SoC01 Naamka nikiwa na miaka 40, Mke wangu amekuwa msaada

Stories of Change - 2021 Competition

Memtata

JF-Expert Member
Jul 27, 2013
552
1,800
Nina miaka 40 sasa lakini ndio naamka nashtuka kuona kwamba nilipoteza sana muda, pesa na sikuutumia vizuri ujana wangu. Ningewaza haya mapema ningekuwa mbali sana kimaendeleo hata kama si kwa pesa nyingi lakini ningekuwa nimepiga hatua kubwa.

NINI KILINIPONZA?

1. UVIVU NA NJIA MKATO

Shule ya msingi niliamini elimu hiyo si ya muhimu na haina msaada wowote katika maisha. Sikufanya vizuri darasa la saba nikaenda secondary za binafsi.

Secondary pia niliona kusoma kote ni kujiandaa kufanya mtihani darasani na si maishani. Sikuwa na wazo la kupoteza miaka miwili tena baada ya kidato cha nne kisha niende chuo. Sikufanya vizuri pia nikaenda chuo cha ufundi – 18+ (nikiwa na zaidi ya miaka18)

Nikiwa VETA nikachukua fani ya uchomeleaji (welding & fabrication) fani hii ilikuwa ni ya nguvu na kuchafuka sikuvutiwa nayo sababu nilipenda utanashati nikaulizia wenzangu wa fani ya umeme wakanipa muongozo theory ilikuwa ngumu kwangu mi kichwa maji nikaona nikomae na fani yangu ya uchomeleaji japokuwa sikuipenda.

Miaka miwili nikamaliza grade II (sikuizi level II) nikaingia mtaani, nikajaribu kazi ya uchomeleaji nikaona ni kazi ngumu na inayodharaulika. Nilikuwa najihisi aibu watoto wakali wanione nimechafuka kwenye kijiwe nachomelea nikaona hainifai nikaachana nayo - 20+

Nilikusanya pesa kidogo nikaanza kusoma IT (Information & Technology) nikafanikiwa kupata certificate nikafungua kijiwe nikishirikiana na rafiki yangu fundi simu. Siku moja ndugu yangu akaja kuniomba niungane naye kwenye ofisi yake ya uwakala wa kukusanya kodi za majengo (property tax) nilikubaliana nae japokuwa maslahi hayakuwa mazuri lakini niliona ni kazi isiyoumiza kichwa.

Wakati huu niliondoka nyumbani nikaenda kupanga chumba kimoja ndani nikiweka kitanda 5x6, sofa la watu wawili, jiko la mchina (miaka hiyo majiko ya gesi bado) na kitrey cha ngazi nne kikiwa na vyombo vichache. Kuna wakati nilikuwa nikiangalia chumba changu niliona maisha naelekea kuyaweza.

Ofisi hii ilianza kukua jamaa aliongezewa eneo la ukusanyaji kodi pia alipata kibali cha court broker. Siku moja akanishirikisha mipango yake mikubwa ya baadae na kunishauri nikasomee finance na store hata certificate tu ili nifanye kazi kwa ufanisi, nikamkubalia nikaanza masomo kwenye chuo binafsi hapo hapo mjini huku nikiendelea na kazi ada akilipia yeye.

Miezi mitatu ya kwanza nilianza kuona masomo magumu nikawaza nasoma ili iweje wakati tayari nakipato niliona kama napoteza muda nikaanza utoro darasani.

2. SIKUJUA KAMA WAKATI NI SASA
Nilipokuwa kwenye hii ofisi posho zilikuwa za kutosha boss hakunisahau kila alipopiga kazi ya maana lakini sikuona umuhimu wa kununua kiwanja au kuanzisha mradi wowote zaidi ya kurembesha gheto. Niliongeza TV ya chogo (wakati huo flat hakuna) na meza yake nikanunua na kabati ya nguo hapa niliona maisha nimeyamaliza kabisa – 23+

Sikumoja nikiwa bar na rafiki zangu jamaa yangu mmoja akanishirikisha mishe zake na kuniambia jinsi zinavyomlipa. Jamaa alikuwa na kampuni ya General Supplies na alikuwa anachukua kila tenda aliyoona ina faida, siku hii aliniomba kama nna muda nikamsaidie kazi zake kwenye mashirika ya wakimbizi kwa muda wa wiki moja niliona ni fursa nikaungana nae siku iliyofuata, ofisini nikiaga nimepata matatizo ya kifamilia.

Huku sasa mambo yalionekana mazuri zaidi siku tunamaliza kazi jamaa akaniwekea mpunga wa maana kwenye akaunti yangu. Nilipofika mjini palikuwa hapatoshi ilikuwa ni pombe na wanawake, vijana tuna kauli yetu moja ya kijinga kwamba ‘ni bora ule bata bado kijana kuliko kusubiri uzeeke’.

Nilikuwa na zaidi ya wiki sijaenda ofisini wala darasani, boss akaanza kunitafuta sikupokea simu yake na sikutaka kuonana nae akakata tamaa hakunitafuta tena. Mi sikujali nikaendelea na mishe na jamaa yangu.

Siku zikasonga nikawa mzoefu kwenye kazi nilipiga kazi na kutafuta tenda za maana. Mambo yalianza kubadilika sikumoja jamaa kalipwa vizuri baada ya juhudi zangu nikasubiri mgao wangu kama ilivyo ada lakini sikuambulia kitu nilipomfata akaanza kunielezea shida za familia yake roho iliniuma sana lakini sikuacha kushirikiana naye. Huu ulikuwa mwanzo jamaa aliendelea kunidhulumu au kunilipa pesa kiduchu baada ya kazi nzito, nilikata tamaa nikaamua nirudi mjini.

Nilipigwa vumbi kwa siku kadhaa, sikumoja nikakutana na mhasibu wa shirika moja tulilowahi kufanyanao kazi akanijulisha kuhusu kazi fulani, nilimwambia kama nimeshatengana na jamaa akaniambia atanisaidia kazi hii niifanye mwenyewe. Kweli jamaa akanipa mwongozo nikatafuta kampuni ya mtu nikapiga kazi vizuri na malipo mazuri yakafanyika nikamtoa kidogo mwenye kampuni kisha mpunga uliobaki nikaweka kwenye akaunti yangu.

Nilifanikiwa kusajili kampuni yangu nikaanza kupiga kazi na bata maisha yakawa mazuri. Lakini bado sikuwa na wazo la kujenga au kununua kiwanja niliona muda bado nitanunua tu, zaidi nilihamia nyumba ya vyumba viwili na kila kitu ndani nikaongeza vitu vyote vya ndani. Nakumbuka sikumoja kaka yangu alikuja kunitembelea alikuta tunafunga flat TV inch 42 ilikuwa kabla ya 2010 wakati huo hapo kijijini nnapoishi TV hizi hazikuwepo kabisa zaidi ya kwenye hoteli moja kubwa ya kitalii. Bro alishangaa sana akaniuliza bei nikamwambia akazidi kushangaa na kunihoji kwanini sijapeleka hiyo hela kwenye ujenzi, wakati huo hajui kama hata kiwanja sina!! – 30+

Miaka michache baadae mashirika ya wakimbizi yakafungwa baada ya wakimbizi kurudishwa kwao hali ikawa mbaya sana, tenda zilikosekana na nikafulia sana hadi kufikia kuanza kuuza baadhi ya vitu vyangu. Mrija mmoja umekatika sina pa kushika nikarudi kwa jamaa yangu fundi simu kupiga kazi za ufundi computer, nilipata shida sana sababu nilizowea maisha ya juu, nikaamua kuchukua mkopo bank kwa dhamana ya nyumba ya kaka yangu. Nikaboresha ofisi nikaongeza na huduma ya stationery. Mambo hayakuwa mazuri sababu sikuwa mtunzaji mzuri wa fedha, kwasiku nikiuza laki natumia 30,000 sikujua kama kuna wakati kwenye 100,000 faida ni 10,000 tu.

Mtaji ukayumba sababu kubwa ni kutokuwa na uzoefu, matumizi mabaya ya fedha na kutaka kuishi maisha ya juu. Miezi sita ya mwisho nikashindwa kumalizia marejesho nyumba ya kaka ikataka kuuzwa bahati nzuri kaka alikuwa vizuri akanipiga tafu akamalizia mkopo. Mimi nikarudi chini hadi kufikia kula mlo mmoja kwa siku.

3. SIKUJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA
Baada ya kupigwa na maisha kwa muda nikabahatika kupata kazi ya kuajiriwa kwenye shirika binafsi nikilipwa mshahara mzuri ukilinganisha na elimu yangu, fani yangu na nilipotoka. Ilikuwa ni mji tofauti na nilipotoka, maisha niliyokuta wenzangu wanaishi yalinishangaza pamoja na kulipwa vizuri lakini waliishi nyumba zenye wapangaji wengi wakichukua chumba kimoja au na sebule tu, waliishi maisha ya kawaida na walijibana japokuwa walikuwa na umri chini ya miaka 30. Mimi sikutaka niishi maisha haya nilichukua nyumba nzima ya kisasa sikujali gharama sababu niliona naimudu. Bata ziliendelea kama kawaida wakati huu niliona yale yaliyonishinda kufanya wakati ule huu ndio muda wake lakini elewa haikuwa kujenga wala kununua kiwanja au kuanzisha mradi wowote – 33+

4. MFUMO DUME

Niliona umri umeenda nikaamua kuoa, nikaoa binti ambaye hatukuwahi kuwa na mahusiano naye kabla. Kuna ujinga mmoja nilifundishwa na jamaa yangu kwamba mke akiwa mpya mzoweshe tabia zako mapema ili asikushike, basi mimi wiki ya pili tu baada ya ndoa nikarudi usiku saa 9 nikiwa chakari na huu ndio ukawa utaratibu kila baada ya siku chache. Mke alinuna mwisho wa siku akajilazimisha kukaa kimya japokuwa hakupenda.

Nikiwa kwenye ndoa sikutaka mke wangu ajue kipato changu, apange bajeti au kuingilia mipango yangu ya pesa, mambo yote ya pesa nilifanya mwenyewe na alipolalamika sikujali kabisa. Kuna wakati bajeti zinagoma kabisa sababu ya starehe zangu na kujikuta naenda kukopa mikopo umiza ilimradi kuziba pengo hatakama jambo si la muhimu.

Mwaka 2018 hali ikawa ngumu sana madeni yakaongezeka mshahara wote unaishia kwenye madeni kisha nakopa tena kuziba pengo. Mpango ukawa hivyo hadi ikafika wakati madeni yakakutana ikashindikana kulipa, usumbufu wa wadeni ukaleta msongo wa mawazo na usononi (depression) hadi kufikia kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Pamoja na kushindwa kwangu lakini bado sikumshirikisha mke wangu.

Siku moja nikiwa chumbani mawazo tele nikawaza zaidi ya miaka 20 natafuta na sijafanikiwa, nikampigia kaka kumuomba ushauri. Kaka alinishauri mengi ila maneno yake ya mwisho ndio nayaishi sasa:

“Mafanikio yako ni yako na familia yako, kipato ni siri lakini si kwa mkeo. Umeshindwa kusimamia au umekwama mshirikishe mkeo”

Nilifikiria sana majibu haya ya ndugu yangu kwanini simshirikishi mke wangu kwenye kipato na bajeti ya familia? Sikupoteza muda siku hii hii nilimwita mke wangu tukaongea nilimuomba msamaha na kuomba tushirikiane kwenye kuijenga familia na maendeleo yetu. Wakati hili linaendelea nilianza kumjenga mke wangu ajue sisi ni kitu kimoja, nachofanya ni kwaajili yetu na anachofanya ni kwa maendeleo yetu na kila mmoja ana jukumu la usimamizi.

Mke wangu amekuwa msaada mkubwa sana kwangu kila mwezi nashirikiana naye kupanga kulingana na nilichoingiza tunaamua sasaivi tujibane wapi na tufanye kipi, sasa naona kabisa mwanga, katika bajeti tuipangayo hakuna bajeti ya bata ila pesa kidogo ya kujikimu (pocket money) na pamoja na shida zote nimefanikiwa kununua kiwanja na natarajia kuanza ujenzi hivi karibuni. Wakati huu wale wenzangu waliokuwa wamepanga katika vijumba vya ajabu wameshahamia kwenye mijengo yao ya maana na hawana madeni.

