Nadhani sasa ni wakati muafaka Wabunge waliomshangilia JK Bungeni kutuomba radhi Watanzania

Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
Kwa Ufisadi na Uhujumu Uchumi huu wa hawa akina Harbinder Seth na James Rugemalira ambao kimsingi ulitokea wakati wa awamu ya nne ( 4 ) sasa nimeshapata jawabu langu la kwanini Wabunge wengi wa Bunge la JMT ( wengi wao kabisa 99.9% wakiwa kutoka CCM ) walimshangilia sana Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ( 4 )Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipoenda Bungeni kushuhudia Kuapishwa kwa Mkewe Mama Salma Kikwete kuwa Mbunge.

Nimshukuru tu sana Mwenyezi Mungu kwa kutuletea Kiongozi Shupavu na Jemedari kabisa Rais wa sasa wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na nitazidi kumuombea kila uchao kwani anafanya kile ambacho Watanzania Wazalendo tulikitaka kwa muda mrefu na Watanzania tutamkumbuka daima.

Mwisho niwaombeni tu Wabunge wa JMT hasa wale mliokuwa mkimshangilia JK pale Bungeni kutuomba radhi Watanzania kwani inaonekana kama vile ile shangilia yenu ilikuwa ni ya kubariki Vitendo hivi vya Kifisadi na ambavyo kimsingi vimeigharimu mno nchi huku Watanzania wengi wakiwa bado taabani Kiuchumi na maisha yao ni magumu kupitiliza.


Nawasilisha.
 

Ombudsman

JF-Expert Member
Apr 18, 2012
3,572
2,000
bfa784630d29788901b8db2cc85b412b.jpg
 

fungi

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,536
2,000
Double standard
Wapinzani
"Wabunge kumshangilia kikwete ni ishara mbaya kwa Magufuli watu hali imekuwa mbaya watu wame mmiss Kikwete"
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,408
2,000
sio ccm hata wapinzani waliimba wana imani na Mkapa na Kikwete bungeni halafu leo wanapiga makelele waondolewe kinga
hapa ndipo palipo na alama nyekundu!
walikuwa wakishupaa mpk misuli ya shingo inatutumka hlf leo wamekuwa wazuri tena wakuaminiwa!!!
sina shaka hata huyu akijaondoka watasema wanaimani nae.... sijui wanaonyesha madudu gani haya! naona wanajiimbisha nyimbo za ccm bila kupenda ha ha ha! kwisha hbr.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom