Nabii M. Thomas: Lowassa atashinda uchaguzi mkuu wa Oktoba, Tanzania

Hamjastuka mpaka sasa kuwa huyo mchungaji ni mshirikina na kuna kila uwezekano kuwa huyo kaka'ke alimtoa kikoa?
 
Hata wasingetabiri ndo hivyo
inapendeza sana ikifikia hatua ya kuamini kupita hata imani aliyonayo mgombea hofu ni pale matokeo yanapokuwa kinyume kwa aaminie hivyo itabidi ale malimau
 
Kama watabiri wameshatuonyesha matokeo.. haina haja ya kwenda kupiga kura ni kulala miguu juu tu mpaka jioni kwenda kuona matokeo.
 
Mtawataja manabii wote mpaka Issa bin Maryam (as) lowassa hatashinda urais.kwa niliyoyashuhudia leo pale sheikh amri abeid aise jamaa anasubiri kuapishwa tu.
 
Nilishatamka na nitaendelea tena. Mimi nasema hivi: lowasa alishinda urais mwaka huu nitabadili jinsia
 
Zikiwa zimebaki siku 17 mwanga na nuru ushaanza kuangaza. Nabii M. Thomas kutoka nchini Kenya kaonyeshwa maono ya kwamba Lowassa atashinda katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 25.10.2015....... (K24, 5.9.2015)...

Nabii Thomas anakumbukwa sana kwa unabii wake kuhusu Uhuru Kenyata. Mnamo siku ya jumamosi tarehe 23.February. 2013 alisema kwamba Bwana kanena naye ya kwamba Uhuru Kenyata ni chaguo lake (Bwana) na atakuwa Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Kenya.
Kwa mara nyingine nabii huyo kasema kuna ishara nyingi ambazo kaonyeshwa za Lowassa kushinda katika uchaguzi huu na kwamba Lowassa atakuwa rais wa awamu ya 5 ya JMT..

Wimbi la manabii kuonyeshwa maono juu ya Edward Lowassa unazidi kushamiri. Ambapo mwaka juzi Nabii TB Joshua alionyeshwa maono. Na mwaka jana Nabii Mabumba wa Tanzania naye alitoa unabii wa Lowassa kuwa rais....

Mytake:... Chaguo la wengi, ni chaguo la Mungu!..... Uungwaji mkono anaopata Lowassa ni ishara tosha kuwa ni chaguo la Mungu....

hiv mpaka mda huu kuna mtu ambae hajui ukweli huu kuwa lowasa ni rais? Labda vichwa sisimiz
 
Mtawataja manabii wote mpaka Issa bin Maryam (as) lowassa hatashinda urais.kwa niliyoyashuhudia leo pale sheikh amri abeid aise jamaa anasubiri kuapishwa tu.

Mafuriko ya kufata wasanii... Mafuriko ya kusomba watu....

Hujaona video watu wanatoka baada ya show kuisha?.. Magufuli hashindi huu uchaguzi... NEVER
 
Uchaguzi huu hauitaji nabii yeyote kuzungumza chochote.....

Kama imeshakuwa imeshakuwa tu, haitaji nabii hapa...kwasababu hawa manabii wanaweza kusababisha watu kugawanyika ki-imani hivyo kukaleta taifa kugawanyika...

Manabii, watulie na utabiri wao...wachungaji/ maaskofu/ mashehe na viongozi wa dini, waendelee kuhamasisha amani na utulivu kwa waumini wao, bila kutumbukiza hisia zao kwenye haya mambo ya kisiasa.. Ili kuliwezesha taifa kuvuka hapa salama.

Ni kweli tunawaitaji, lakini pia hatuitaji watu wagawanyike kwa misingi ya kidini....itakayotokana na matamko yao..haijalishi inaendana vipi na kile ninachotaka kukisikia au mwingine anachotaka kusikia..

Matamko ya viongozi wa kidini yamekuwa yakichukuliwa vibaya sana na wanasiasa na hivyo kuhatarisha umoja wa kitaifa...

Wewe mbali na kutoa matamko....

Ila jamani shetani hawezi kuwa chaguo la Mungu. Manabii walikuwepo enzi hizo. Leo hii kuna vibaka tu na wafanyabiashara za kulevya tu.
 
Unabii ni nini ? Manabii wote walishakufa wako zao mbinguni. Duniani kuna washirikina tupu
 
Back
Top Bottom