Naacha rasmi kusaidia wenye uhitaji


hilo sawa kabisa japo sio wote, nakumbuka kuna mtu hivyohivyo japo uwezo nimemzidi sana kuna siku after 1 year nikampigia as a friend hakupokea hata simu, siku nyingine nikakutana naye akawa na haraka ila psycholocally nikamsoma nkamwambia napenda tu tukapate kinywaji wengine ndo hivyo nshawasahau kabisa.

all in all lengo nikupata company tu ya kupiga story weekend but ndo hivo na wapo wanaoshukuru ila huwa nawaambia hicho kidogo wasaidie wasiojiweza mtaani kwako au peleka kanisani!!!!
 
Kuna mdau kakuuliza swali zuri sana, wewe ulitaka wakulipe nini??!! Usidhani hawataki kukulipa, lakini wanakulipaje ndiyo ishu. Inawezekana washafanya/wanafanya kitu ambacho wao wanatafsiri ni kukulipa wewe hung'amui kwa kuwa una tafsiri yako. Kama vipi wakati wa kuwapigia hayo unayoyaita mapande muwekane sawa kabisa nini unategemea kutoka kwao; kama kweli unahitaji kulipwa!
 
Hao unaowasaidia ni jinsia gani? Na pia kama unasaidia wewe saidia tu, kurudisha fadhila ni moyo na roho ya mtu mwenyewe.
 
Kuna jamaa mwingine humu alikuja na stori kama hii hii na mbwembwe kibao lakini baada ya kuusikiliza upande wa pili ikaonekana kumbe jamaa ndiye kimeo.

Mkuu,Too much expectations huishia kwenye disappointments tu siku zote.
 

Kama unaweza kuwasaidia kwa njia hiyo ni vizuri zaidi ila sio kuwa nao kila siku.
 

shutuma zako hazina ukweli wowote mkuu; sasa inakuwaje tena niombe fedha kwa mtu niliyemsaidia kupata nafasi ya kutengeneza kipato. kama inatokoea nakutana na hizo nafasi badala ya kuomba ningekamata fursa na kupiga mwenyewe. roho mbaya tu na kujisahau. i wish ningeweka wazi kila detail ila ni ngumu.

binadamu tuna hulka ya kujisahau. hilo tu. sihitaji fedha wala lolote ila nachogusia hapa ni behaviour za wahusika baada ya kufanikiwa.

mfano kabla hajapata nafasi mawasiliano hua mazuri na approach pia ila akishatoka all of a sudden hutamsikia tena.
 

Kama unaweza kuwasaidia kwa njia hiyo ni vizuri zaidi ila sio kuwa nao kila siku.
 

Tulivyomaliza chuo nilibahatika kupata kazi mapema sasa pale ofisini wakawa wanahitaji mtu mie nikaona ngoja nimvute mshkaji lakini huwezi amini huyo mshkaji wangu ndio ilikuwa sababu ya mimi kufukuzwa kazi sababu ya majungu yake! kuna watu na viatu!
 
Kuna mmoja nilimtoa humu jf,tulibadilishana contacts nika muekekeza sehemu ya kazi akakutana na boss wake.sijawai kumuona na wala hajawai kuniona.alivyopata hiyo kazi hata asante tu ilimshinda huwa napata habari zake tu kutoka kwa boss wake...!!
 

Umenena vyema...
 
Mkuu shukurani inakuja wakati ukiwa hutegemei. Ukishaidai hiyo sio shukurani tena bali malipo kwa ulichofanya.
 

Zekidon,nakushauri tuliza mori kwanza.
Hao hata kama hawatakukumbuka basi Kizazi chake kitakukumbuka.
Maisha ni dynamic kama Lowasa,kuna siku yanaweza kuwageukia then wakaona hakuna pa kwenda zaidi ya kuja kwako.
We vuta subira tu,ila endelea tu kuwaombe maisha mema na kazi njema.
Mungu humbariki sana anaewaombea mema wenzio hata kama kuna tofauti za kimaisha.
 
Mi huwa naona misaada bora nipeleke kanisani
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…