GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,553
- 108,889
Kwa Ufisadi na Uhujumu Uchumi huu wa hawa akina Harbinder Seth na James Rugemalira ambao kimsingi ulitokea wakati wa awamu ya nne ( 4 ) sasa nimeshapata jawabu langu la kwanini Wabunge wengi wa Bunge la JMT ( wengi wao kabisa 99.9% wakiwa kutoka CCM ) walimshangilia sana Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ( 4 )Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipoenda Bungeni kushuhudia Kuapishwa kwa Mkewe Mama Salma Kikwete kuwa Mbunge.
Nimshukuru tu sana Mwenyezi Mungu kwa kutuletea Kiongozi Shupavu na Jemedari kabisa Rais wa sasa wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na nitazidi kumuombea kila uchao kwani anafanya kile ambacho Watanzania Wazalendo tulikitaka kwa muda mrefu na Watanzania tutamkumbuka daima.
Mwisho niwaombeni tu Wabunge wa JMT hasa wale mliokuwa mkimshangilia JK pale Bungeni kutuomba radhi Watanzania kwani inaonekana kama vile ile shangilia yenu ilikuwa ni ya kubariki Vitendo hivi vya Kifisadi na ambavyo kimsingi vimeigharimu mno nchi huku Watanzania wengi wakiwa bado taabani Kiuchumi na maisha yao ni magumu kupitiliza.
Nawasilisha.