na shaka hii kitu imerudi na tuhimizane wenyewe kujilinda na kuchukua hatua.. si lazima kubaki kuilaumu serikali sababu hata watu wanaongoza serikali wanaweza kuugua... Najaribu kufikiria tu serikali itakua na nia ya kupunguza tension ya watu, maana muda mwingine uoga ndio mbaya kuliko ugonjwa wenyewe

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom