Kifo ni fundisho kubwa kwetu sisi tulio hai

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,160
7,734
Apumzike kwa amani Waziri wetu Mkuu Edward Lowasa, hakika ni kiongozi aliyependwa na kila rika kwa uhodari wake wa kuchapa kazi.

Kwetu sisi tulio hai haswa viongozi walio pewa dhamana katika nafasi mbalimbali, fanyeni kazi kwa kutanguliza masilahi ya wananchi, tatueni kero za wananchi ili siku mkitangulia mbele za Mungu basi watakao baki hai wakusimulie kwa mambo mazuri.

Kuna viongozi JEURI, VIBURI, wananyanyasa walio chini, wabadhirifu, wazinzi na kuwadhalilisha wasio na uwezo. Tuache hayo mambo.

Kifo kipo, tenda mema kwa binaadamu wenzako, huwezi kuzikwa na Cheo chako. Ukifa kila kitu kinaishia hapohapo.
kamwe huwezi kuzikwa na vyeo ulivyo tunukiwa hapa duniani bali mambo mema ulio watendea binaadamu wenzako ndio yatakusaidia mbele za mungu.
 
Binaadamu tunajisahau sana. Mtu akiwa na cheo au uwezo wa kifedha anakuwa Jeuri, Kiburi na Maringo yasiyo na mfano kama vile hawezi kufa.
Tuache jeuri, kiburi, ubadhirifu wa mali za umma, tutende haki kwa binaadamu wenzetu.
 
Watakuelewa wachache sana
wenye hofu ya mungu. tatizo viongozi wetu wengi hawana hofu ya mungu. hawajali wala hawana cha kujifunza wanapo hudhuria misiba na kuwazika watu walio kuwa nao. wakitoka misibani/kuzika wao wanaendeleza wizi, jeuri, viburi na maringo....kama vile wao hatakufa!!.....
 
wenye hofu ya mungu. tatizo viongozi wetu wengi hawana hofu ya mungu. hawajali wala hawana cha kujifunza wanapo hudhuria misiba na kuwazika watu walio kuwa nao. wakitoka misibani/kuzika wao wanaendeleza wizi, jeuri, viburi na maringo....kama vile wao hatakufa!!.....
Kiufupi hawajawahi jali mkuu
 
Ninawapa pole sana wanafamilia wote, pia, na Taifa zima la Tanzania. huyu alikuwa PM wetu, Mungu alimtumia maeneo mengi kuijenga nchi yetu.

Naungana nawe, kifo ni somo kubwa kwetu sisi tulio hai, ni mtihani mkubwa sana, wapo wanaofeli na wapo wanaofaulu. kufeli au kufaulu kunategemea wapi utaelekea baada ya kifo. Where are you going to spend your eternity? kuna maeneo mawili tu, aidha UZIMA WA MILELE au MOTO WA MILELE. this is real na inaogofya. maamuzi yako unayoyachukua hapa duniani, ndiyo yatakayokupeleka utakapostahili, Mungu hadhihakiwi na Mungu ni wa haki atampa kila mtu anachostahili, bila kujalisha ulikuwa nani hapa duniani.

Marko 8:36 Yesu aliwafundisha kwamba, Kwani itamfaidia nini mtu kuupata ulimwengu wote, akapata hasara ya nafsi yake katika moto wa milele, au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake (ili isiangamie baada ya kifo)? hii ndio theme ya huo mstari. pia,

Ufunuo 14:13 imeandikwa, Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sana. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

Yohana 14:6 Yesu alithibitisha kwamba, Mimi ndimi njia kweli na uzima, mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi.
Yesu alifanyika kafara la dhambi zetu alimwaga damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi, ukitubu leo atakusamehe dhambi zako zote, utahesabiwa haki na hata ukifa aidha kwa ajali au ugonjwa (ambako hakupigi hodi, hatujui siku wala saa) utapata thawabu ya kuepuka moto wa milele, utaenda uzima wa milele. nakuasa, okoka leo, mpe Yesu maisha yako ili kufa kwako kuwe na faida.

ni hatari kufa bila Mungu. nanyi nyote wenye masumbufu ya dunia, Yesu alikufa kwa ajili yenu, kaa chini, tafakari, kwanini watu wanasema ukiokoka utakombolewa, chukua hatua, jaribu, ukiona wokovu haujakusaidia basi, ila umeshajaribu, isijekuwa hata kujaribu hutaki kumbe huko ndiko kwenye ukombozi wako. Mungu awasaidie.
 
Ishi na Fanya matendo ya kupendeza Mungu kaburini utakuwa mwenyewe Hawa wanadam wakisha zika Wana sepa binadam hawana shukran
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom