Elli
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 55,502
- 86,050
Juzi nimefurahi na kusikitika, hii ni baada ya TBC1 kutangaza kuwa mara baada ya taarifa ya habari Rais atahutubia taifa kufuatana na utaratibu wake wa "kuhutubia Taifa kila mwezi". Nilianza kushtuka kusikia neno hilo "kuhutubia Taifa kila mwezi" maana ni miezi kadhaa imepita sijamsikia. Taarifa ikaisha hakuna lolote hadi mida ya saa nne au tano hii kucheki ndio nakuta anahutubia.
Japokuwa hotuba yake haikuwa na jipya wala mvuto ila nilishangazwa na mambo kadhaa, moja; kwanini ahutubie Taifa muda huu ambapo tulikua tunaingia kwenye uchaguzi wa Igunga? pili, Ni suala la raisi kututangazia taifa zima kuwa kaenda kupokea medali ambayo ni heshima kwa Taifa. Hapa napo sikumwelewa kabisa raisi huyu.
Kwa Ufupi alipaswa kuzungumzia hali halisi ya nchi kiuchumi na kubwa suala la umeme, mfumuko wa bei, udini alioupalilia na mkakati gani kuhusu vijana wetu waliokosa mikopo huku wachache wakifaidi mikopo hio, lakini pia angetoa sababu za kueleweka kuhusu kucheleweshwa kwa salary za watumishi wake wa umma, tupo katika kipindi kigumu cha maisha so kutuambia suala la medali HAISAIDII hata kidogo maana kama ni medali tumezikosa kwenye michezo ambayo ndio ingekua sahihi kuzipata huko hizi za kisiasa ni upotevu wa muda na kuleweshwa madaraka ya kisiasa.
Swali langu ni hili; Je mwezi huu utahutubia tena? Kama ni kweli utaratibu wako wa "kuhutubia Taifa kila mwezi" basi uje na hoja zenye mashiko na maana kwa mustakabali wa taifa na sio usubiri hadi kuwe na events fulani fulani ili upate nafasi ya kuwatisha wananchi waichague CCM yako.