NABII TITO: Msifanye mapenzi mtapata laana

Anasema yeye na mkewe wanatazamana tu
Je yeye hakuzaliwa?
Je hana watoto?
Ana uhakika gani mkewe hapati msukumo wa kihisia?
Je ana uhakika gani kwamba mkewe haruki ukuta?
 
Hii nchi inashida gani aisee! Halafu hiyo content mbele ya watoto wadogo na mamlaka zipo zinachekelea tu.
 
Adai yeye na baby mama wake hawafanyi mapenzi - wamepata watoto kwa uwezo wa roho mtakatifu...
USHAURI WA MUHIMU SANA: tunaweza kubishana, tunaweza kufanya lolote katika haya majadiliano, lakini kumbuka kuwa Mungu alijidhihirisha kwetu kwa njia ya Yesu Kristo, na baada ya kupaa akatuletea Roho Mtakatifu, lakini katika hilo Yesu alituonya kuwa unaweza kumtukana au kumkufuru Mungu kwa nafsi yake yeyote ile ila ukimkufuru katika nafsi yake ya Roho Mtakatifu, hautasamehewa milele, manake umeshaandika tiketi yako ya motoni milele na milele. wengu tunaweza tukawa hatuamini aidha kwasababu sio wakristo au vyovyote vile, ila bora kuepuka hiki kitu isije siku moja ukagundua kilikuwa cha kweli na umeshakufuru.

MATHAYO 12:31 -32 inasema: Kwasababu hiyo nawaambia, kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa wala katika ule ujao.

sihukumu mtu, ina nashauri katika majibizano yeyote ya kidini ukiwa hapa duniani, au unapotafuta sifa au followers wako kwa namna yeyote, au unapotafuta umaarufu, uwe makini usijetenda dhambi isiyosameheka, ipo, ndio hiyo. kwenu ninyi ambao hamjaokoka, hivyo hivyo ulivyo Mungu atakupokea na atabeba mizigo yako yote, sali sala hii pamoja na mimi:

Eee Mungu wangu, mbele zako mimi ni mwenye dhambi, ninaamini ulimtoa Yesu Kristo alikufa kama kafara kwa ajili ya ukombozi wangu, naomba unisamehe, uniokoe kuanzia leo, mimi niwe mali yako, futa jina langu katika Kitabu cha hukumu, andika jina langu katika Kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo Yesu Kristo, Katika Jina la Yesu! Amen.

hivihivi kimchaezo mchezo umeshaokoka, acha dhambi, kimbia dhambi na jiunge na wale waliookoka ili mmwabudu Mungu pamoja. Ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom