Multi-skilled
JF-Expert Member
- Mar 1, 2023
- 802
- 3,048
Umasikini mbaya sana nimekulia kwenye umasikini uswahilini ambako wizi, uchawi, umbea, uvivu, umalaya, uhalifu roho mbaya, chuki n.k ni vitu vya kawaida sana. Huko shule si kipaumbele na watu wanaamini mtoto akiwa hana akili hata akienda shule ni kazi bure, wanaamini utajiri ni bahati na uchawi kwa mtu ambaye hajawahi kuishi huko anaweza kupata shida sana.
Lakini Sisi tuliozaliwa huko tuliona ni maisha mazuri na tumepewa na Mungu na yeye ndiye apangaye nani ampe ushua nani asimpe.
Baada ya kutembea na kupata exposure nchi mbali mbali na mikoa tofauti nimekuja kugundua kuwa Umasikini ni kitu kibaya sana ambacho natakiwa kukikataa kwa namna yoyote ile, tangu nimearealize hilo naitumikisha akili na mwili wangu kwa bidii sana ili kizazi changu kijacho kisionje ladha ya umasikini.
Pia umasikini sio sifa hakuna raha yoyote ya kuwa masikini au mnyonge, hakuna raha yoyote ya kuchukia matajiri na kuona kuwa ni wachawi, hakuna raha yoyote kwenye kukosa huduma nzuri za afya, makazi mazuri na kukosa pesa.
Inawezekana ni kweli Pesa hainunui furaha lakini Umasikini unanunua nini ndugu zangu?
Tuukatae umasikini.