NACTE yabadilishwa jina, sasa kujulikana kama NACTVET

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Baraza la Taifa na Elimu ya ufundi (NACTE), sasa limebadilishwa jina na litajulikana kama Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (NACTVET), mabadiliko hayo yamefanywa kufuatia Bunge kufanya mabadiliko mbalimbali ya Sheria ikiwemo Sheria namba 4 ya 2021.

Mabadiliko hayo madogo yameliongezea Baraza jukumu la urekebu na udhibiti wa mafunzo ya ufundi stadi ambayo awali yalikuwa yakifanyika chini ya mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya ufundi stadi (VETA)

Shabaha ya marekebisho haya ni kuongeza ufanisi katika usimamizi, urekebu na udhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa hapa nchini.


Kufuatia marekebisho ya sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte), jina la baraza hilo kwa sasa limebadilishwa na kuwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NactVet).

Mabadiliko hayo ya sheria yameliongezea baraza hilo jukumu la urekebu na uthibiti ubora wa mafunzo ya ufundi stadi ambayo hapo awali yalikuwa yakifanyika chini ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta).

Taarifa iliyotolewa leo Februari 22 na Katibu Mtendaji wa NactVet Dk Adolf Rutayuga inaeleza kuwa mabadiliko hayo yanalenga kuongeza ufanisi.

Amesema shabaha ya marekebisho hayo ni kuongeza ufanisi, urekebu na uthibiti ubora wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa nchini.

“Kwa mabadiliko haya ya sheria jukumu la urekebu na udhibiti ubora wa mafunzo ya ufundi stadi yamehamishiwa rasmi kutoka Veta hadi NactVet,” alisema Dk Rutayuga

Kufuatia hilo alisema maombi ya usajili wa vyuo, vituo na mafunzo ya ufundi stadi yanatakiwa kuwasilishwa NactVet ambako majukumu yamehamishiwa.

Katika hatua nyingine baraza hilo limetoa wito kwa vyuo na vituo vyote vilivyosajiliwa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kuendelea kuendesha mafunzo hayo kwa mujibu wa sheria.

“Baraza litaendelea kushirikiana na wadau ikiwa ni pamoja na vyuo katika kuendeleza na kukuza utoaji wa elinh bora kwa ajili ya maendeleo ya taifa,”.
 
Nilishazoea NACTE sasa itabidi nizoee jina jipya, halitaki papara wakati wa kulitamka sharti uwe ume rilax.
 
Baraza la Taifa na Elimu ya ufundi (NACTE), sasa limebadilishwa jina na litajulikana kama Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (NACTVET), mabadiliko hayo yamefanywa kufuatia Bunge kufanya mabadiliko mbalimbali ya Sheria ikiwemo Sheria namba 4 ya 2021...
Aisee!
 
Daah kwa hiyo VETA nayo wameibebeshwa? Niliwahi kuongea na jamaa zangu ambao ni walimu wa VETA kiukweli hili jambo haeakuliafiki na waliniambia ndiyo mwisho wa utendaji bora wa hivi vyuo. Mimi nilikubaliana nao kwa sababu wamejiongezea mzigo tuu...
 
Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi> Hii mbona ina mkanganyiko? Labda wabadili tena ili ilete maana inayoeleweka vizuri. Maana hapa inasomeka ni vitu viwili tofauti vyenye maana sawa. Sasa tofauti yake ipo wapi kati ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi?
 
Ndiyo litaleta ubora kwenye elimu au ndiyo kuzorotesha Tu elimu!
Hii nchi inachoshaa
kusema ukweli nacte pale ndani hawana kazi so wanajalibu kushika kila tawi linakatika yani kama vile kifo cha nyani miti yote huteleza kuna kipindi wakachukua kazi ya vyuo ya usajili wa wanafunzi ili wapate hela ya fomu hawa jamaa janja janja sana hawana creativity mule
 
Kubadilisha majina haina maana kuna mabadiliko ndani yake, wasipoangalia bado watabadilisha majina bila kuwepo na manufaa yoyote.
 
Back
Top Bottom