Sikatai wapo watakaopingana na mimi kuhusu kumshirikisha mwenzi wako kipato chako lakini mimi binafsi imenisaidia sana naamini bila ushirikiano huu inawezekana hadi leo bado ningekuwa na maisha yale ya kisela.

Leo ndio naamka lakini naimani sijachelewa – miaka 40!
 
Mke wangu amekuwa msaada mkubwa sana kwangu kila mwezi nashirikiana naye kupanga kulingana na nilichoingiza tunaamua sasaivi tujibane wapi na tufanye kipi, sasa naona kabisa mwanga, katika bajeti tuipangayo hakuna bajeti ya bata ila pesa kidogo ya kujikimu (pocket money) na pamoja na shida zote nimefanikiwa kununua plot na natarajia kuanza ujenzi hivi karibuni. Wakati huu wale wenzangu waliokuwa wamepanga katika vijumba vya ajabu wameshahamia kwenye mijengo yao ya maana na hawana madeni.

Sikatai wapo watakaopingana na mimi kuhusu kumshirikisha mwezi wako kipato chako lakini mimi binafsi imenisaidia sana naamini bila ushirikiano huu inawezekana hadi leo bado ningekuwa na maisha yale ya kisela.

Na ulevi uache.
 
hujachelewa mkuu.Kwanza BATA UMEKULA la KUTOSHA so ni sawa kabisa ukianza kufocus kwenye Familia.Ama sio.All the Best.
 
Life begins at 40.

Endelea kukomaa na mkeo .

Unaweza kuja tusua pakubwa kuliko hao wengine kikubwa usijiweke kwenye nafasi zao yaani usijifananishe nao utakuwa unajidharau.

Focus kwenye ujenzi Kisha hamia kwenye miradi.

Achana na pombe Kama unataka starehe nunua kuku na kreti la soda au chupa za wine mbili peleke home kanywe na mkeo imetoka Hadi mwezi ujao.

Hujachelewa Sana

Kuna mmoja ndio anaanza kujenga nyumba at 60
 
Ushauri wa maana sana huu, Asante sana mkuu
 
Mkuu.. pole sanaa kwa yaliyo kukuta hii ume iandika kama ushuda na Funzo kwa sisi ambao tunapambana na maisha..! Ila nilicho jifunza kikubwa sanaa japo sija oa ila nta anza prosess za ujenz ata vyumba viwili tu kama mungu ata nijalia Ahsante
 
Asante mkuu, ni wazo zuri sana kama umeelewa nilichokosea mimi "sikujua kama wakati ni sasa"
 
Mkuu.. pole sanaa kwa yaliyo kukuta hii ume iandika kama ushuda na Funzo kwa sisi ambao tunapambana na maisha..! Ila nilicho jifunza kikubwa sanaa japo sija oa ila nta anza prosess za ujenz ata vyumba viwili tu kama mungu ata nijalia Ahsante
Kitu kingine cha msingi; Usianze kujenga nyumba ndogo kwa matarajio ya kujenga kubwa baadae maana unaweza kujikuta umeishia kujenga hiyo maisha yako yote maana itafikia wakati majukumu yanakuwa mengi alafu utawaza kama ni nyumba unayo ni bora uhangaike na vitu vya msingi na sio nyumba tena hadi kuzeeka na kijumba chako cha kuanzia maisha.

Ushauri wangu: Kama una uwezo anza na nyumba ya familia angalau vyuma vitatu na kila kitu ndani ila kama hauko vizuri kwa sasa unaweza anza na hiyo ndogo ya kuanzia maisha.

Nakushauri hivi sababu nimeona baadhi ya rafiki zangu walianza hivi na hadi leo bado wameishia hapo hapo.
 
Ume niongezea kitu kizuri mkuu...ila kwa tunaofanyia kazi maeneo ya chaka tunachelewa sana kujenga ila ntajitahid nitafte raman nzuri ya vyumba vinne au vitano then nianze tathimini ya msingi then nta panda mdogomdogo
 
Back
Top Bottom