Nabii wa Afrika Kusini Atabiri kifo kwa kiongozi wa kisiasa Tanzania

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,775
2,400
Hakika huyu nabii aliyemtabiria Lowassa kifo nitafunga na kuomba Mungu amchukue yeye na kizazi chake.

Mwenye uwezo ni Mungu pekee.

Jamaa hajatabiri kuwa Lowassa atakufa, ila amemuombea asife, maana ameona roho ya kifo ikimuandama.

Hii kwenye ulimwengu wa kiroho ni kitu cha kawaida sana kwa mtu wa maombi.

Kuna miaka kabla akili za kimadenge hazijanivamia nilikuwa mtu wa kupenda sana maombi niliwahi kuota jirani yangu mama mmoja mtu mzima analiletea sinia la chakula mchana akiwa amevaa kilemba huku ndani ya chakula kachanganya unga unga fulani hivi kutoka kwa mganga wa kienyeji na nikala kile chakula na kweli nilikufa.

Huyu mama alikuwa mshirikina sana na alikuwa anasemwa semwa sana mitaani, ila kwa kuwa nilikuwa bachelor na mtu niliyekuwa napenda penda sana utani na yule mama alikuwa mchangamfu, nilitokea tu kupatana naye bila sababu ya msingi.

Ndani ya wiki hiyo hiyo siku moja nimo ndani nasoma soma mambo mitandaoni ghafla yule mama akapiga hodi mbele ya mlango wangu na sinia lake la chakula mchana kweupe akiwa amevaa kilemba kile kile na mpangilio wa sahani ule ule na vibakuli vya mboga kama nilivyomuota kwenye ndoto, akiniletea chakula ambacho nilikuwa hata sijamuomba nafikiri kwa sababu nilikuwa bachelor na nilikuwa sinaga ratiba ya kupika mchana ali-take advantage ya hilo.

Nilichokifanya nikachukua lile sinia la chakula nikamshukuru yule mama na kuingia nalo ndani, chakula na mboga nikavimwaga kwenye ndoo nikafunika nikapiga maombi ya nguvu na kumshukuru Mungu halafu nikasubiri mpaka usiku watu wamelala nikaenda kukimwaga jalalani.

Asubuhi narudi kumrudishia vyombo vyake yule mama akabaki anatetemeka tu anaogopa hata kuniangalia usoni, baada ya siku kama 4 hivi yule mama alihama pale mtaani na hajulikani alikimbilia wapi.

Haya mambo ya kuona roho ya kifo ni kitu cha kawaida sana ukiwa mtu wa sala, ila haina maana kuwa tayari ushakufa, ni onyo tu kwenye ulimwengu wa roho kuwa kuna tatizo mahali shughulika nalo.
 
Ameshamuombea rehema na nyongeza ya siku zake. Kuoneshwa kifo ni kitu ya kawaida kabisa. Mbona yule mwingine alisema kuwa kuna kiongozi mkubwa Tz atakufa mwaka huu hamkunung'unika?? Huyu kaoneshwa, lakini amemuombea
 
Lakini ukimya wa lowassa unatisha sana,unanikumbusha alivyokuwa jk,tuendelee kumpiga mawe tuone uwezo wake wa mwisho.
 
Hakika huyu nabii aliyemtabiria Lowassa kifo nitafunga na kuomba Mungu amchukue yeye na kizazi chake.

Mwenye uwezo ni Mungu pekee.

Tatizo lako hujui maana ya unabii. Unadhani unabii unatoka kwa utashi wa mtabiri kama vile mchawi anavyoweza kuamua kufanya influence katika maisha ya mtu.

Ulitakiwa ujue kwanza maana ya unabii, halafu ufahamu nabii anafanya uanbii kwa kutumia nguvu gani, malengo ya unabii na uzuri wa unabii.

Nabii kutabiri kifo cha mtu, haina maana yeye anamtakia mtu huyo kifo. Kama huna maarifa unatakiwa kukaa kimya na kujifunza kabla halijakupata baya usilolijua.

Ufunge na kuomba nabii afe na kizazi chake, kwa sababu amesema yale Mungu aliyosema naye? Kizazi chake kimekukosea nini?

Mwenye Uwezo ni Mungu, kwani nabii anapewa na nani karama ya unabii?

Ujinga wako utakuangamiza. Chukua hatua haraka kabla hujaangamiza uzao wako na wewe mwenyewe. Usidhani kila mahali ni siasa na propaganda!. Nimekuambia wala sikutanii. Usipochukua hatua mara moja, utaona yatakayokupata lakini usije ukasema hukujua.
 
Huyu mjinga na shetani kama ameoneshwa kifo kwanini asimfate mzee mwenyewe amwambie bwana kamuonesha hivi hivo basi atengeneze njia zake vizuri yeye anakimbilia kwenye media kama siyo uwendawazimu ni nini hiki

Nabii Ezekiel alioneshwa mfalme Ezekiel atakufa akamfata private akamwambia sasa huyu Nabii gani anae expose public mambo ya eternity
Na namuomba Mungu mwezi huu ufe kabla haujaisha umedharirisha unabii Nabii wa uongo wewe
 
Mkuu usinitishe hata kidogo

Nabii ninani hasa hakuna aijuae kesho yake Nimungut

Unabii wauongo huwezi niteteresha mm

Hakuna mwandamu anae weza ingilia mamlaka ya mungu hata maramoja yy mwenyewe haijui siku wala saayake
Nahawa ndio manabii wauongo

Walio tajwa navitabu vitukufu hakuna sehemu yyt kwenye kitabu chochote kile kinachoweka wazi kifo

Mtoa roho mwenyewe hajui hadi apewe order hivyo

Usinitishie mkuu

Naasimtabirie uongo mzee wawatu ilihali kifo kipo juu yauwezo wake

Kamaanatafuta kikk

Ataanzayy na kizazi chake
 
Huyu mjinga na shetani kama ameoneshwa kifo kwanini asimfate mzee mwenyewe amwambie bwana kamuonesha hivi hivo basi atengeneze njia zake vizuri yeye anakimbilia kwenye media kama siyo uwendawazimu ni nini hiki

Nabii Ezekiel alioneshwa mfalme Ezekiel atakufa akamfata private akamwambia sasa huyu Nabii gani anae expose public mambo ya eternity
Na namuomba Mungu mwezi huu ufe kabla haujaisha umedharirisha unabii Nabii wa uongo wewe
Nabii husemea kwenye ofisi yake ambayo ni madhabahuni.

Kama ambavyo Chadema husemea kwenye ofisi zao pale Kinondoni au Rais anasemea akiwa ofisini kwake pale Ikulu, au mkuu wa shule anaposemea jambo kwenye master parade.

Hio ilikuwa ni ibada ya kawaida, kwa hiyo sio vibaya kusema jambo kwenye ibada ya madhabahuni.
 
Back
Top Bottom