Nabii wa Afrika Kusini Atabiri kifo kwa kiongozi wa kisiasa Tanzania

Huyo prophet anasema kiongozi wa upinzani Tanzania mwenye mwele nyeupe ananyemelewa na mauti.

Akauliza jina la kiongozi mwenye nywele nyeupe akaambiwa anaitwa Lowassa. Akasema whatever his name is anamwombea na balaa la mshituko wa moyo ambao unaweza sababisha kifo.

Pia emeendelea kusema kuna kiongozi hapo kwa Madiba atajiua. Anawaombea wote hayo mabalaa yawapite mbali.

Teh teh teh..

Mimi kinachanishangaza kwanini hawaonyeshwi mambo mazuri wao wanajua kutabiri kuhusu ugonjwa na vifo tu?

Au ndiyo mbinu anataka Lowassa amfuate?

Haya mambo ya dini sometimes hayana tofauti na watumiaji wa opium
 
Ahaa wapi lowasa analindwa na mungu, watu wamemita jeneza, vitoto vidogo vimemuita marehemu siku hizi anakutana navyo wala hana noma,

lowasa atakufa wakati wake ukifika humu jf watu walinadi ugonjwaaaa mpaka wakapauka lowasa bado anapumua, wacha mungu aitwe mungu
 
Jamaa hajatabiri kuwa Lowassa atakufa, ila amemuombea asife, maana ameona roho ya kifo ikimuandama.

Hii kwenye ulimwengu wa kiroho ni kitu cha kawaida sana kwa mtu wa maombi.

Kuna miaka kabla akili za kimadenge hazijanivamia nilikuwa mtu wa kupenda sana maombi niliwahi kuota jirani yangu mama mmoja mtu mzima analiletea sinia la chakula mchana akiwa amevaa kilemba huku ndani ya chakula kachanganya unga unga fulani hivi kutoka kwa mganga wa kienyeji na nikala kile chakula na kweli nilikufa.

Huyu mama alikuwa mshirikina sana na alikuwa anasemwa semwa sana mitaani, ila kwa kuwa nilikuwa bachelor na mtu niliyekuwa napenda penda sana utani na yule mama alikuwa mchangamfu, nilitokea tu kupatana naye bila sababu ya msingi.

Ndani ya wiki hiyo hiyo siku moja nimo ndani nasoma soma mambo mitandaoni ghafla yule mama akapiga hodi mbele ya mlango wangu na sinia lake la chakula mchana kweupe akiwa amevaa kilemba kile kile na mpangilio wa sahani ule ule na vibakuli vya mboga kama nilivyomuota kwenye ndoto, akiniletea chakula ambacho nilikuwa hata sijamuomba nafikiri kwa sababu nilikuwa bachelor na nilikuwa sinaga ratiba ya kupika mchana ali-take advantage ya hilo.

Nilichokifanya nikachukua lile sinia la chakula nikamshukuru yule mama na kuingia nalo ndani, chakula na mboga nikavimwaga kwenye ndoo nikafunika nikapiga maombi ya nguvu na kumshukuru Mungu halafu nikasubiri mpaka usiku watu wamelala nikaenda kukimwaga jalalani.

Asubuhi narudi kumrudishia vyombo vyake yule mama akabaki anatetemeka tu anaogopa hata kuniangalia usoni, baada ya siku kama 4 hivi yule mama alihama pale mtaani na hajulikani alikimbilia wapi.

Haya mambo ya kuona roho ya kifo ni kitu cha kawaida sana ukiwa mtu wa sala, ila haina maana kuwa tayari ushakufa, ni onyo tu kwenye ulimwengu wa roho kuwa kuna tatizo mahali shughulika nalo.
Ni kweli kabisa mkuu!
Hii nayo huwa ikoje?
Mi wakati mwingine huwa inatokea naota ndugu wa karibu amefariki lakini nikiota hivyo huwa haimaanishi kuwa ndio kweli huyo niliyemuota kafariki badala yake kesho yake lazima nipewe taarifa za mtu wa mtaa wa kwetu au mtu ninayemfahamu kwa ukaribu kuwa amefariki. Hii imekuwa ikitokea mara kadhaa na kila nikiota kuna mtu kafariki nikiamka kesho yake na kupiga simu nyumbani lazima anakuwepo mtu ninayemfahamu amefariki usiku huo!

Iliyonishitua zaidi ni hii, kuna siku niliota mzee wangu amefariki nikaanza kulia ndotoni nilipostuka nikajikuta machozi yananitiririka. Niliogopa sana ilikuwa kama saa nane usiku mda huo huo nikampigia simu mzee akapokea simu yangu lakini naye alipokea kwa wasi wasi kweli maana sijawahi kupiga simu usiku wa manane hivyo. Alipopokea simu akaanza kuniuliza maswali ambayo niligundua amepokea kwa hofu sana nami nilimuuliza wazima wote nyumbani akasema wote wazima basi nikamwambia nilikuwa nimewakumbuka sana akanisisitiza kuwa ni wazima nisiwe na wasiwasi. Kesho yake mchana akanipigia simu kuwa kuna mtu wa mtaa wetu amefariki usiku wa kuamkia siku hiyo!

Mara nyingi vifo vya watu wa maeneo ya nyumbani au ninaowafahamu hata kabla sijafahamishwa huwa ninakuwa nimeota kuna mtu amefariki ila kujua ni nani hapo ndio sijawahi kuoneshwa moja kwa moja.

Siku ya krismasi mwaka uliopita nayo niliota kuna mtu amefariki kesho yake kweli nikapata taarifa classmate wangu alipata ajali ya gari na kufariki papo hapo!
 
Ukiona unamchukia mtu hadi kumuombea kifo ujue tayari umeua moyoni ...katubu ...binadamu wote wabaya kwa wazuri ni watoto wa Mungu ....wabaya leo wengine ndio watakatifu kesho ...Mungu angekuwa na ubaguzi tulionao binadamu ....jua na mvua vingewagusa watakatifu tu ....tuombeane badala ya kuchukiana tena sababu za siasa ....chukia uovu wa mtu na si mtu ....
 
Katika MANABII hawa ndani ya MAKANISA haya kunamengi sana.

Naomba kuweka kumbukumbu sawa, hapa kwetu "BONGO" kuna mchungaji mmoja alimtabilia Mh Lowassa kua atalua Rais lakini Rais ni Mh Magufuli.....

Kazi kweli kweli.
 
Tb jushua alitabili atakuwa rais huyu anatabili kifo je Mungu huyu huyu mmoja ndo anapanga?
 
Jamaa hajatabiri kuwa Lowassa atakufa, ila amemuombea asife, maana ameona roho ya kifo ikimuandama.

Hii kwenye ulimwengu wa kiroho ni kitu cha kawaida sana kwa mtu wa maombi.

Kuna miaka kabla akili za kimadenge hazijanivamia nilikuwa mtu wa kupenda sana maombi niliwahi kuota jirani yangu mama mmoja mtu mzima analiletea sinia la chakula mchana akiwa amevaa kilemba huku ndani ya chakula kachanganya unga unga fulani hivi kutoka kwa mganga wa kienyeji na nikala kile chakula na kweli nilikufa.

Huyu mama alikuwa mshirikina sana na alikuwa anasemwa semwa sana mitaani, ila kwa kuwa nilikuwa bachelor na mtu niliyekuwa napenda penda sana utani na yule mama alikuwa mchangamfu, nilitokea tu kupatana naye bila sababu ya msingi.

Ndani ya wiki hiyo hiyo siku moja nimo ndani nasoma soma mambo mitandaoni ghafla yule mama akapiga hodi mbele ya mlango wangu na sinia lake la chakula mchana kweupe akiwa amevaa kilemba kile kile na mpangilio wa sahani ule ule na vibakuli vya mboga kama nilivyomuota kwenye ndoto, akiniletea chakula ambacho nilikuwa hata sijamuomba nafikiri kwa sababu nilikuwa bachelor na nilikuwa sinaga ratiba ya kupika mchana ali-take advantage ya hilo.

Nilichokifanya nikachukua lile sinia la chakula nikamshukuru yule mama na kuingia nalo ndani, chakula na mboga nikavimwaga kwenye ndoo nikafunika nikapiga maombi ya nguvu na kumshukuru Mungu halafu nikasubiri mpaka usiku watu wamelala nikaenda kukimwaga jalalani.

Asubuhi narudi kumrudishia vyombo vyake yule mama akabaki anatetemeka tu anaogopa hata kuniangalia usoni, baada ya siku kama 4 hivi yule mama alihama pale mtaani na hajulikani alikimbilia wapi.

Haya mambo ya kuona roho ya kifo ni kitu cha kawaida sana ukiwa mtu wa sala, ila haina maana kuwa tayari ushakufa, ni onyo tu kwenye ulimwengu wa roho kuwa kuna tatizo mahali shughulika nalo.
wangapi wanakufa kila siku ya mungu?!
 
Nimekuelewa vyema, lakini mambo ya ulimwengu wa roho kwa mtu mwenye imani ya Kikristo sio ya kutafutia kiki. Alikuwa na haja gani kuyatangaza? Wachungaji wa kweli hawawaambii watu mambo ya kuwatia hofu.
 
Mwanzo nilistuka lakini baada ya kugundua kwamba ni Nabii wa Afrika ya Kusini, sikusumbuka tena. Angekuwa Nabii wa Mungu ningemwelewa!
 
Kulikuwa na mada humu mdau mmoja ameileta lkn nadhani Moderator ameiondoa.
Sjui km kulikuwa na tatizo (moderator atanisaidia) ..
Niende direct..
Je mpango wa kumuua Tundu Lissu ilikuwa ni plan B ya ule utabiri wa Prophet Bushiri uliokuwa criticized na Askofu Gwajima?
Wadau tuendelee kuliangalia hili swala kwa jicho la tatu
 
Huyu mdau..
sijui nae amekula maharage ya wapii..
Alichokiandika hata yeye akielewii..bure kabisa
 
Atakufa au atauwawa? Akifa au akiuwawa then what? Mbona utabiri ulikuwa haujajitosheleza? Au mnashindwa kuuelezea vizuri?
 
ungeuweka kwani sio wote tunaoujua
Prophet Bushiri alitabiri kuwa Rais Magufuli atauawa kabla ya kumaliza muhula wake wa kwanza..
Askofu Gwajima akau' criticize utabiri huo na kwenda mbali zaidi akisema alietoa utabiri huo ni nabii wa shetani anaetumiwa na watu wanaopanga kumuua Rais ili baadae wamuue Mh Lowassa ionekane kwamba watu wa Lowassa ndio walimuua Magufuli kisha watu wa Magufuli wakalipiza kisasi wakamuua Lowassa ili hao watu wa Bushiri wasimike serikali wanayoitaka wao inayofavor mabepari..
 
Ni sawa Mkuu, ingawa mimi nilisikia tofauti kidogo, kwenye nani ataanza kufa!
 
Back
Top Bottom